WU Tanzania na ukusanyaji wa taarifa za watu.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WU Tanzania na ukusanyaji wa taarifa za watu..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 28, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kuna mabadiliko yamefanyika kwenye Western Union Tanzania ambapo sasa mtu kukutumia fedha kutoka Bongo hawezi kufanya hivyo isipokuwa hadi utoe taarifa zako za huko uliko (nchi unayotumiwa). Hii ni kwa mujibu wa maelekezo ya Benki Kuu ambayo WU(T) wamebandika katika vituo vyao.

  Kwa hiyo mnaotumiwa fedha kutoka Bongo mjiandae kwa invasion mpya ya privacy. Mimi leo imebidi nitoe hadi jina la kijiji ninachoishi ili kuweza kupata vijisenti vyangu vya madafu!

  Cha kushangaza sisi tunaotuma fedha nyingi zaidi kutoka sehemu kama Marekani kwenda Bongo tunazituma bila kulazimishwa kutoa taarifa za yule tunayemtumia, kazi yake, nambari yake ya passport, kijiji chake n.k!
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Kuna kipindi nilishindwa kununua kitabu kupitia rafiki yangu aliye marekani kwasababu hizohizo maana walinitaka wajue ni nani ninayemtumia zile fedha na yeye hakuwa tayari niwape hizo details zake. Nia yao ni ndogo tu. Monitoring!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  yaani inakera kabisa nadhani tunakoelekea kwenye uchaguzi mkuu tutaona mengi sana.. hasa baada ya Gavana kudai kuwa watu walio nje ya nchi ndio wana lengo la kumchafua sasa wanakuja na huu upuuzi.. Kama sisi tunaotuma hadi dola 1000 bila kuulizwa tunamtumia nani huko Bongo iweje mtu anayetuma vijisenti vyake kwa mwanae kule Uganda atakiwe kupata hadi namba ya passport ya mtoto?
   
 4. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hii yote ni katika uchaguzi unaokuja, wanataka kuwafahamu WTZ wote walio nje na shughuli zao kwani mumewakalia kooni na hivi sasa wine haipiti vizuri kooni.

  Shida moja kubwa hivi wanashindwa vipi kuthibiti Capital Flight inayotokea Tanzania?
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Oh yeah....mtu akiwa anatuma hela kutoka bongo kwenda let's say Marekani, jamaa (Western Union) wanataka jina, immigration status (visa, green card, citizenship) na taarifa kama hizo za mtu anayetumiwa hela. It's very annoying wakati mtu aliyeko Marekani anaweza kutuma hela bongo kupitia Western Union kutoka kwenye comforts za nyumbani kwake kwenye kompyuta!!! Hakuna hata haja ya kwenda dukani na kujaza ile mifomu yao....ni click mbili tatu tu kitu na boksi
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa kweli wamenishangaza sana; sasa angalu wangekuwa wanafanya kama hapa Marekani ambapo ukituma zaidi ya dola 1000 ndio wanataka taarifa ZAKO wewe zaidi. Sasa mbongo anataka kumtumia shemeji yetu mdogo kule Kampala anaambiwa aeleze hadi wazazi wa binti wanafanya kazi gani huko! mnataka kuvunja ndoa za watu?
   
 7. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2009
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Vipi tena wanataka kufanya kazi ya Immigration ya Marekani? Tutaona mengi kabla ya uchaguzi.
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  It is pathetic melancholy fallacy.
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hii misheria yao ya kijinga jinga wanalala na kuamkia kushoto na kujiwekea, wanajisahau itakuja kuwaliza wao wenyewe na ndugu zao!

  Basi hapo wao wameona wamewiiiiiin kichizi kuwakomoa wakina Mwkjj, kina Tumain na akina Rev. Kishoka huko ng'ambo.... little do they know that infrastructure za IT kumonitor flow za hela in and out ya nchi ziko flawed. It only takes three entities to bypass everything. Isitoshe atatokea jamaa mmoja au hata haya makampuni mengi ya nje yaliyowekeza hapa Bongo kwenye finance sector kuleta service ambayo itaifanya hiyo ridiculous monitoring kuwa redundant.

