Rashiditanz
Senior Member
- Apr 4, 2014
- 167
- 61
Kasi ya namna hii Tanzania haijawahi kuiona, kwa hivyo watu hawa amini wanachokiona, kilichobaki kwa sasa hivi ni watu waliokuwa wana uchuki na mfumo wa zamani kuendelea kuikosoa kila kukicha, na ni haki yao... ila kubadili tabia nchi unaanza na walio kabidhiwa nchi mpaka ngazi ya chini kabisa ambaye ni raia wa kawaida mitaani... hii kitu siyo kazi ya wiki au miezi michache tu! Kadri muda unavyo songa mbele, na mambo mengi yatanyooka tu..
Nina imani na ninacho kisema.. kwani siioni chama kinachotawala kwa sasa hivi, bali anaye kiendesha.. na nina imani pia kwamba anafanya kila anachoweza kwa moyo mmoja.. msione hana changamoto zilizojificha ambazo sisi waraia hatuwezi kuziona kirahisi hivyo..
Anajitahidi sana kuimulika kila sekta iwezekanavyo, na bado mengi tu yatamulikwa, kwa uwezo wa mwenyezi mungu. Kama mheshimiwa ana mapungufu yake kwa sasa hivi na zile ambazo anamulikiwa yeye za zamani, kuna binadamu aliyenyooka mia kwa mia? Mbona mheshimiwa wa Monduli tulitaka kumkubali? Sababu zilikuwa kumkubali kwa sifa zake tu, au kwa sifa tulizo aminishwa ambaye ingebadili mwelekeo wa chii hii?
Kama mheshimiwa wetu sasa hivi hatoweza kubadilisha mfumo wa chama tawala kwenye miaka mitano ijayo, itakuwa vigumu sana kumpata mwingine atakayeweza.. Na misingi ukisha sawazishwa, iije chama chochote tu kile, tabia nchi ndio utatawala! Kwani tabia naye ni mjeuri sana..
Sahihisho -> mwenyezi Mungu