Tahadhari kwa wateja wote wenye magari mnaoweka mafuta kituo cha Puma Sinza Kijiweni. Kituo hiki kina wahudumu Wanawake ambao ni wezi wenye ujasiri wa kutisha wa kuwaibia wateja mafuta mchana kweupe.
JINSI WANAVYOFANYA
Wanapouza mafuta kwa mteja, hasa wanaonunua mafuta kidogo chini ya sh elfu ishirini, wanategesha mpira kwa namna ambayo mashine haifuti mauzo hayo, inabaki inasoma kuwa tayari imeuza mafuta ya sh kadhaa. Unapokuja mteja mwingine, wanakuita kwa bashasha, wanakusogeza mbele kabisa, mbali na pampu kiasi kwamba huwezi kusoma kwenye mashine.. Haraka haraka wanakuuliza mafuta ya sh ngapi? Unapotaja tu, fasta wanaweka mpira kwenye tanki yako na kuendeleza pale alipoishia mteja wa awali.
KWA MFANO
Mteja wa awali amenunua mafuta ya sh elfu kumi, unapokuja wewe na kutaka mafuta ya elfu ishirini, unaendeleza pale alipoishia mwenzio, that means unatoa elfu 20, unapata mafuta ya elfu 10 tu. Ni tabia ya muda, mara kwa mara wateja wanashtukia, wanalalamika lakini uongozi hauchukui hatua yoyote.
Nawaomba EWURA wafuatilie hii kwa mbinu zao, watawanasa. Mwenye gari yoyote ukifika kituo hicho, ukiona unasogezwa mbele mbali na pampu, jua inakula kwako. Ogopa kununua mafuta nyuma ya Boda boda . bajaji au teksi, utaanzia walipoishia wenzio.. Na hela wanayopiga wanagawana muda huo huo hata kabla mteja hujaondoka.