Wizi wa laptop na simu ndani ya mabasi Morogoro

wizardxp

Senior Member
Feb 15, 2017
141
40
Kumekua na wizi wa laptop na simu ndani ya mabasi pale Morogoro pindi watu wakishuka kwenda kutafuta chakula.

Mara nyingi hutokea kwa mabasi yanayopita muda wa jioni, zaidi hutokea kwa mabasi yanayotoka Dodoma. Nimeona sio vizuri kutaja aina ya mabasi hayo. Nini kifanyike kupunguza kero kama hiyo?
 
umeniwahi na hilo swali mkuu. Kwa uzito upi hasa wa hiyo laptop au simu mpaka uiache ndani ya basi?
Itakuwa ni ule ubrotherman mtu kakaa na pisi kali anaacha kibegi chake kwenye siti ili aonekane hajali vitu vidogo.
Hapo hakuna wizi ni kwamba umewawekea walimwengu rizki yao. Wizi ni pale unapoporwa.
Sure Kiongozi. Bongo ujinga mwingi.
 
muda wa jioni, zaidi hutokea kwa mabasi yanayotoka Dodoma. Nimeona sio vizuri kutaja aina ya mabasi hayo. Nini kifanyike kupunguza kero kama hiyo?

Kuna asiyejua kwamba Tanzania hakuna uaminifu? Kama una vitu vyako vya thamani usiache bag lako nyuma shuka nalo.
 
Mali uloingia nayo kwa gari sio dhamana ya dereva/konda/mwenye gari - endapo eneo husika mikasa hiyo hutokea mara kwa mara ni bora ukapataja --- utaanza weka screpa za laptop kwa begi ka chambo ya kuwanasa wahusika

abiria chunga mzigo wakoooo
 
Yaani unaacha simu ndani ya bus huu ni uzembe. Laptop unaiachaje ndani ya bus kisa kwenda kuchimba dawa na kununua machungwa.

Muda mwingine tuwe waangalifu tunaposafiri.
 
UTAACHAJE BEGI LENYE LAPTOP NA NYARAKA ZAKO MUHIMU NDANI YA BUS....

Ova
 
Hawawezi kuwa serious, unaachaje laptop ndani ya bus kwa mfano, typical uzembe na wawaibie Tu wewe na hao wenzio
 
Back
Top Bottom