Wosia aliouacha prof Muhongo mmeuelewa?


Wewe unajua hayo ya Norway na USA, tuulize ya bongo tukupe za kibongobongo
 

Sasa huyo Muhongo wenu mbona hajaweka wazi mkataba hata mmoja wa gesi tumpime kama sio dalali wa wazungu. Legacy ingekuwepo kama angeweka mikataba wazi tujue nani dalali na nani mzalendo. Huyu mzee kavuna aibu ya mwaka
 

sidhani kama kuna haja ya kwenda kutafuta hiyo sera, wala mimi au mtu yeyote aliye against na muhongo ana shida na sera za gesi.. kwani kilichomfanya ajiuzuli ni sera za gesi??? kila mtu anajua hata wewe unajua... mbona tunataka kudanganyana mchana jamani..
 

Je, alikuta tanesco ina deni la sh.ngapi na sasa ni sh.ngapi?
 

Mhongo alikuwa na Kikwete Uswiss mpango wake wa kujiudhuru ulifanywa collaboratively na Kikwete ili kuwater down nguvu ya kuandikwa vibaya na kwa kweli ilifanya kazi kwa sababu vyombo vya habari frontline ilikuwa mawaziri na sio kujiudhuru kwa hiyo
 

Mkuu inaonekana una uchungu sana juu ya kuondoka kwa kwa Prof lakini ukisoma kwa makini utajua huyo Meela kasema ukweli mtupu. Prof yawezekana alikuwa nafanya vizuri kwenye kazi zake pale wizarani lakini kwa hili la ESCROW hakubahatika kulisimamia vyema hivyo kuondoka kwake ni haki na hakuonewa na mtu yeyote.

Jambo la ajabu ni watu kusahahu kuwa ni huyu Prof aliyekataa mikataba iwekwe wazi jambo hili halina tofauti na yale tuliyokuwanayo kwenye mikataba ya madini alafu badaye wanajaribu kutudanganya eti ni mikataba mibovu kwavile hatukuwa na uzoefu. Watanzania amkeni, mikataba mibovu tunayoingia sasa na tuliyoingia wakati ule si sababu ya ukosefu wa uzoefu bali ni wizi kwa wale waliokuwa na dhamana ya watanzania na yote hayo ni asante kwa koti la usiri ule ule aliokuwa ameanza kuukumbatia Profesa Muhongo.

Vile vile naamini si Vyema kumuhukumu Simbachawene hata kabla hajamaliza wiki ofisini, hizo hisia za lazima waziri awe na utaalam wa wizara husika si za kweli kwa uzoefu wetu hapa Tz. Wasomi wengi ndo wametuingiza kwenye maafa makubwa ya kifisadi. Ngoja tumpe nafasi waziri mpya na tutamuhukumu kwa utendaji wake!


 
People need chance to prove themselves I too believe in that viewpoint however 'Simbachawene' was there before at the time when things were run in a manner of business as usual according to the ministry culture of the time; where by order of the day was being incompetence, signing shady contracts which led to national energy deficiency and grand corruption which permeated the ministry and its subsidiary institutions.

Sasa uwezi kumrudisha mtu ambae ulishampa nafasi na hakufanya chochote kubadilisha walau jinsi ya kusimamia utekelezaji wa sera kwa ubora wachalia mbali technical reasoning on what is best for the nation. Mikataba inaweza isiwekwe wazi kwa sababu ya madai ya usiri wa mwekezaji ingekuwa miaka ya nyuma ningekuwa na wasiwasi zaidi kumbuka Prof Muhongo ame introduce measures za kwamba wawekezaji watachukua 25%-35% only based on the level of reserves found on each plot.

Kuna swala la kusambaza umeme unajua tunadhani Tanesco/wizara ya nishati; tu ndio inasaidiwa ilihali kuna wizara luluki pia zina miradi ya kimataifa na bado impact wananchi hawazioni hata kama millenium project imechangiwa kiasi kikubwa na fedha za kigeni kupitisha umeme, lakini Prof alifuatilia kwa karibu maendeleo ya mradi kwa ukaribu kwa Tanzania ni mawaziri wachache sana wanaofatilia miradi yao kwa karibu.

Kuna mengi Prof kafanya kujaribu kubadilisha wizara mengine ni kwa sababu tayari kakuta kuna mikataba iliyokuwa imekaa, kumbuka pia ni yeye ndio wakwanza kusema gharama halisi za kuzalisha umeme wa mafuta na kwanini Tanesco inaendeshwa kwa mikopo, serikari ifidie gharama za uzalishaji na kulazimisha ubadilishaji wa mafuta kwenda kwenye gesi, in short mimi binafsi ata kama ningejua jamaa kweli kachukua hela ningemwita pembeni nikwamwambia rudisha hiyo hela nitafute namna ya kumlinda ikibidi wengine wawe scapegoats on the reasoning what he offers is more beneficial to the nation than what he took or mistakes he made.

Anyway lets see what the new team brings on the table.
 

Kwani ingekuwaje kama tungesomesha hao watu kwanza kisha ndio tukaingia kwenye business ya kuchimba gesi? Si tungefaidika sana kwa kuwa na resources zetu badala ya kuwapa watu kazi hiyo huku sisi wataalam ambao ndio tunaanza kuwasomesha sasa wakibaki wanaangalia kwa pembeni tu? Kama nchi nyingine zimeweza kusomesha wataalam wao na kisha kuwatumia katika kuvuna rasilimali zao, kwa nini Tanzania tumeng'ang'ania kusema kuwa madini, gesi au mafuta hatuwezi kuvivuna sisi wenyewe hadi tuwape wageni? Ni kweli kwamba tukiwa na nia ya dhati hatuwezi kusomesha na kupata wataalam pamoja na zana za kufanya shughuli hiyo kwa faida zaidi hata kama itakuwa baada ya miaka 15? Tuna haraka ya nini? kwani madini, gesi au mafuta visipochimbwa (kuvunwa) leo au kesho vitapotelea huko ardhini?

Hilo ni swali nimekuwa nikijiuliza maana miaka yote. Tokea uhuru hatujajenga uwezo wa ndani katika kuvuna madini yetu matokeo yake tumekuwa tukiwagawia 'bure' wageni na sisi tunaambulia vyumba vya madarasa tu. Mafuta na gesi vimegunduliwa, sasa tumewapa wageni vile vile kwa kisingizio kuwa hatuna elimu wala nyenzo. Suala la kujiuliza ni je, tukiitafuta hiyo elimu na hizo nyenzo makusudi kwa miaka kama 15 au 20 hatuwezi kuvipata? Au ndio ile kila mmoja anataka aje na mipango yake ya zima moto ili aonekane amefanya kitu fulani na ahalalishe kuteuliwa au kuchaguliwa tena awamu inayofuata? Huko ni kukosa mwelekeo kama taifa. Naona serikali daima inapanga mipango ya maendeleo ya miaka miwili au mitano tu. Isingekuwa hivyo, nina hakika hadi sasa tungekuwa tayari tuna uwezo wa kuvuna madini, gesi na mafuta sisi wenyewe kama tungepanga mipango ya muda mrefu tokea uhuru. Nchi kama Korea zilizokuwa masikini kama au kuzidi Tanzania mwaka 1960 sasa hivi ndizo tunakimbilia kuomba misaada ya teknolojia. Wao wameondokaje pale tulipokuwa na sisi tumebakiaje pale miaka zaidi ya 50? AIBU!
 

Kiongozi yeyote anapotekeleza majukumu yake huo sio msaadabali ni wajibu wake kwani ndio dhamana aliyopewa na wananchi. Kuondoa mgao waumeme au kufanya lolote lile ambalo ni ndani ya wajibu wake hakuondoi uhalaliwa kuwajibika anapokosea sehemu nyingine.

Yaani apige dili ya udalali na Singasinga halafu aachwe tukwa sababu hakuna mgao..!! Akili za wapi hizi?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…