Wizi wa mifuniko barabarani Dar

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,083
5,066
Wizi huu umekithiri katika mitaa ya Upanga na inahatarisha magari na usalama wa watu.
Jiji na manispaa husika pamoja na polisi hebu kemeeni wizi huu.
Mojawapo ya tetesi ni kuwa kuna wakubwa wanavizia tenda ya kurudishia mifuniko hiyo na ndio wafadhili wa wizi huu.
 
Hii ni aibu kwa Taifa na Kila Mtunza Usalama wa Hii Nchi!! Mifuniko ya Chemba za barabarani / Heavy duty covers Unachukuliwa na Kupelekwa Gerezani kwa Mauzo na Hakuna wa Kuuliza!! Fuso Linajaza mifuniko kibao na linakuwa pale Mikocheni Kwenye foleni kuingia katika Kiwanda Cha "MMI," Na hakuna wa kuuliza kisa Wanauza Vyuma Chakavu!! Jamani Kweli Hivi ni Vyuma Chakavu? Kwa nini tumefikia Hapa? Nashauri serekali Ianze kuzuia wanunuzi kabala ya kupambana na hawa wanaoiba!!
Je Tujiulize ni nani Mwenye Huu uwezo wa kuweza kuzuia Haya yasitokee? Kwa Jinsi Hali ilivyo Hakuna ambaye anaweza kujitokeza kuzuia yote haya yasitokee; kwani atafanya kwa Faida ya Nani? Duh!! Hili Taifa linahitaji Kuombewa!!
Mimi Nawashauri Halmashauri,DAWASCO, TTCL, TANROADS NA wadau wengine waathirika wa hii mifuniko iliyoibwa na ambayo inasababisha Athari nyingi za kiusalama kwa watembea kwa miguu, waungane na Kuwa na sauti Moja na Kusema sasa Hii iwe ni Mwisho!! Kwani serekali imeshindwa kazi Yake!!
 
Kumbe inazungumziwa mifuniko ya chemba za maji taka!!
Asante Mkweli21 kwa ufafanuzi wa kina.
 
Wizi huu umekithiri katika mitaa ya Upanga na inahatarisha magari na usalama wa watu.
Jiji na manispaa husika pamoja na polisi hebu kemeeni wizi huu.
Mojawapo ya tetesi ni kuwa kuna wakubwa wanavizia tenda ya kurudishia mifuniko hiyo na ndio wafadhili wa wizi huu.

Kwani ajira milioni moja zimeshakwisha?
 
Wizi huu umekithiri katika mitaa ya Upanga na inahatarisha magari na usalama wa watu.
Jiji na manispaa husika pamoja na polisi hebu kemeeni wizi huu.
Mojawapo ya tetesi ni kuwa kuna wakubwa wanavizia tenda ya kurudishia mifuniko hiyo na ndio wafadhili wa wizi huu.

nawaunga mkono wanaoiba...kwani mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake...
mi nadhani tungekuwa wazalendo kama tungeanza kukemea wizi unaofanyika maofisini
na viongozi wetu....then tuangalie huu wa vibaka wanaotafuta hela ya kula ili waishi,
sio hela ya kujilimbikizia kama wafanyavyo vigogo we2..... kikwte mwenyewe keshaturuhusu
kwa kusema ukitaka kula lazima ukubali kuliwa....sasa sisi tunaliwa sana na masisadi...ngoja
na sisi tule sasa....na pia ni namna ya kutengeneza fursa za ajira...kwani kuna watu wataajiriwa
kuja kutengeneza mifuniko hiyo tena...halafu tunaichukua then wanakuja tena...life goes on.
 
Two mistakes will never make one right.Naamini kuna njia nyingi za kukabiliana na viongozi wezi ila shida yetu watanzania waoga na ndo maana hata jina langu sijaandika.
 
Kali zaidi ni kwamba, wameiba mfuniko hadi pale nje ya wizara ya mambo ya ndani (pale kwenye parking ya taxi), sehemu ambayo wengi tunadhani ni 'wizi proof'. Shame on them
 
nawaunga mkono wanaoiba...kwani mbuzi hula kutokana na urefu wa kamba yake...
mi nadhani tungekuwa wazalendo kama tungeanza kukemea wizi unaofanyika maofisini
na viongozi wetu....then tuangalie huu wa vibaka wanaotafuta hela ya kula ili waishi,
sio hela ya kujilimbikizia kama wafanyavyo vigogo we2..... kikwte mwenyewe keshaturuhusu
kwa kusema ukitaka kula lazima ukubali kuliwa....sasa sisi tunaliwa sana na masisadi...ngoja
na sisi tule sasa....na pia ni namna ya kutengeneza fursa za ajira...kwani kuna watu wataajiriwa
kuja kutengeneza mifuniko hiyo tena...halafu tunaichukua then wanakuja tena...life goes on.

kwanini tushangae hilo la wizi wa mifuniko ya maji kuliko kushangaa polisi waliiba mishahara yao wenyewe hii ndio "FISADISTAN"
 
Back
Top Bottom