World Military Geniuses Of All Time

Well tufanye basi Byzantine ilishinda vita zote, na haikupigwa, na Jerusalem haikuanguka
Kwenye world history hakuna jeshi limewahi kuwa na nguvu, organized na strategy kama la Roman empire. Ile ni empire mzee, sio nchi. Kama waarabu walishinda kwenye jimbo moja tu la empire haina maana waliishinda empire nzima. Inategemea na priority za empire kipindi hicho. Unaweza kuta walikuwa na camping zingine za maana wameconcetrate huko
 
Duh, yaani kwenye list yako umemuweka John Okello? Kwenye list yako hayupo Khalid ibn Walid, 'Amr ibn al-'As, S'ad ibn Abi Waqqas, Tariq ibn Ziyad, Genghis Khan, Muhammad al-Fatih, Aurangzeb, George Washington, Erwin Rommel, George Patton na Douglas McArthur!!
Balj....
Ahsante sana.

Field Marshall Josip Tito.
 
Kwenye world history hakuna jeshi limewahi kuwa na nguvu, organized na strategy kama la Roman empire. Ile ni empire mzee, sio nchi. Kama waarabu walishinda kwenye jimbo moja tu la empire haina maana waliishinda empire nzima. Inategemea na priority za empire kipindi hicho. Unaweza kuta walikuwa na camping zingine za maana wameconcetrate huko
Roman empire haikunyang'anywa Jimbo moja tu na Waarabu, Bali Ilinyang'anywa majimbo mengi including, Syria, Mesopotamia(Irak), Palestine, Egypt
Baada ya hapo haikubaki Roman Empire ile yenyewe tunayoisoma!
 
Byzantine haikuwa Syria tu. Hivyo kama alishinda vikosi vya Syria haina maana kuwa aliwashinda warumi. Hakuna mtu mwenye ubavu wa kuwashinda warumi
Mkuu, dola la Rumi katika miaka yake zaidi ya 2000 halijawahi kufanikiwa kuwapiga waajemi hata siku moja. Baada ya dola la Karthago (Carthage) nadhani madola ya Uajemi (The Parthian Empire and The Sassanian Empire) ndiyo yalikuwa maadui wakubwa wa Roma ambao Roma alishindwa kuwashinda. Hizi nyingine za kusema Roma hawezi kushindwa nadhani ni propaganda za kidini ambazo inabidi zitazamwe upya. Haya hebu zingatia vita zifuatazo:

The Battle of Carrhae: Hii vita ilipiganwa mwaka 53 BC, kule eneo la Carrhae ambako ni Uturuki ya leo, ambapo mwanajeshi wa Roma mwenye uwezo wa kipekee kabisa na aliyewahi kushinda vita (Imperator) Marcus Lucianus Crassus. Huyu alivamia dola la kiajemi la Parthia na wanajeshi 4,3000. Hawa wanajeshi walikuwa ni wazoefu wa vita (Battle Hardened) maana kabla ya hii vita walikuwa wametoka kupigana na jeshi la watumwa lilikuwa chini ya Spartacus na Crixus (The Third Servile Wars) na kushinda. Walikuwa na jeshi la wavaa vyuma vizito (Legionaries/Heavy Infantry) wasiopungua 35,000, huku adui wao kiongozi wa jeshi la Parthia, Rustem Surena alikuwa na wanajeshi 10,000.

Hao wanajeshi 10,000 waligawanywa katika makundi mawili ambayo ni wapanda farasi wenye mishale 9,000 (Mounted Archers) na Jeshi la wapanda farasi wenye vyuma 1,000 (Heavy Cavalry/Cataphracts). Jeshi la Roma lilizidiwa na maelfu ya Warumi waliuwawa huku watu zaidi ya 10,000 wakichukuliwa mateka. Silaha kubwa ya waajemi ilikuwa ni mishale (The Scythian Composite Bow) ambao uliletwa na mfalme Koreshi miaka mingi nyuma. Wanahistoria wanasema waajemi waliwazunguka Waroma huku wakiwa wananyesha mvua ya mishale kwa masaa mengi bila kusimama. Fuatilia utaona......