  While they've got a valid case katika kupunguza money laundering na sponsorship ya terrorism, but their approach is more punitive wala haina maana pale mtu mwenye dola 500 anapokuwa treated the same way na yule mwenye kutuma dola 10,000 kwa mkupuo. As always, people will find other means to accomplish the deed now that we sort of have reverted to the communism era.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli mtu utumie Western Union au Moneygram ku launder money? Lol....
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ask them, am dead sure they'll pass that as one of the reasons behind this gimmick!
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Dec 28, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Oh I'm sure that could be (one of) the rationale behind it...but I'd like to think that If one wants to launder money, then they would use more sophisticated means than Western Union or Moneygram...
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Na Nyumba ya Gavana wa fweza watajengea nini? Akili yao yato ipo pale pale kwenye ufisadi na kunyonya kila kitu na kumwacha mwanachi akiwa mtumwa na mkimbizi nchini kwake.
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Idea ya ku-control pesa kutoka nyumbani ni nzuri, tatizo ni hiyo method wanayo-impose kuitumia..........

  BoT wawe wanatoa kibali kwa anayetaka kutuma pesa nje ya nchi....ofcourse with a limit in relation na kipato cha mtumaji
   
 15. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MMJJ,
  Usilikuze sana hili maana sio jipya. WU wamekuwa na sheria ngumu kwenye baadhi ya nchi walishawahi kutakiwa hata kuacha kutoa huduma, kama sijakosea South Afrika, Namibia, Dubai ni baadhi ya hizo nchi.

  Lakini so far Money Gram wao kwa vile volume yao ya biashara ni ndogo, bado masharti yao ni madogo sana. Next time watumie na hutaulizwa chochote hata test question haihitajiki.

  Punguzeni pressure, sio kila jani ni nyoka.
   
 16. TingTing

  TingTing Member

  #16
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Hii ilinitokea wakati nipo Dar nilipotumwa na Bosi wangu kumsaidia kwenda kutuma hela kwa mwanae asomaye Australia. Nilishangaa sana vitu nilivyoambiwa nikabidhi wakati hapo nilikuwa na passport yangu na lesseni pia. WU wakasema niwape copy ya Visa ya huyo wa Australia, Original letter ya Shule kuonyesha yuko Shule etc. Kuuliza why all requirements naambiwa ni sheria za BOT. Kilichotokea hapo….ilibidi tu nisepe zangu kurudi ofisini maana kungekuwa hamna tofauti na Moneygram (MG).

  Hapo ndipo tunapokosewa na viongozi wetu katika mambo ya upokeaji na utumwaji wa pesa. Sidhani kama kuna mtu atakuwa tayari kwa hilo kutoa information/details za mwenzake haswa kama hela inaenda nje ya Tanzania. MG na WU za nchi za watu unatuma hela kupitia net, unabofya pale halafu unasubmit hapo unakuwa unangojea mpokeaji akupe taarifa kuwa ameipata sawasawa. Isitoshe unaweza enda tuma hela hata supermarket au vijiduka tu vya kawaida kama ilivyokuwa kuwa kwa vijiduka vya M-PESA vile. Yaani service full available everywhere.  Yaani hata hujakosea Mkuu…ishanitokea hiyo sana tu haswa kwangu ni wakati naagizia kitabu amazon.com cha fani yangu pale ambapo CRDB Visa Card ilipogoma yet tunaambiwa kuwa “YOU CAN BUY ANYTHING ONLINE WITH YOUR NEW CRDB VISA ATM CARD”. Nimefuatilia naambiwa eti hadi ujaze fomu za kukubaliana matumizi ya ATM online. Duh…..nimejiuliza bila kupata jibu…kwani walipoleta kadi mpya za ATM si lazima taarifa ilibadilika hususan katika matumizi na masharti yake. Iweje tena unatakiwa kujaza mifomu wakati ulishaanguka kidole katika mikaratasi yao mingi isiyo na maana hata. Hao viongozi wetu mtazamo wangu sidhani wana nia nzuri bali naona wanataka wawe wanaiba wenyewe tu huku wakitupumbaza sie walalahoi kwa kutuwekewea masharti katika masuala ya kutuma hela nje ya nchi kwa wale wanaoweza.


