WMN ni Namba au herufi?

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Nimesikiliza redioni na kusoma katika magazeti utambulisho wa magari (identification ante) ya viongozi wetu ambazo zinatumia
herufi, waandishi wakiandika kwamba kuwa hiyo ni namba ambapo hakuna tarakimu yo yote.

Hebu soma: ".............. ameiambia mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo wakati Waziri Nahodha akiwa ndani ya gari yenye namba WMN alipokuwa katika ziara Mkoani Mbeya ....." Je, gari ikiwa na JM (Jaji Mkuu), JK (Jaji Kiongozi) au S (Spika).

Kwa mawazo yangu namba inatafsirika kama tarakimu.
 
Uko sahihi lakini vipi kuhusu T463AAA ni namba ya gari au herufi na namba ya gari?
 
Hiyo si namba wala tarakimu itasomeka kama usajili ....( Ukitaja tarakimu na namba kama zilivyo kwenye kibati cha usajili)
 
Mnasahau matumizi ya lugha kulingana na muktadha. Kimsingi magari husajiliwa kwa kupewa namba za utambulisho kwa madhumuni mbalimbali likiwemo suala la malipo ya kodi.

Kwa hiyo pale gari linapoonekana limenominiwa WMN, JK, S, WM n.k ieleweke kimuktadha kwamba hizo ndiyo 'namba' zake.

Jambo hili lafanana kabisa na mnapokutana sehemu ya maakuli kama hotelini au mgahawani ambapo mhudumu hutokea akiwa amebeba oda nyingi na kuanza kuzisambaza kwa kuuliza: 'nani kuku?'.

Na kwa hiyari yako mara zote umekuwa ukiitikia: 'mimi hapa'. Katika muktadha huu hatuwezi kuanza kukuita kuku licha ya ukweli kwamba ni wewe mwenyewe ulitutangazia kuwa wewe ni kuku!
 
Mnasahau matumizi ya lugha kulingana na muktadha. Kimsingi magari husajiliwa kwa kupewa namba za utambulisho kwa madhumuni mbalimbali likiwemo suala la malipo ya kodi. Kwa hiyo pale gari linapoonekana limenominiwa WMN, JK, S, WM n.k ieleweke kimuktadha kwamba hizo ndiyo 'namba' zake. jambo hili lafanana kabisa na mnapokutana sehemu ya maakuli kama hotelini au mgahawani ambapo mhudumu hutokea akiwa amebeba oda nyingi na kuanza kuzisambaza kwa kuuliza: 'nani kuku?'. Na kwa hiyari yako mara zote umekuwa ukiitikia: 'mimi hapa'. Katika muktadha huu hatuwezi kuanza kukuita kuku licha ya ukweli kwamba ni wewe mwenyewe ulitutangazia kuwa wewe ni kuku!
.
Ha! ha! ha! ... Mkuu Omonto wa-hene mimi mtu akiniuliza hivyo siitikii! ... bora nikose ... kwani mimi Kuku?!
 
Back
Top Bottom