HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,569
Hbr wana MMU?
Ktk kipindi hiki cha mwisho wa mwaka pamoja na shamra shamra za x-mas na mwaka mpya, nilikuwa nimejipanga kupata muda wa kumshukuru Mungu kutulinda mwaka huu wote na kutuepusha na mabalaa na kisha kupata wasaa wa kuzunguka na marafiki zangu kadhaa sehemu mbali mbali za kuvutia na kuenjoy maisha!
Lakini kumbe mipango, si matumizi! Tar 23 nilipata taarifa kuwa mama yetu mdogo alikuwa akitoka mkoani kuja Dar akiwa na msichana wa kazi kuja kushehereka nasi na sikukuu za mwisho wa mwaka. Treni lilipofika pande za Dom ikasimama kwa ajili ya abiria kushuka na wengine kupata mahitaji mawili matatu kabla ya kuendelea na safari. Ma mdogo naye alishuka kwa ajili ya kununua vitu viwili vitatu, lakini bahati mbaya alianguka ghala. Aliwahishwa hosp kuu dom na kupelekwa ICU lakini baadaye alipoteza maisha. Manesi walifanya jitihida kuwasiliana nasi kupitia simu yake kupitia namba zilizohifadhiwa huko na kufanikiwa kutupata.
Tulifanikiwa kumsafirisha kuja Dar na tulizika tar 26. Tunashukuru kwa umati wa watu waliojitokeza kutufariji. Hii ilituthibitishia kuwa alikuwa mtu wa watu.
Mwenzenu niko chini bado naendelea kuomboleza kwa tukio hili zito lililotukuta. Pia nafikiria kumbukumbu aliyojijenga juu ya msichana huyu wa kazi aliyeondokewa na mwenyeji wake akiwa safarini asijue wapi pa kwenda na nini cha kufanya. Mungu amfariji pia kwa magumu yaliyomkuta. Nitumie muda huu pia kuwapa pole wana JF wote walipoteza wapendwa wao mwaka huu wa 2012. Mungu aendelee wakuwafariji na kuwatia nguvu.
Nilichojifunza:
Maisha ya mwanadamu ni kama maua, asubuhi yanachanua na jioni yananyauka. Hivyo basi, ni vyema kwa kila mtu kwa imani yake kuishi ktk maisha ambayo yanampendeza Mungu wake. Tujitahidi kutenda yaliyo mema, na pia kuwa tayari kusamehe na kusahau mabaya tuliyotendewa. Hii uitasaidia tunapokutana na tukio kama hili tuweze kuagwa vyema na kuacha kumbukumbu njema kama wapendwa wetu walivyoagwa. Tunapousogelea mwaka 2013, tuusogelee tukiwa na mitazamo wa kutokuwatenda watu mabaya. Tujitahidi kuishi kwa amani huku tukikwepa vurugu za kidini, kuacha ufisadi, rushwa na mabaya mengine yote yanayofanana na hayo. Pia tuwe wavumilivu kwa wanaotutenda mabaya na kuwareport kwa vyombo husika badala ya kuchukua sheria mkononi.
Nawaombea dua Mungu awalinde na kuwavusha na mwaka huu wa 2012 na hatimaye tuingie mwaka 2013 tukiwa na afya njema. Nawatakia baraka, mafanikio na ushindi ktk kila mfanyalo.
Wenu ktk maombolezo,
HorsePower
Dec 2012.