Ona ulivyo mjinga , Muhammad alikuwa haongei jambo Kwa utashi wake mnatuambia alikuwa anatoa Kwa Allah , apa wewe unakuja kusema hajatoa Kwa Allah ila ni maneno yake Muhammad
Soma hapa na husirudie tena kasome ujinga ukutoke
33:36. Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allah na Muhammad wanapo kata shauri katika jambo lao.
Maneno ya Allah subhanah ndio QURAN.
Maneno ya Mtume -swalla llahu allaihi wasallam- ndio HADITH ZA MTUME, ingawa hii inajumuisha na vitendo, sifa za Mtume, na mambo ambayo aliyakiri.
Mfano wa hadith ni hiyo uliyoitaja hapo juu.
Katika hadith kuna ambazo maana yake inatoka kwa Allah na lafydhi ni ya Mtume -swalla llahu allaihi wasallam- hizi zinaitwa HADITH AL-QUDSIY.
TOFAUTI
QURAN: ni maneno ya Allah kilafudhi na kimaana.
HADITH ZA MTUME: ni maneno ya mtume kilafudhi na kimaana.
HADITH AL- QUDSIY: ni maneno ya Allah kimaana na lafudhi ni ya Mtume -swalla llahu allaihi wasallam-.
Tunaposema Mtume swalla llahu allaihi wasallam- hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake bali ni Wahyi(ufunuo) kutoka kwa Allah.
Maana yake ni kuwa Mtume hazungumzii mambo ya dini kwa utashi wake bali ni ufunuo kutoka kwa Allah.
Mfano ni hiyo hadith uliyoitaja hapo juu, Mtume -swalla llahu allaihi wasallam- hakuwepo kipindi cha Nabii Ibrahim -alaihi ssalaam- bali ni kwa ufunuo kutoka kwa Allah ndio amejua hivyo.
Lakini itabaki kuwa hayo ni maneno ya Mtume -swalla llahu allaihi wasallam- kilafudhi na kimaana.
Na Allah ndiye mjuzi zaidi.