XGirlfriend wangu anamambo!!!!

XGirlfriend wangu anamambo!!!!

EnockM

Member
Joined
May 31, 2014
Posts
35
Reaction score
1
katika hali ya kawaida mnapo kuwa wapenzi mambo mbalimbali hufanyika mnapo kuwa wapenzi na kupelekea kupeana zawadi mbalimbali.

nilikuwa na mpenzi wangu ambaye ilikuwa yaelekea tuwe wachumba siku zote alijifahamisha kuwa yeye anafanya kazi ya afisa mikopo midogo midogo katika taasisi moja kubwa ya fedha hapa nchini na kupelekea kuwa ananipatia fedha hizo mara kadhaa na wakati mwingine mwingine namrudishia

katika hali isiyo ya kawaida kwangu na kwake mara ya mwisho kiasi cha tzs laki 4 sikuweza kukirudisha kwa sababu zilizo mbali na uwezo wangu kilichofuata hakika sikutegema na ukijumlisha kuwa penzi limekufa
- amepiga simu na kutuma msg kwa kila mtu niliyemtambulisha hasa ndg zangu na rafiki zangu wote wa karibu kuwa nananidai fedha na zawadi kede kede za wakati wa penzi letu moto moto
- aendelea mbele kusema kauli tata za uchonganishi {kuwa nilimwambia kuwa kaka yake amelala na yeye na pia nilimwambia mama yangu anamtoto nje}
- aliweza kuwa na access ya akaunti yangu ya benki na ivo kutangaza details za akaunti hiyo
- anatambwe nyingi haswa nakupeleka mahakamani navidhibitisho vyote ivo atashinda!!!!
baada ya hayo
- nilikwenda taasisi hiyo ya fedha na kukuta kuwa binti huyu sio mwajiriwa ila ni dada yake ndio mwajiriwa ivo taasisi hiyo inaendelea kufanya uchunguzi je ni nani anayempatia nyaraka za siri na kutoa nje ya utaratibu!!!
- bado message za tabwe kunitishia kunishitaki zinazidi sana kutumwa na kuniita mfa maji haachi kutapatapa na jambo usilo lijua ni sawa na usiku wa giza


KWA MUSTAKABALI HUO NAJUA HUMU KUNA WATU WA AINA MBALIMBALI NIPATIE USHAURI UNAOFAA
NB; KAMA HUNA LA KUCHANGIA JUST LEAVE IT!!!
 
Unahitaji ushauri gani kijana?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Duh ilo furushi ulilokuwa umeliokota halikufai, nyamaza usifuatilie chochote kuhusu mambo anayoyafanya atanyamaza tu mwenyewe. Mith26:4 km mkristo
 
Jifunze kuandika Kiswahili fasaha ndugu.

Ndo ukome kabisa kubebwa na wanawake,simama kama mwanaume.
 
Mlipe hela yake ili asiwe na sababu ya kuwasiliana na wewe
 
ushaur gani unataka? toa hela ya watu.
 
Mlipe alichokuwa anakupatia nadhani hataendelea kukusumbua
 
Sijaelewa hapo zaidi ya kuona Laki 4 tu
 
Duh ilo furushi ulilokuwa umeliokota halikufai, nyamaza usifuatilie chochote kuhusu mambo anayoyafanya atanyamaza tu mwenyewe. Mith26:4 km mkristo

asante sana ndugu yangu kwa ushauri mzuri sana tena wenye mashiko, tangu nianze kuingia humu ndani wewe n i wa kipekee sana, Mungu akutie nguvu
 
Back
Top Bottom