Wizi wa mafuta BP/Puma Sinza Kijiweni

Wizi wa mafuta BP/Puma Sinza Kijiweni

Doulos

Member
Joined
Nov 10, 2009
Posts
15
Reaction score
6
Wana JF.

Leo asubuhi nimetoka kuweka mafuta BP/ Puma ya Sinza Kijiweni kiasi cha Lita 6.

Nimeondoka moja kwa moja kwenda posts ila cha kushangaza gari limenizimikia dar free market.

Huu si wizi huo?!
 
Wana JF.Leo asubuhi nimetoka kuweka mafuta BP/Puma ya sinza kijiweni kiasi cha Lita 6. Nimeondoka moja kwa moja kwenda posts ila cha kushangaza gari limenizimikia dar free market. Huu si wizi huo?!!!!

Kama uliweka lita 6 wizi uko wapi sasa??!! Hatujui unaendesha hummer au gari lako lina hitilafu/misfiring au fuel tank linavuja. Hebu tufahamishe kwanza gari lako na hali yake.
 
U wizi upo hata puma kituo cha mwanamboka wako hivyo, ukitaka kujua kuwa unaibiwa we angalia geji yako ya mafuta, unaweza kwenda sheli nyingine ukaweka utakuta geji yako inapanda, ukienda weka sheli zingine ukiweka mafuta geji haisogei kupanda.
Tatizo u wizi uko kwenye machine zao fuel pump.
 
Sio sinza hata pale kinondoni PUMA Mwanamboka na penyewe sio ni wezi haswa
 
Kabla ya kulaumu weka mafuta kwingine angalia fuel consumption ya gari yako then kama haina tatizo wareport ila pia ukienda kuweka mafuta macho yako yaelekeze kwenye mashine zao ila kama wameset hivyo ni ngumu kugundua pia. Gari yangu lita 6 ni siku mbili kutoka ubungo posta ubungo
 
Puma hapa kijiweni ni wezi balaaa ukienda unakuta wameweka pump vibaya usipo kuwa nao makini wanakuingiza mjini,
Mara mbili walitaka kuniibia nikawaletea balaaa, sasa wamekalili na gari awanifanyii upuuzi
 
Pole sana hao ni wezi na wanaoshangaa lita 6 povu linawatoka wao wanaweka full tank au waende zao huko humu hatutaki mashauzi ushuzi kwendraaaaaa huko kwanza hata gari huna ww
 
Hawa wa Sinza kijiweni wamezidi ni balaa kubwa sana!!!.Mimi na ki stalet changu walinipiga ni siwezi weka tena kituo kile!!!!!!!!!
 
Unaongelea 15000 hapo ww unazo? Asubuhi hii au unashikishwa bomba kwenye daladala tu , unakazi ya kubeza wenzio baada ya kumshauri
 
Wana JF.

Leo asubuhi nimetoka kuweka mafuta BP/ Puma ya Sinza Kijiweni kiasi cha Lita 6.

Nimeondoka moja kwa moja kwenda posts ila cha kushangaza gari limenizimikia dar free market.

Huu si wizi huo?!

Panga siku moja nenda kaweke pale gapco Victoria uone....Lazima geji ipande
 
Aiseee kweli ccm ni ile ile..!!
 
Panga siku moja nenda kaweke pale gapco Victoria uone....Lazima geji ipande
Pale victoria jamaa anajua customer care , nasikia yule bwana mvaa mapama alitokea kenya ndio maana anajua huduma ,na imani pia imemjaa nakumbuka kipindi kile cha mgomo wa wauzaji mafuta alikugoma kugoma kuuza mafuta , yaani unawekewa mafuta huku unaimbiwa mapambio.
 
mi sikuizi naenda na kidumu cha lita tano. ananijazia kwanza kwenye kidumu then nayahamishia kwenye gari. bora nichelewe lakini nisiibiwe!
 
Malalamiko juu ya Kituo cha Sinza sasa ni kilio kilichozoeleka. Watu wamelalalamika kwa miaka kadhaa sasa. Huenda kweli kukawapo tatizo. Mimi nilishaumizwa miaka minne hivi iliyopita. Tangu wakati huo napatazama kama chumbani kwa mama mkwe-siingii.
 
Pale victoria jamaa anajua customer care , nasikia yule bwana mvaa mapama alitokea kenya ndio maana anajua huduma ,na imani pia imemjaa nakumbuka kipindi kile cha mgomo wa wauzaji mafuta alikugoma kugoma kuuza mafuta , yaani unawekewa mafuta huku unaimbiwa mapambio.
Yule mmiliki anaitwa matembo amekaa sana nairobi kna wakati nlikuwa napiga mishe huko yeye alikuwepo huko kabla hajaokoka huko alikuwa ni maf. ..balaa siku hzi kamrudia mungu anakwambia, mm nikienda Victoria akiwepo ah lazima anipe lita 5 za wwese. ..jamaa ana stori ndefu sana hata ule mguu wake unaona anachechemea ni balaaa a hahahah, utajiri una stori ndefu watu kupata
 
mi sikuizi naenda na kidumu cha lita tano. ananijazia kwanza kwenye kidumu then nayahamishia kwenye gari. bora nichelewe lakini nisiibiwe!
Ukienda na kudumu lazima wauzaji wakununie
 
Back
Top Bottom