Wizi wa pes Mix by YAS

Wizi wa pes Mix by YAS

Ukiwa unatumia VPN Airtel money app inaji-logout, Kutumia apps ambazo hazieleweki au tunazidownload kupitia Google Moja Kwa Moja ni risk sana, Bora kudown load kutoka play store au apple store. Pia kuingia kwenye link ambazo hujui source yake ni hatari sana.
 
Imeshangasha Pesa imeweza kuhamishwa kutola kwenye namba yangu ya YAS bila mimi kujua au kuona meseji.
Imenishangaza kwasababu nimeigundua baada ya kuangalia statement kwenye Yas app na kuona nimetuma hela mara tatu kiasi cha laki 3 kwa watu nisiyowafahamu.
Hakuna msaada kutoka Yas wanasema nichukue hatua za kisheria.
Huenda technolojia imekuwa zaidi au pesa zetu haziko salama kwenye mitandao.
Kama watu wanaweza kuhamisha pesa kutoka kwenye simu hii ni hatari sana
Simu yangu ninakaa nayo mwenyewe na hakuna aliyeishika kwakuwa ina password ya fingerprint.
Hii imenitokea jana aisee nmepigwa laki 9 jana usiku nipo hapa hata sijui what to do. ukiwapogia watu wa mixx hata hawatoi ushirikiano.
 
Hii imenitokea jana aisee nmepigwa laki 9 jana usiku nipo hapa hata sijui what to do. ukiwapogia watu wa mixx hata hawatoi ushirikiano.
Duuh hakuna mtu alieshika simu yako hivi karibuni? hasa Hawa wanaosajili line njiani
 
Pole sana mkuu
Huo ni mtandao wa hovyo kabisa hapa nnchini. Hata wale wa. TUMA KWA NAMBAA HII ni wana connection na Yas naweza kuthibitisha
Juzi nilinunua umeme nikaambiwa nadaiwa NIVUSHE jambo ambalo siyo kweli.
Jana nilinunua VOCHA ikakatwa ati nadaiwa jambo ambalo siyo kweli na ukipiga customer care mlolongo ni mrefu sana. Naitumia namba yao KUPOKELEA SIMU TU wakwende zao huko mix mix wezi wakubwa hawa TIGO
Kweli mkuu hawa Tigo wanashirikiana na wezi wa mitandaoni, Nilikopaga kwenye kampuni hizi za Mitandaoni baada ya siku ya kulifa haijafika nikaanza kutishiwa na kutukanwa na wakatuma sms kwenda kwenye namba za watu wangu wa karibu,Sasa mimi sikuwalipa, Sasa kuna siku nikatumiwa pesa nyingi kidogo kwenye line yangu ya Tigo baada ya Dakika tano kampuni niliyokopa wakaanza kunipigia simu ya kuniambia niwalipe deni lao toka siku hiyo nikajua Tigo wanashirikiana na Wezi wa Mitandaoni kutoa Taarifa za Wateja wao, nahisi hawa Tigo wanatoa Taarifa za Wafabiashara wapya waliofungua Tigo pesa mpya kwa Wezi ili waende wakawaibie.
 
Unapotoa tuhuma jaribu kua na uhakika na unachosema...

Tatizo mnapokopa mnawaza pesa tu hata masharti hamzingatii, hizo app unazosema hua zinaomba access ya simu yako kama sms,contacts etc kabla hujapewa pesa... ukikubali tu ina maana wanakua wanaweza kuona call logs zako zote, sms zako zote na contact zako zote.... hivyo ikiingia sms ya tigo pesa kama ulivyosema kwasababu uliwapa access wewe mwenyewe
wanaona tu vizuri kabisa

Achana na hio, kuna app wanatoa mikopo wao wanaomba full phone access, kwasababu wengi wanakimbilia pesa tu unakuta kila anachoulizwa anakubali, hapo ndo utachoka sasa, wanakua na uwezo wa kuona kila unachofanya na simu yako yani wanakua kama wana copy ya simu yako wanaangalia unavyofanya, ukiingia m pesa,tgo pesa,airtel money etc wanaona unaweka pin, ukitumia mobile banking, selcom wanaona kila kitu mpaka pin unavyoweka, hapo ndo utaamka siku ukute wamekusafisha kila mahali urudi kulalamikia mitandao ya simu na serikali
 
Back
Top Bottom