The Battle of Nisibis: Hii vita ilipiganwa mwaka 217 AD, kule Nisibis ambako nako ni Uturuki ya leo. Hii vita ilianza kwa ugomvi mkubwa ambapo Kaisari wa Roma Caracalla alivunja mkata alioingia na mfalme wa Uajemi (Parthian Empire), Artabanus IV kwa kuvamia Uajemi na kuua raia wasio na hatia. Waajemi walipanamba na Waroma kwa siku tatu mfululizo, ambako maelfu yao walikufa. Kaisari wa Roma baada ya kuona atauwawa ikabidi akubali kushindwa na kumlipa mfalme wa Uajemi fidia kubwa mno ya pesa pamoja na kurudisha mateka wa kijeshi.

Halafu ukumbuke kipindi hiki dola la Kiparsi ndiyo lilikuwa linaelekea kuanguka , maana walikuwa wanapigana vita vya wao kwa wao (Civil War) kugombania madaraka. Wafalme wa Roma waliona hii ndiyo nafasi kuvamia Uajemi, lakini waliangukia pua vibaya mno.

The Battle of Edessa: Hii vita ilipiganwa mwaka 260 A.D kule Edessa, ambako ni Uturuki ya leo. Nadhani hii ni moja ya vita mbaya zaidi kuwahi kuikuta Roma ukizitoa vita kama zile za Vita ya Cannae (The Battle of Cannae) na vita ya ziwa Trasime (The Battle of Lake Trasimene) ambazo majeshi ya Roma yalichinjwa vibaya sana na vikosi vya mwanajeshi wa Karthago, Hannibal Barca. Hii vita ya Edessa ilikuwa ni mbaya sana hadi kupelekea Kaisari wa Roma Publius Lucianus Valerianus pamoja na wanajeshi 70,000 walitandikwa vibaya na kuchukuliwa mateka na mfalme Shapur I wa dola la Kiajemi la Sassani (The Sassanian Empire). Kaisari wa Roma alifia Uajemi na nchi ikaingia kwenye taharuki kubwa mno. Hichi ni kitu ambacho wengi hatufundishwi kwenye vitabu vilivyojaa propaganda za kidini na kizungu. Fuatilia utaona.......

Wababe wengi wa Roma kama Mfalme Trajan ,walipambana na Uajemi hadi kufika mji mkuu Ctesiphon na kuupiga lakini hawakufanikiwa kuwashinda waajemi. Sasa hebu fikiria, mtu kama Trajan alishindwa kuwatawala waajemi unadhani walikuwa ni watu wa aina gani hawa. Mfalme Heraclius naye alijaribu na kushindwa vibaya mno hadi kufanya makubaliano ya amani.

NB: Dola la Mrumi kuanzia mji wa Rome hadi Constantinople walikuwa wanapigika sana. Wafalme kama Attila The Hun, Theodoric The Great, Khosrow na majeshi yao walifanikiwa kufika sehemu za ndani kabisa za Roma huku Sultani Mehmed II (The Conqueror) akifanikiwa kuwaangusha kabisa Waroma na kuutwaa mji mkuu wa Constantinople huku akijipa jina la Kaisari.

NO BODY IS INVINCIBLE............
 
Wa kwangu ni:
(1) Alexander the Great
(2) Field Marshal Zhukov
(3) Admiral Nimtz
(4) General Eisenhower
(5) Field Marshal Ben Montgomery
(6) Shaka Zulu the Great
(7) Mzilikazi, also spelled Mosilikatze or Moselekatze,
(8) Chief Songea
Msimsahau yule mama wa Singida aliyewakimbiza wajerumani kwa kutumia nyuki
 
Wa kwangu ni:
(1) Alexander the Great
(2) Field Marshal Zhukov
(3) Admiral Nimtz
(4) General Eisenhower
(5) Field Marshal Ben Montgomery
(6) Shaka Zulu the Great
(7) Mzilikazi, also spelled Mosilikatze or Moselekatze,
(8) Chief Songea
Sio Songea sema full AbdulRauf Songea Mbano chief of Rovuma
 
Roman empire haikunyang'anywa Jimbo moja tu na Waarabu, Bali Ilinyang'anywa majimbo mengi including, Syria, Mesopotamia(Irak), Palestine, Egypt
Baada ya hapo haikubaki Roman Empire ile yenyewe tunayoisoma!
Ni sahih Ruum au roma ilikua great roman empire.lakin walikuja kupoteza na kufutika.
 
