Wizi wa mafuta Petrol Stations

Wizi wa mafuta Petrol Stations

Toxic Concotion

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
5,782
Reaction score
21,008
I salute you all in God's name.

Mimi si mgeni Jf bali ni mgeni kwa kuandika post as in this is my first post. I have always been a guest.

Kilichopelekea kuandika kwangu uzi huu ni wizi uliokithiri kwenye vituo vya mafuta kutoka kwa wahudumu wake. Hili jambo nimeliona kwa macho yangu kwenye Petrol Station zaidi ya tano.

Kumekuwa na mchezo wa Attendants wa Petrol Station kutozima pump baada ya kutia mafuta kwenye gari ama piki piki ambapo baada ya hapo gari itakayofuata pump haitoanzia zero bali kiasi kile kilichowekwa kwenye chombo cha kabla.

Kama gari ya mwanzo iliweka 5000 na pump haijazimwa na gari inayofuata ikataka 20000 inamaanisha ni 15000 tu ndo itakayowekwa.

Na hili jambo nahisi linajulikana hata na wamiliki maana kuna Petrol Station moja niligombana na muhudumu baada ya kuanzia 3000 na nikahitaji kuongea na meneja lakini cha ajabu meneja hakutoa ushirikiano uliotakikana.

To cut the story short, kuna haja ya wamiliki wa vituo vya mafuta kuliangalia hili swala kwa makini maana leo kuna mtu kama mimi nalijua hivyo nakua makini nikiwekewa mafuta ila kuna wale wasiofahamu ambao kila siku wanalizwa.

Mafuta bei ghali na wengi wa watu wanatembelea magari kwa kuhesabu mileage kulingana na mafuta yaliyowekwa sasa haiwi haki kwa watumiaji.
 
Hili ni kweli, usipokuwa makini unaibiwa, angalia pampu ainze 0000 kabla hajaweka mkono kwenye tundu la tenki
 
M kuu wizi huu umekithili,mwanzo nilikuwa na kawaida ya kukwepa pump attedant wanaume nakimbilia females lakini siku hizi na wanawake wamekwisha itimu hakuna cha gender tena,wizi ni mbele kwa mbele! Nimefika hatua ya kufikilia niwe najaza petrol kwenye jerrycan nijazie nyumbani kila asubuhi!
 
Kinachotokea ni kwenye matanki yanakuwa na mafuta kidogo,sasa wanapojaza mafuta kwenye gari upepo unakuwa 50% na 50% mafuta. Mimi sikuhizi natumia kidumu nikienda sheli kuweka wese,ukiona wanakataa ujue wanataka wakupige. pili uzembe w Ewura kutokuwa makini na rushwa wakati wa ukaguzi. Wizi huo unaanzia kwea meneja wakishirikiana na watumishi wao. Kuweni makini,usione aibu kutembea na Vidumu. shell hizo ni Puma ya Kimara,Olx ya Magomeni na nyinginezo nyingi.
Mi naweka kwene kidumu thn napaki pembeni nakamiliosha fueling yangu,maisha laini.
 
wewe umenunua gari juzi juzi na umeshajua kua kuna wizi wa nzmna hii.
 
Jamalm335

na nyie mnatuchosha kila siku mtaibiwa style hio hio??? acheni ubwanyene muwe mnashuka kuhakikisha unawekewa mafuta sahihi kulingana na hela uliolipa!!
 
Last edited by a moderator:
Style hii kwangu imekoma kwa kuwa tank inatumia funguo kwa hiuo lazima nishuke nifungue tank mwenyewe.
 
na nyie mnatuchosha kila siku mtaibiwa style hio hio??? acheni ubwanyene muwe mnashuka kuhakikisha unawekewa mafuta sahihi kulingana na hela uliolipa!!

Sidhani kuna sehemu yeyote umeshurtishwa kusoma sasa kuchoshwa huko umechoshwaje? Au ndo nyie wa kucomment ili mradi mcomment. Just coz u have an ability to write it doesnt mean u should write even when not required to.
 
mimi huwa natoa macho kama mjusi nahakikisha pump inasoma 0000 kabla haijaanza kupush.
 
OilCom ya chini barabara ya Kawe (Karibia na Raibow) wamekithiri hii michezo
 
ndo maana kuna siku naweka mafuta yanatofautiana kwenye gage wakati amount ni ileile,,,kweli shidaaa
 
Unakuta kituo kina myumba ya ibada pembeni utadhani wacha Mungu kumbe ndio wezi wakubwa
 
Kituo kimojawapo ni Engen ya mbezi makonde Kuna jamaa alinipiga buku 10 akaweka ya 20 wkt nimempa 30....ilipanda mishale miwili badala ya mi3.
 
Hawaangalii hata tanki ya gari ina ujazo gani wezi watupu. unashangaa tenki la vitz linaingia lita 50 limekuwa basi hilo? cha muhimu ukifika petrol station shuka angalia pump isome zero na itoe mafuta sio hewa.
 
Back
Top Bottom