Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,068
- 43,511
Una app ya Tigo Pesa? Umesajili mastercard tigo? Ama malipo mengine yanayo tumia Tigopesa?Imeshangasha Pesa imeweza kuhamishwa kutola kwenye namba yangu ya YAS bila mimi kujua au kuona meseji.
Imenishangaza kwasababu nimeigundua baada ya kuangalia statement kwenye Yas app na kuona nimetuma hela mara tatu kiasi cha laki 3 kwa watu nisiyowafahamu.
Hakuna msaada kutoka Yas wanasema nichukue hatua za kisheria.
Huenda technolojia imekuwa zaidi au pesa zetu haziko salama kwenye mitandao.
Kama watu wanaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye simu hii ni hatari sana
Simu yangu ninakaa nayo mwenyewe na hakuna aliyeishika kwakuwa ina password ya fingerprint.
Cha muhimu hapo Nenda Tigo makao makuu ama ofisi kubwa ya Tigo yenye watu wanaojielewa, ujue exactly kifaa gani ama huduma gani imetoa hio Hela.
Unaweza kukuta mtu anatumia app ya Tigopesa na no yako, kaverify kidole gumba chake anagusa tu akitaka kutoa hela zako.