Wolper na Isalito penzi moto, wavujisha chats zao

Wolper na Isalito penzi moto, wavujisha chats zao

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,112
Muigizaji Wolper aweka wazi namna alivyokuwa akifanya mawasiliano ya kimapenzi na muigizaji Isalito.

Mawasiliano ya picha za jumbe fupi (chat) yaliyovuja mtandaoni yamezua gumzo kubwa miongoni mwa mashabiki, baada ya kuonyesha muigizaji mashuhuri wa filamu nchini Tanzania, Jacqueline Wolper, akibadilishana jumbe za mahaba na mwigizaji mwenzake, Isalito.

Katika gumzo hilo lililoanza kusambaa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii, wawili hao wanaonekana wakitumia majina na maneno ya mahaba kama “My Man” na “Good morning my beautiful woman.”

Pia, jumbe hizo zilionyesha Wolper akimpa taarifa Isalito kuhusu ratiba na shughuli zake za asubuhi, jambo linaloashiria kuwepo kwa uhusiano wa karibu wa kimapenzi baina yao.

Uvujaji wa mawasiliano hayo umeibua mijadala na maswali mengi miongoni mwa ulimwengu wa burudani, huku mashabiki wakijiuliza iwapo wawili hao wameamua kuweka wazi mahusiano yao rasmi au ni siri zao za ndani zilizofichuka bila ridhaa yao.

Mpaka sasa, hakuna yeyote kati ya wasanii hao aliyetoka hadharani kuthibitisha au kukanusha ukweli wa jumbe hizo.
1789907157490.png
 
Ujinga ujinga tu

USSR

Badala ya kujenga mapenzi yao wenyewe wa wawili, ambayo kusema kweli yako very fragile, wanataka kuwaoyesha walimwengu wanapendana.

Hawa watu hawa.....
 
Back
Top Bottom