Written Interview inavyopukutisha wataalamu

Cvez

JF-Expert Member
May 19, 2018
4,345
13,078
Kutokana na ukosefu wa ajira na wingi wa wasomi, imepelekea kua na mlundikano mkubwa wa wahitaji wa kazi kuliko uhitaji. Mathalani kada moja unaweza kuta nafasi moja lakini kuna waombaji zaidi ya 100.

Hapa changamoto inapoanza huwezi kuongea na watu 100. Hivyo kuna haja ya kuwachuja ubakiwe na watu kama 5 hivi ili uweze kufanya nao usaili wa mazungumzo. Hapo ndio written Interview inavyopukutisha watu, maana kufeli written Interview haimaanishi wewe ni kilaza. Unaweza kukuta huyo aliefeli written ana uzoefu mkubwa wa kazi plus vyeti vizuri zaidi ila ndio hivyo hakufanikiwa kupita.

Dogo fresh from school anakunyoosha vizuri na kupita oral huyoo anapata mchongo. Mfano nafasi kama hizi za Tutorial Assistant dogo katoka shule halafu hajawahi fanyia kazi field yake halafu anarudi tena kuzalisha wataalamu wengine hali ya kua yeye hajui chochote zaidi ya kusoma notes. Mwengine ana 3+ years ya experience na good certificates ila ndio hivyo kashaliwa kichwa.

Ila ndio hivyo hamna namna lazima watu wapunguzwe.​
 
Nje ya mada kidogo.
Hivi kwa ujobless uliopo kwa sasa, experience unaitoa wapi? Au kujitolea na intership unaiongeza kwenye experience?

Halafu kuna tetesi ya mitihani ya utumishi kuvuja!
Na pia kuna tetesi za watu kupitishwa! Inakuwaje mnapiga written watu 1000 mitihani inasahihishwa kwa siku moja na Matokeo yapostiwa fastafasta, sio kupanga watu wao?
 
Kutokana na ukosefu wa ajira na wingi wa wasomi, imepelekea kua na mlundikano mkubwa wa wahitaji wa kazi kuliko uhitaji. Mathalani kada moja unaweza kuta nafasi moja lakini kuna waombaji zaidi ya 100.

Dogo fresh from school anakunyoosha vizuri na kupita oral huyoo anapata mchongo. Mfano nafasi kama hizi za Tutorial Assistant dogo katoka shule halafu hajawahi fanyia kazi field yake halafu anarudi tena kuzalisha wataalamu wengine hali ya kua yeye hajui chochote zaidi ya kusoma notes.​
Marks ni kipimo cha kujua vitu
Tutorial Assistant huchukuliwa mwenye.marks za juu sana.Ujue.kafunfishwa na maprofesa tofauti tofauti.s bado kuonyesha uwezo wa juu kufaulu kila somo
Huwezi chukua mbumbumbu toka mtaani lifundishe chuo kikuu!! Mfano yeye ni fundi magari makubwa mzuri ana experience ya Miaka 20 huwezi mpeleka akafundishe.motor vehicle Engineering!! Kule funga kazi magari yote mtu anafunzwa hadi yale digital yanayoenda bila dereva!! Na uzoefu wake atakwama sababu kabobea eneo moja tu

Ndio maana Vyuo huajiri vipanga wenye akili waliofaulu vizuri masomo yote kila angle kwa ufaulu wa juu mno
 
Utumishi kuna mambo meng mengine hayaelweki uhalisia wake na nini knapelekea wawe na maamuzi hayo...sisi tuliletewa pepa aihusiani na hiyo position lakn ndo hivyo hakuna namna tukafnya waliopita wakapita....lakni it's not fair na mambo kama haya ndio yanaibua hisia kwmba kuna hila nyingi utumishi ktk kuendesha mchakto wa ajira
 
Inakua 50 kwenda juu ingawa mkifaulu sana wanachukua waliofaulu zaidi.
Nimeuliza hivyo maana juzi kati nilifanya interview sehemu, nilipata 63.1, wawili wa juu walipata 74 kwa 72, waliitwa hao wawili pekee.

Nikaongea na mhusika mmoja wa mahali hapo akasema, utumishi pass mark yao ni 70 na ikitokea hakuna aliyefikisha 70 inabidi nafasi itangazwe upya.
 
Back
Top Bottom