ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,265
- 4,452
Yumkini mnaposoma waraka huu basi huenda sip nanyi kimwili ili kiroho nitakuwa nanayi daima.Nilijitenga nanyi pamoja na mama yenu kwa sababu ya usalama wenu.Sikutaka kuwaweka hatarini kwani ninyi ndio tumaini liliobaki la taifa hili.Nimerudi Tanzania hata baada ya niny kunisihi sana nisirudi.
najua mnaanza maisha mapya huko ugenini mlipo na kwamba kwa sasa nyie ni watalii tu lakini baada ya muda najua mtaitwa wakimbizi na nina hakika mtapitia changamoto.Mimi nimerudi Tanzania leo,siku mbili kabla ya tarehe tuliyopanga.Nimefikia huku kwenye nyumba yetu ambayo mnajua haikuuzika hata baada ya kushusha bei sana.Niko na mama yenu mdogo pamoja na mdogo wenu wa mwisho ambaye nafikiri ninao uwezo na wajibu wa kuwalinda hawa pia.
Wanangu,mimi baba yenu ni kijana mdog sana na katika umri wangu huu na nguvu zangu nina wajibu kwenu na kwa taifa langu.Nina wajibu wa kuhoji,kulalamika na hata kuandamana ili nihakikishe taifa langu linaendelea kuwepo.
Najua hawawezi kunikamata wala hawana uwezo wa kuniua wala kunijeruhi.najua kuwa hata kwa jitihada zao hawataweza kuua mawazo haya na tumaini tulilo nalo ya kwamba wakati wa mabadiliko ni sasa.
Wanangu,nina ndoto juu ya taifa letu.Nina ndoto ya taifa la haki,la watu wasio waoga wanaotii sheria.Imani hiyo ndiyo inayonifanya nishiriki katika wito huu wa maandamano ya kuhakikisha kuwa viongozi wetu,tunaowalipa kwa kodi zetu,na kuwachagu wenyewe wanatuheshimu.
Sitaki kizazi chetu kihukumiwe na historia.Sitaki siku moja watoto wetu waseme wazee wetu walikuwa waoga nchi ikavurugwa.Nataka hata nikifa,nife nikijua kwamba nilikuwa sehemu ya waliosimama kupinga udhalimu katika taifa letu.Najua hata nisiposimama,kama ni wa kufa basi nitakufa ndio maana najianda kuishi pamoja nakufa.
Nikiishi naishi kwa kristo na nikifa nakufa kwa kristo.Nasikitika kwamba wengi wasio na hatia ambao ni kama Akwilina watakufa bila hata kushiriki moja kwa moja katika harakati,nina hakika laiti wangekufa kwa kuwa walishiriki basi jina na haki ya o ingesimamiwa,lakini tazama AKWILINI amekufa na waliomdhuluma uhai wake wako mtaani na hakuna anayefuatilia.
Tumechoka,nimechoka.Niwaambie wanangu,kama nikifa basi nitakufa kwa sababu sahihi.La nisipokufa basi nawahakikishi kuwa nitakuwa mwiba mchungu kwa watesi wetu na kwamba nitatumia uwezo na karama zote nilizojaliwa na Mungu kuhakiksha kuwa nchi yetu inaondoka mikononi mwa wasio haki madhalimu.
Wanangu.Pembeni ya pesa kidogo nilizompatia mama yenu,kuna pesa zingine nimehifadhi katika akaunti yangu ambayo mama yenu anaijua basi muitumie pesa hiyo vizuri iwapo sitakuwepo.Nikiwepo basi nitaitumia kuhakikisha kuwa taifa letunlinakuwa huru na watanzania tunatembea kifua mbele bila kuogopa vitisho vya wasio haki.
Mueendelee kuniombea niwe salama na jasiri ili nishiriki katika safari hii kwa ukamilifu.tafadhali msinitafute mpaka nitakapowatafuta mwenyewe
Nawapenda sana,Mnisamehe iwapo mtaona uamuzi wangu huu sio sahihi