Wosia aliouacha prof Muhongo mmeuelewa?

Kwa tunaoelewa mambo Muhongo yupo sahihi. Norway ilipopata mafuta haikukabidhi wazawa kuendesha uchimbaji, ilileta wa USA, ila ilichokifanya ni kusomesha watu wake (pia kufungua vyuo vya Trondheim na Stavanger university) ili kusomesha wataalam. Ilichokifanya ni kuwa na umiliki kupitia serikali. Ilipofika kipindi wakaona labour force inatosha waliwafukuza wa USA na serikali kupitia STATOIL wakaendea na uchimbaji na wazawa wanachofaidi ni supporting industries (mfano vyakula, repairs za mitambo, ulinzi etc). Hiyo model iko pia uarabuni etc. sasa kwa nchi kama Tanzania hao akina mengi hawana ubavu na niwabinafsi. Model ilioichukua serikali ni sahihi, na uzuri mikataba ilishatiwa sahihi hakuna wa kubadilisha.

Wewe unajua hayo ya Norway na USA, tuulize ya bongo tukupe za kibongobongo
 
Prof. Muhongo atabaki kuwa mtu ambaye ameitendea haki nchi hii kwa kusimamia vyema wizara yake. Ameleta mabadiliko makubwa sana kwenye idara ambazo zipo chini ya wizara. Ameingia kuna mgawo wa Umeme wa kufa mtu, watu wanapiga dili za udalali wa kuuza majenereta, leo maduka ya majenerata hakuna.

ni bahati mbaya sana kwamba mafisadi wa vitalu, waliokuwa wakiinyonya TANESCO, mafisadi wa mafuta , mafisadi wa elimu (nakumbuka siku anataka kusoma matokeo ya mtu bungeni) wamefanikiwa kumumaliza. Ila ametuonyesha kwamba mgawo ulikuwa wa kutengeneza na mafisadi hawawezi tena kuingilia hapo.

Sasa huyo Muhongo wenu mbona hajaweka wazi mkataba hata mmoja wa gesi tumpime kama sio dalali wa wazungu. Legacy ingekuwepo kama angeweka mikataba wazi tujue nani dalali na nani mzalendo. Huyu mzee kavuna aibu ya mwaka
 
Ninakushauri, pengine na wadau wengine wasiofahamu, utafute, usome na kuielewa sera ya Tanzania ya gesi asilia ambayo Prof. Muhongo aliasisi, kuisimamia na baadaye kupitishwa na Baraza la Mawaziri dhidi ya upinzani mkali wa Benki ya Dunia. Baada ya hapo urudi JF kuposti juu ya Muhongo. Tafadhali mdau yeyote asi-comment hapa kabla ya kusoma sera husika.

sidhani kama kuna haja ya kwenda kutafuta hiyo sera, wala mimi au mtu yeyote aliye against na muhongo ana shida na sera za gesi.. kwani kilichomfanya ajiuzuli ni sera za gesi??? kila mtu anajua hata wewe unajua... mbona tunataka kudanganyana mchana jamani..
 
Prof. Muhongo atabaki kuwa mtu ambaye ameitendea haki nchi hii kwa kusimamia vyema wizara yake. Ameleta mabadiliko makubwa sana kwenye idara ambazo zipo chini ya wizara. Ameingia kuna mgawo wa Umeme wa kufa mtu, watu wanapiga dili za udalali wa kuuza majenereta, leo maduka ya majenerata hakuna.

ni bahati mbaya sana kwamba mafisadi wa vitalu, waliokuwa wakiinyonya TANESCO, mafisadi wa mafuta , mafisadi wa elimu (nakumbuka siku anataka kusoma matokeo ya mtu bungeni) wamefanikiwa kumumaliza. Ila ametuonyesha kwamba mgawo ulikuwa wa kutengeneza na mafisadi hawawezi tena kuingilia hapo.

Je, alikuta tanesco ina deni la sh.ngapi na sasa ni sh.ngapi?
 
Uhuni aliofanya Muhongo leo hata Mimi niliwahi kuufanya pale Vwawa, nilimpiga jamaa nikamtoa manundu halafu nikakimbia fasta kwenda kushtaki polisi. Jamaa alipopata nguvu na kwenda kushtaki akakuta tayari askari wanajipanga kwenda kumkamata. Ndio ya Muhongo leo, alijua fika kuwa anapigwa chini na mawaziri wapya wameitwa kuapishwa, akawahi kuitisha press conference kabla ya muda wa Ikulu kuzuga kuwa amejiuzuru. Tujiulize, je asingejiuzuru angebakia kwenye baraza jipya? Je hao mawaziri wapya walioapishwa walipewa notice ya masaa manne kati ya kujiuzuru Muhongo na kuapishwa kwao?

