Worthless Degrees From Fake Colleges in the UK

Guys Academic competency hasa MBA ukitaja tu institution uliyosoma then waliosoma MBA wanajua who you are hsa huku ughaibuni. An MBA ni expensive Course kuliko masters zingine. At least will cost you £10,000 na kuendela. ukiambiwa 3000 au 4000 umeliwa utamaliza kihiyo!
 
Maarifa: I think you are not well informed check the tuition fees for Master Degree Programmes in International Trade anywhere in the world. They cost higher than that you better revisit your archives.
 
Hivi wakuu naombeni mniambie mwenye kujua status ya online degrees! Kuna jamaa yangu anafanya MBA online, lakini mpaka sasa hivi mimi kwa kweli sina imani na degree ya kwenye keyboard!
 
Hivi wakuu naombeni mniambie mwenye kujua status ya online degrees! Kuna jamaa yangu anafanya MBA online, lakini mpaka sasa hivi mimi kwa kweli sina imani na degree ya kwenye keyboard!
Mkuu na mimi niliuliza hapa,hizi degree kwangu mimi siziamini amini,si mnakumbuka ile degree ya Mhesh Mrema.
Chuo gani kinachotoa degree online inayotambulika kimataifa?
 
Hiyo degree ya Mh Mrema kama nakumbuka vizuri ni ya chuo cha Pacific Western University. Kuna watu wanawazodoa wasomi wa Mzumbe University na VC wao Warioba ambao pia wana PhD kutoka chuo hicho. Inaelekea kuna namna fulani ya kutokikubali chuo hicho pale Bongo.

Tukirudi kwenye on-line degrees, zinaweza kukubalika kama utaratibu wa chuo husika unawezesha wanafunzi kusoma genuinely na kupata instructions na assessment ambazo kimsingi zina ubora sawa na wale wanaosomea chuoni. On-line degrees ni mfumo uleule wa Open University, tofauti iliyoongezeka hapo ni teknolojia ambayo inaharakisha mawasiliano baina ya wanafunzi na chuo. La muhimu ni kujiunga na chuo ambacho kiko accredited na mamlaka husika kutoa distance education, kama Tanzania kuna HEAC ambayo inashauri watu kupata kutoka kwao inventories za vyuo kabla hawajaamua kujiunga. Kwa hapa UK kuna board inayohakiki distant learning, na zote zimewekewa standards, na mara kwa mara wanafanya quality checks.

Kwa hiyo distance learning inakubalika kama njia mbadala ya kupata elimu ambayo ni convenient kwa mwanafunzi na ni bei nafuu, japo huchukua muda zaidi kuliko campus-based learning. Cha maana cha kuzingatia ni reputation ya chuo unachotaka kujiunga nacho, na accreditation, mambo ambayo ni muhimu pia hata unapotaka kujiunga na campus-based course.
 
Kithuku,
Ujue zilikuwepo Pacific Western University mbili, moja California na nyingine Hawaii, sasa ile ya Hawaii bomu walishapelekwa mahakamani na nadhani ilifungwa ndio hiyo iliyokuwa inatoa Ph.D za ajabu ajabu; ile ya California iko approved na State ya California(not accredited na say WASC though) kutoa nadhani bachelors tu tena kwenye fani mbili kama sikosei. Sasa Mrema alihitimu PWU ya wapi na baadhi ya wahadhiri wa Mzumbe na kwingineko walisoma ya wapi?

Online degrees ambazo ziko accredited zipo halali kabisa ila inabidi kuwa vigilant kujua accreditation ipi inatambulika na Department of Education ya US, la sivyo utajikuta unalizwa na tapeli kajichimbia kwenye basement yake anaprint sheepskins bandia.
 
Nakubaliana na wote ambao tunapiga vita hizi shahada zinazotolewa kiholela na hizi shule ambazo hazina baraka ya wizara za elimu katika nchi zinazohusika.

Tukumbuke pia kuna shahada zisizofaa zinatolewa kwa watu wasiofaa ambao wanaendelea kuwapo miongoni mwa wenzao kwa muda unaokubalika (wanabebwa) katika shule zinazokubalika zenye baraka na vibali vya wizara zao za elimu.

Hata hivyo, kwangu mimi binafsi, ninachokijali zaidi, sio shule uliyokwenda au mwalimu aliyekufundisha wala vitabu ulivyosoma bali wewe umetoka na nini hapo kichwani mwako na unakitumiaje hicho ulichotoka nacho kwa manufaa yako na jamii?

Shahada sio muhimu, wewe mwenye shahada ndio muhimu.
 
Kwaminchi, maneno mazito hayo nami nakubaliana nayo mia kwa mia.

Napenda kuongezea tu kwamba ili kuweza kupima ufahamu/uelewa katika fani husika basi inabidi viwango vinavyokubalika ama kitaifa au kimataifa viwepo na vitumike.

Mathalani waajiri watakachoangalia kwanza ni je shahada unayo? Baada ya hapo ndio utendaji wako utaonekana, sasa hata kama kazi ile unaimudu lakini huna shahada basi hata kuitwa kwenye mahojiano itakuwa ndoto, au naongopa?
 
Back
Top Bottom