Wizi wa TV Dar es Salaam

Wizi wa TV Dar es Salaam

fisi 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
3,284
Reaction score
4,651
Wimbi la wizi wa TV FLAT SCREEN TU LMV umeshamiri sana. Kuanzia Tabata, Kinyerezi, mitaa yote ya Mbezi Louis hadi Salasala na Bunju. Wajuaji hawa wanakata grill za dirisha kuingia na kuiba. Pamoja na mikakati ya kiulinzi ambayo tunafanya naomba POLISI kwa umoja wao wachunguze hili SOKO kubwa hivi la TVs ni wapi sababu mfano jana tu nyumba 6 zimeibiwa. Wengine ambao haijawafika tujilinde na mali zetu jamani.
 
Duh aisee vp mkuu wamekuibia nini maana uzi asubuhi asubuhii

Mi nikikuwaga na chogo bwana lile la kilogram 50 mwizi akaingia chumbani ile kulibeba tu likamzidi nguvu akaanguka nalo mpaka miguu yake ikavunjika
 
Ikipotea wewe kariri tu IMEI ya TV yako akiwasha tu popote pale unajua ilipo.
 
Atakaye ibiwa Tv na anataka kumshughulikia mwizi wake aje PM,tumfanye kitu mbaya,haiwezekani watu waishi kwa hofu na mali zao,utakuta mijitu imejazana Dar ikiwa haina kazi za kufanya wakati wameacha mapori kijijini kwao.
Dawa yao ipo,wasengerema hao!!
 
Wimbi la wizi wa TV FLAT SCREEN TU LMV umeshamiri sana. Kuanzia Tabata, Kinyerezi, mitaa yote ya Mbezi Louis hadi Salasala na Bunju. Wajuaji hawa wanakata grill za dirisha kuingia na kuiba. Pamoja na mikakati ya kiulinzi ambayo tunafanya naomba POLISI kwa umoja wao wachunguze hili SOKO kubwa hivi la TVs ni wapi sababu mfano jana tu nyumba 6 zimeibiwa. Wengine ambao haijawafika tujilinde na mali zetu jamani.

Soko kubwa la Flat TV ni Vibanda Umiza (Vibanda vya kuonyesha Movie na Mpira Uswazi)
 
Zinauzwa kwa mabaa cha msingi ni kutunza imei ya TV ikiwashwa tu unapata signal,
 
Mimi wamewahi kunipiga TV inchi 42 then nikanunua nyingine. Baada ya kama miezi 9 wakarudi tena. Siku hiyo bahati nzuri nilikuwa macho so nikawasikia kabisa wanavyoangaika na dirisha. Nikawaweka kwenye target nimdedishe moja. Wife akawaonea huruma, so nikaenda pale dirishani nikawaambia "madogo sijalala, mtakuja kufa".
 
Hawa vibaka wamekuwa mtihani mkubwa, watu hawana amani majumbani mwao, huko Goba nasikia ndo kumekithiri. Tuendelee kushauriana nini cha kufanya, labda tutoe mapendekezo irudi sheria ya uzururaji
 
Mimi wamewahi kunipiga TV inchi 42 then nikanunua nyingine. Baada ya kama miezi 9 wakarudi tena. Siku hiyo bahati nzuri nilikuwa macho so nikawasikia kabisa wanavyoangaika na dirisha. Nikawaweka kwenye target nimdedishe moja. Wife akawaonea huruma, so nikaenda pale dirishani nikawaambia "madogo sijalala, mtakuja kufa".
Ungevunja ht mguu asee mkuu wangepeana habari
 
Mimi wamewahi kunipiga TV inchi 42 then nikanunua nyingine. Baada ya kama miezi 9 wakarudi tena. Siku hiyo bahati nzuri nilikuwa macho so nikawasikia kabisa wanavyoangaika na dirisha. Nikawaweka kwenye target nimdedishe moja. Wife akawaonea huruma, so nikaenda pale dirishani nikawaambia "madogo sijalala, mtakuja kufa".
Huyo mke wako bhana... dah!
 
Huyo mke wako bhana... dah!
Hahaha. Eti aliniambia alianza kuwaza jinsi mama wa huyo kijana anakavyoumia akipata taarifa kijana wake ameuliwa. Akaangalia thamani ya TV na uhai wa huyo kijana! Anaona maadam hawajaingia ndani na hakuna madhara ya kimwili waliofanya basi akaona busara ni kuwakurupusha wakimbie.
 
Alikua yupo sahihi,japo ungevunja hata mguu tu akaadithie
 
Mimi wamewahi kunipiga TV inchi 42 then nikanunua nyingine. Baada ya kama miezi 9 wakarudi tena. Siku hiyo bahati nzuri nilikuwa macho so nikawasikia kabisa wanavyoangaika na dirisha. Nikawaweka kwenye target nimdedishe moja. Wife akawaonea huruma, so nikaenda pale dirishani nikawaambia "madogo sijalala, mtakuja kufa".
Mchunguze mkeo anashilikiana nao
 
Back
Top Bottom