  Ukweli ni kuwa masharti haya wamechemsha sana na sijaelewa ni kwa nini wamekuja nayo haswa. Ukienda bank kutumia EFT (Electronic Fund Transfer) basi hapo ndipo masharti chungu nzima. Nakumbuka kuna kipindi mdogo wangu alikuwa anatakiwa kutumiwa hela ya haraka ili alipie fees na accommodation pia bila hivyo chuo watamtema ikiwa na kufukuzwa hostel, duh…tukatumia postal bank kumtumia hela bwana weee…kwanza ilichukuwa muda zaidi ya wiki moja kutuma hiyo hela hapo chini tu South Africa, pili hawakutuma Fax chuoni ya risiti ya EFT, tatu..gharama yao ya kutuma hela ilikuwa juu sana tena wanaquote in dollars na kila bank ina gharama zake kumbuka. Siku nipo Mwanza dogo anapiga simu kusema shule hawajapata Bank EFT risiti ya malipo. Nilichukuwa jukumu la kuwapigia simu TPB na kuwajia juu sana tena wakakataa kutuma ile risiti ya EFT chuo (EFT Advice Note) nikawaambia kuwa namtuma mtu aje kuichukua hapo TPB HQ pale TTCL MAwasiliano House aitume kwa fax na kwa gharama zake.

  Money laundering haiwezi kufanywa kinamna hiyo ikionekana waziwazi halafu kwa hela ndogo ndogo si rahisi. Bank za Kenya zina gharama sawa za kutuma hela kwa EFT (Swift Transfer) ya KES1,500 isipokuwa Barclays tu ndio wanachaji KES2,000. Katika bank zote za Kenya, Diamond Trust Bank walinishangaza sana kwa kunifungulia akaunti pending submission ya barua ya ref, barua ya ofisi na copy ya passport. Katika ATM mteja ndiye mwenye kuchagua kiasi cha fedha anachotaka kiwe limit ya kutoa kwa siku ingawaji limit yao ni KES35,000 kwa siku. Wakati nataka kumtumia pesa tena mdogo wangu kwa Western Union imfikie haraka, wakanishauri kuwa nitumie Swift Transfer ambayo ni cheap (@KES1,500) compare na WU ambayo ni % fulani ya hela unayotaka kutuma. Walinihakikishia kuwa inafika chini ya dakika 10 na dogo atakuwa kaipata…kumbe kweli. Zote hizi zilifanywa kwa simu na risiti ya swift transfer nilienda kuichukua baada ya wiki ingawaji ilikuwa tayari baada tu ya kutuma.

  Hivyo sie Tanzania, viongozi wetu ndiyo wanatupoteza halafu wanasema wanamonitor hela na ku-control biashara ya hela kwa upande mwingine. Vyote hivyo ni Tanzania tu pekee yake ndipo vipo. Vizingiti vya kila haina hadi kwa wazawa.
   
 17. TingTing

  TingTing Member

  #17
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Dar Express wao wanafanya kazi kama hii tu na wala hawahitaji vitu vingi wala maswali mengi. Unakatwa aslimia 10 ya hela unayotuma ambayo ni constant kwa hela yoyote unayotaka kutuma kwenda kokote ambao mabasi yao yanaenda. Akamba nao wanafanya hiyo business, Vodacom kupitia M-Pesa lakini nchini tu na Zain's Zap. Sasa sijui mabenki na vituo vya kutuma hela ndiyo vimebanwa pekee au inakuwaje. Maendeleo ya nchi yanatakiwa yawe "both ways" na barriers ziwe zimetolewa ama kurahisishwa ama kulegezwa kwa lengo la kuweza kunyanyua maendeleo ya nchi. Kuna baadhi ya watu mie nawajua ambao solution kwao ni kwenda kutuma hela nje ya nchi Nairobi maana hamna vizingiti kwa hela hizi za kawaida tu toka kwa watu wa kawaida na kwa matumizi ya binafsi, masomo, matibabu ama maisha. Viongozi wajue tunafukuza wawekezaji wadogo wadogo ambao ni wenye kushika uchumi haswa zaidi ya hao wakubwa wakubwa.
   
 18. TingTing

  TingTing Member

  #18
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tukisema kuwekwe sheria kulingana na kipato cha mtu itakuwa unfair kwa wengine ambao hawana kipato in maana hawaturusiwa kutuma hela hata ikitokea wakipata. Nadhani BOT watoe notice kwenye gazette kuhusu kiasi cha fedha mtu anaweza tuma nje ya nchi kwa yeyote yule awe na kipato au lah bila masharti na kikizidi limit pia waseme ni nini vitahitajika kabla ya hela kutumwa na kituo husika cha kutuma fedha nje ya nchi. Lengo ni kuweka usawa pande zote kwa mwenye kipato na asiye na kipato. Hii itarahisisha sana baadhi ya mambo haswa katika suala zima la kutuma na kutumiwa hela toka nje ya nchi.
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kweli, labda inahusiana na hii sheria mpya ya Election Financing ambayo wanataka kuipeleka Bungeni mwezi ujao
   
Loading...