Mhongo alikuwa na Kikwete Uswiss mpango wake wa kujiudhuru ulifanywa collaboratively na Kikwete ili kuwater down nguvu ya kuandikwa vibaya na kwa kweli ilifanya kazi kwa sababu vyombo vya habari frontline ilikuwa mawaziri na sio kujiudhuru kwa hiyo
 
Ni wapi CAG au TAKUKURU aliposema Muhongo anausika? Yeye mwenyewe kasema waende kwenye mabenki na watafute alipopewa hela popote.

Halafu inashangaza sana serikari inapotaka kutufanya sisi mapimbi eti achukue group responsibility kwa maamuzi aliyoyafanya ya kuachia hela zitoke, what the F#@K aliesema hela za escrow zilipwe ni wizara ya nishati au shauri la mahakama baada ya kusikiliza kesi za wabia na kuamua kumalizana, hapo tena waziri analipi la kupinga.

Some people would have to pay the price na matendo yao one day kwa kuwapotosha watanzania na kuwalazimishia umaskini. Unaenda kupoteza mtu makini it must be said kwa sababu za kithenge sana, sijapata kuona upuuzi kama huu duniani. Hivi unadhani watu wawe wanatumia a lot of efforts kupotosha jamii na wewe ukae kimya tu halafu utegemee wananchi wakuelewe kwa majibu yako yenye long gaps? halafu unasema ni maamuzi ya yanayotokana na maazimio ya bunge mbona hilo bunge alikugusia ni nani alietoa shauri la malipo ambapo ni mahakama yetu.

Uitaji kuwa smart kujua Simbachawene wizara si size yake kuna wizara za kufurahishana huko sijui kwenye mavazi na sanaa na sehemu zingine ni vitega uchumi vya taifa avitaki mtu yeyote zaidi ya professa mwenye experience na hayo mambo it is simple as that.

Escrow ni kwa sababu waziri aliyeileta miaka ya tisini hakuwa makini leo mali zote zinazogundulika kwenye madini unamweka simbachawene waziri wa wizara muhimu hivyo mtu ambae ajui lolote kuhusu haya mambo hata kama TPDC kuna kipanga lakini walau waziri awe na level fulani ya competence, tumesahau haraka mikataba mibovu ya huko Geita, dowans, IPTL, songas and the like; stupid Tanzania government.

Mkuu inaonekana una uchungu sana juu ya kuondoka kwa kwa Prof lakini ukisoma kwa makini utajua huyo Meela kasema ukweli mtupu. Prof yawezekana alikuwa nafanya vizuri kwenye kazi zake pale wizarani lakini kwa hili la ESCROW hakubahatika kulisimamia vyema hivyo kuondoka kwake ni haki na hakuonewa na mtu yeyote.

Jambo la ajabu ni watu kusahahu kuwa ni huyu Prof aliyekataa mikataba iwekwe wazi jambo hili halina tofauti na yale tuliyokuwanayo kwenye mikataba ya madini alafu badaye wanajaribu kutudanganya eti ni mikataba mibovu kwavile hatukuwa na uzoefu. Watanzania amkeni, mikataba mibovu tunayoingia sasa na tuliyoingia wakati ule si sababu ya ukosefu wa uzoefu bali ni wizi kwa wale waliokuwa na dhamana ya watanzania na yote hayo ni asante kwa koti la usiri ule ule aliokuwa ameanza kuukumbatia Profesa Muhongo.

Vile vile naamini si Vyema kumuhukumu Simbachawene hata kabla hajamaliza wiki ofisini, hizo hisia za lazima waziri awe na utaalam wa wizara husika si za kweli kwa uzoefu wetu hapa Tz. Wasomi wengi ndo wametuingiza kwenye maafa makubwa ya kifisadi. Ngoja tumpe nafasi waziri mpya na tutamuhukumu kwa utendaji wake!

People need chance to prove themselves I too believe in that viewpoint however 'Simbachawene' was there before at the time when things were run in a manner of business as usual according to the ministry culture of the time; where by order of the day was being incompetence, signing shady contracts which led to national energy deficiency and grand corruption which permeated the ministry and its subsidiary institutions.

Sasa uwezi kumrudisha mtu ambae ulishampa nafasi na hakufanya chochote kubadilisha walau jinsi ya kusimamia utekelezaji wa sera kwa ubora wachalia mbali technical reasoning on what is best for the nation. Mikataba inaweza isiwekwe wazi kwa sababu ya madai ya usiri wa mwekezaji ingekuwa miaka ya nyuma ningekuwa na wasiwasi zaidi kumbuka Prof Muhongo ame introduce measures za kwamba wawekezaji watachukua 25%-35% only based on the level of reserves found on each plot.

Kuna swala la kusambaza umeme unajua tunadhani Tanesco/wizara ya nishati; tu ndio inasaidiwa ilihali kuna wizara luluki pia zina miradi ya kimataifa na bado impact wananchi hawazioni hata kama millenium project imechangiwa kiasi kikubwa na fedha za kigeni kupitisha umeme, lakini Prof alifuatilia kwa karibu maendeleo ya mradi kwa ukaribu kwa Tanzania ni mawaziri wachache sana wanaofatilia miradi yao kwa karibu.

