Carina
Senior Member
- Jan 4, 2011
- 190
- 65
Ndugu zanguni napenda kuwasimulia yaliyonikuta weekend hii katikati ya jiji kwenye parking ya serikali, ni kwamba nilitoka bank kudraw some amount (kama 1m) hivi kisha nikaiweka kwenye gari lakini ndani kwenye dashboard kwa chini pale mlango wa abiria, kisha nikaenda kufanya some shopping maduka ya karibu, nikarudi baada ya nusu saa.
Hapo ndipo niliposhikwa na mshangao nimekuja garini na kukuta hela zote (1m) hakuna na gari haijavunjwa kioo wala mlamngo. walichofanya (wezi hao) wametoboa kwa juu ya kioo kisha wakabetua ile lock kwa ndani na kufungua mlango kilaiiini na kuchukua chao.
Maswali:
Je huu ndio mtindo wa kisasa wa kuwaibia watu kwenye magari jijini? manake sikuwa najua hii kitu, kama na nyie hamfahamu napenda kuwajulisha sasa huu wizi wa namna hii upo na mnatakiwa kuwa makini mnapodraw hela Bank, na nahisi kuna kundi la watu wanafuatilia watu wanaotoka Bank.
Je kwenye Parking areas za serikali ni kwamba hakuna ulinzi au ndo ile parking at your own risk?? kwani gari ina alarm kabisa lakini cha kushangaa wale wa parking hawakusikia chochote.
Pili, je ni hatua gani natakiwa nichukue ili haki itendeke kwani inavyoonekana wale jamaa wa parking system watakuwa wanahusika kwa njia moja ama nyingine.
Ni hayo tu