Duh, yaani kwenye list yako umemuweka John Okello? Kwenye list yako hayupo Khalid ibn Walid, 'Amr ibn al-'As, S'ad ibn Abi Waqqas, Tariq ibn Ziyad, Genghis Khan, Muhammad al-Fatih, Aurangzeb, George Washington, Erwin Rommel, George Patton na Douglas McArthur!!
Khalid ibn walid.sayfuu llah.huyu jamaa alikuwa anaenda na jeshi wakat fulan amekwenda kuvamia rome.kapaki jesh mpakana akaandika barua kwenda kwa kaesar.akimwambia. nje yako kuna jeshi ambalo kufa kwao ni kuzuri zaid kama ambavyo kuishi ni kuzuri kwenu.silimu au lipa kodi,.. hakuna aliyekuwa anaweza vita na huyu mwamba
 
1. Saladin
2. Shaka
3. Napoleon Bonaparte
4. Attila the Hun
5. Genseric the Vandal
6. Alexander the Great
7. Charlemagne
8. John Okello
9. Chris Hani
10. Hannibal
11....
Hii list bila Sun Tzu, Genghis Khan, Sima Yi na Zhughe Liang basi ni batili. Hao ndo walotengeneza foundation ya tactics za kupambana dhidi ya adui iwe nje au ndani ya vita. Nikimaanisha hata mahakamani au kwenye business competition tactics za hao jamaa bado zinafanya kazi
 
George S.Patton
General Deouglas MacArthur
Erwin Rommel
Julius Caesar
King David
Zhukov
Pavlov
General Mayunga
Dwight Eisenhower(Iyke)
 
1. Saladin
2. Shaka
3. Napoleon Bonaparte
4. Attila the Hun
5. Genseric the Vandal
6. Alexander the Great
7. Charlemagne
8. John Okello
9. Chris Hani
10. Hannibal
11....
Zelensky the Visionary!
 
Bado wapersia walikuwa ni watu wagumu kukutana nao vitani, Mimi naona kabisa Kuna jamii huwa zinapewa vitu fulani ambavyo wengine hawana in nature kabisa...ila Genghis Khan,Timur(Timerlane),Mehmed the conqueror, Napoleone Bonaparte, Salahudin Al ayub, Alexander the great, Khalid bin Walid, Subutay, Wellington, stori zao zinasisimua sana, watu wenye ujasiri Sana....
 
Hapo namba 8 na 9 ni changa la macho. Yaani hao wawazidi Field marshals Erwin Rommel na Eric von Manstein? Wako akina Admiral Chester Nimitz, Dwight D Eisenhower, Suleyman the Magnificent, Mehmet the Conqueror of Constantinople na wengine wengi tu.
 
Byzantine haikuwa Syria tu. Hivyo kama alishinda vikosi vya Syria haina maana kuwa aliwashinda warumi. Hakuna mtu mwenye ubavu wa kuwashinda warumi
Nikupe tu hii ya karibu ottoman empire ilitawala hiyo ulaya yote Asia na Africa
 
Kwenye hii orodha Muhammad bin Maslamah anatakiwa awemo. Huyu alikuwa Chief of Covert operations in the army of the Prophet of Islam Muhammad (PBUH).
 
Erwin Rommel

huyu Wamarekani wanamjua, hali kadhalika Waingereza wanamjua

Huyu bwana Akiwa na Silaha duni za kiitaliano katika vita kuu ya pili ya dunia alikuwa anawaburuza Kundi la wamarekani,Waingereza,Wafaransa kwamuda mrefu na akiwa anatumia silaha duni na zana chache

Shujaa Erwin Rommel hata waliowachukia Wajerumani licha ya kuwa Rommel ni mjerumani ila walimpenda Rommel
Anaitwa Field Marshall Erwin Rommel wenyewe wakimwita Desert Fox. Alitikisa sana na Afrika Korps yake kule Afrika ya Kaskazini wakati wa vita ya pili ya dunia. Rommel was a military genius!
 
Back
Top Bottom