Kuna mengi Prof kafanya kujaribu kubadilisha wizara mengine ni kwa sababu tayari kakuta kuna mikataba iliyokuwa imekaa, kumbuka pia ni yeye ndio wakwanza kusema gharama halisi za kuzalisha umeme wa mafuta na kwanini Tanesco inaendeshwa kwa mikopo, serikari ifidie gharama za uzalishaji na kulazimisha ubadilishaji wa mafuta kwenda kwenye gesi, in short mimi binafsi ata kama ningejua jamaa kweli kachukua hela ningemwita pembeni nikwamwambia rudisha hiyo hela nitafute namna ya kumlinda ikibidi wengine wawe scapegoats on the reasoning what he offers is more beneficial to the nation than what he took or mistakes he made.

Anyway lets see what the new team brings on the table.
 
Kuna watanzania kibao tu wapo Trondheim na Stavanger University huko Norway. Pia kuna watanzania kibao tu wanasomea uhasibu wa mafuta na mlimani kwa mfano kuna intake ya wahasibu, hr, marketing itafanyika karibuni sema logistic hazijakamilika, hiyo yote ni Muhongo!

Kwani ingekuwaje kama tungesomesha hao watu kwanza kisha ndio tukaingia kwenye business ya kuchimba gesi? Si tungefaidika sana kwa kuwa na resources zetu badala ya kuwapa watu kazi hiyo huku sisi wataalam ambao ndio tunaanza kuwasomesha sasa wakibaki wanaangalia kwa pembeni tu? Kama nchi nyingine zimeweza kusomesha wataalam wao na kisha kuwatumia katika kuvuna rasilimali zao, kwa nini Tanzania tumeng'ang'ania kusema kuwa madini, gesi au mafuta hatuwezi kuvivuna sisi wenyewe hadi tuwape wageni? Ni kweli kwamba tukiwa na nia ya dhati hatuwezi kusomesha na kupata wataalam pamoja na zana za kufanya shughuli hiyo kwa faida zaidi hata kama itakuwa baada ya miaka 15? Tuna haraka ya nini? kwani madini, gesi au mafuta visipochimbwa (kuvunwa) leo au kesho vitapotelea huko ardhini?

Hilo ni swali nimekuwa nikijiuliza maana miaka yote. Tokea uhuru hatujajenga uwezo wa ndani katika kuvuna madini yetu matokeo yake tumekuwa tukiwagawia 'bure' wageni na sisi tunaambulia vyumba vya madarasa tu. Mafuta na gesi vimegunduliwa, sasa tumewapa wageni vile vile kwa kisingizio kuwa hatuna elimu wala nyenzo. Suala la kujiuliza ni je, tukiitafuta hiyo elimu na hizo nyenzo makusudi kwa miaka kama 15 au 20 hatuwezi kuvipata? Au ndio ile kila mmoja anataka aje na mipango yake ya zima moto ili aonekane amefanya kitu fulani na ahalalishe kuteuliwa au kuchaguliwa tena awamu inayofuata? Huko ni kukosa mwelekeo kama taifa. Naona serikali daima inapanga mipango ya maendeleo ya miaka miwili au mitano tu. Isingekuwa hivyo, nina hakika hadi sasa tungekuwa tayari tuna uwezo wa kuvuna madini, gesi na mafuta sisi wenyewe kama tungepanga mipango ya muda mrefu tokea uhuru. Nchi kama Korea zilizokuwa masikini kama au kuzidi Tanzania mwaka 1960 sasa hivi ndizo tunakimbilia kuomba misaada ya teknolojia. Wao wameondokaje pale tulipokuwa na sisi tumebakiaje pale miaka zaidi ya 50? AIBU!
 
Prof. Muhongo atabaki kuwa mtu ambaye ameitendea haki nchi hii kwa kusimamia vyema wizara yake. Ameleta mabadiliko makubwa sana kwenye idara ambazo zipo chini ya wizara. Ameingia kuna mgawo wa Umeme wa kufa mtu, watu wanapiga dili za udalali wa kuuza majenereta, leo maduka ya majenerata hakuna.

ni bahati mbaya sana kwamba mafisadi wa vitalu, waliokuwa wakiinyonya TANESCO, mafisadi wa mafuta , mafisadi wa elimu (nakumbuka siku anataka kusoma matokeo ya mtu bungeni) wamefanikiwa kumumaliza. Ila ametuonyesha kwamba mgawo ulikuwa wa kutengeneza na mafisadi hawawezi tena kuingilia hapo.

Kiongozi yeyote anapotekeleza majukumu yake huo sio msaadabali ni wajibu wake kwani ndio dhamana aliyopewa na wananchi. Kuondoa mgao waumeme au kufanya lolote lile ambalo ni ndani ya wajibu wake hakuondoi uhalaliwa kuwajibika anapokosea sehemu nyingine.

Yaani apige dili ya udalali na Singasinga halafu aachwe tukwa sababu hakuna mgao..!! Akili za wapi hizi?
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom