Dr Lizzy
Platinum Member
- May 25, 2009
- 30,811
- 59,364
Haya uliyoandika sio yanayofanywa na wanawake. Wanawake wanachoomba ni kupendelewa because they can not compete with men. Mfano Kwa sababu wanawake wengi walikuwa hawawezi kuendelea na elimu ya sekondari, wanafaulishwa kwa viwango tofauti. Pia kwenye viti vya ubunge, kwa sababu mwanamke hawezi kushindana na mwanaume ndio maan mmepewa viti maalumu.
Mi naona mbadilishe tu msemo kwamba tunaomba wanaume wawe wanatupendelea na sio kuomba haki sawa. Halafu mbona hizo haki sawa mnazitafuta kwa kufanya mambo wanayofanya wanaume. Mnatamani kuwa wanaume?????!!!!!
Hayo siyo yanayofanywa na wanawake wapi?!Unaowafahamu wewe?!Kama jibu ni ndio je wao ni wawakilishi wa wanawake dunia nzima?!Kama jibu ni hapana je unajuaje kama siyo?!
Kama kweli ungekua na vithibisho vya unayoongea swala la ubunge wa viti maalumu lingekua dogo sana maana sidhani kama ndivyo inavyofanyika dunia nzima. Pia swala la kufaulishwa kwa viwango tofauti sikuwahi kufahamu....na hata kama ndivyo bado I can guarantee you kwamba kufaulu kwangu wakati nasoma hakukua kwa upendeleo.Unless 50% ya msichana inatambulika tofauti na 50% ya mvulana. Kama kwenye mitihani ya shule tu (achana na ya taifa maana labda ndipo upendeleo ulipo) wasichana wengi tu wanawapiga kikumbo wavulana iweje muamini kwamba wanahitaji upendeleo kupata marks za juu?!
Huo sasa ndio mfumo dume unaopingwa...kinachotakiwa ni kwa wanawake kupewa nafasi ya kufanya mambo kwa uwezo wao wenyewe badala ya kupewa ushindi wa mezani kwasababu hatuuhitaji.Kwenye siasa bado sisi ni wachanga sana kama nchi..hivyo kitendo cha kuwakabidhi wanawake ubunge (japo sikubaliani nacho) ni njia ya uhamasishaji pia nyingine kati ya mifumo dume. Hakika sio wanawake wengi wanaojishughulisha na siasa hapa kwetu kwasababu mwanzoni waliaminishwa kwamba HAWAWEZI hivyo kinachofanyika sasa hivi ni wanaume kuwahamasisha wanawake waanze kujihusisha nayo...ila sasa kwasababu bado mfume dume umetawala wanawagawia ili waamini kwamba wenyewe bila msaada wa mwanaume HAWAWEZI.
Na kama utaniambia kwamba hata mawaziri wa kike (nje ya Tanzania) nao walibebwa basi ntakuona bado unaishi enzi za agano la kale na unahitaji kuwa UPDATED haswa!