Wizi wa kwenye magari mchana kweupee .........

Carina

Senior Member
Jan 4, 2011
190
65
Ndugu zanguni napenda kuwasimulia yaliyonikuta weekend hii katikati ya jiji kwenye parking ya serikali, ni kwamba nilitoka bank kudraw some amount (kama 1m) hivi kisha nikaiweka kwenye gari lakini ndani kwenye dashboard kwa chini pale mlango wa abiria, kisha nikaenda kufanya some shopping maduka ya karibu, nikarudi baada ya nusu saa.

Hapo ndipo niliposhikwa na mshangao nimekuja garini na kukuta hela zote (1m) hakuna na gari haijavunjwa kioo wala mlamngo. walichofanya (wezi hao) wametoboa kwa juu ya kioo kisha wakabetua ile lock kwa ndani na kufungua mlango kilaiiini na kuchukua chao.

Maswali:

Je huu ndio mtindo wa kisasa wa kuwaibia watu kwenye magari jijini? manake sikuwa najua hii kitu, kama na nyie hamfahamu napenda kuwajulisha sasa huu wizi wa namna hii upo na mnatakiwa kuwa makini mnapodraw hela Bank, na nahisi kuna kundi la watu wanafuatilia watu wanaotoka Bank.

Je kwenye Parking areas za serikali ni kwamba hakuna ulinzi au ndo ile parking at your own risk?? kwani gari ina alarm kabisa lakini cha kushangaa wale wa parking hawakusikia chochote.

Pili, je ni hatua gani natakiwa nichukue ili haki itendeke kwani inavyoonekana wale jamaa wa parking system watakuwa wanahusika kwa njia moja ama nyingine.

Ni hayo tu
 
Nakupa pole..
 
Sijajua umri wako na umakini wako katika kutunza pesa

1. Umetoka bank na pesa ukaiacha kwenye gari bila kujua kama unafuatiliwa........ukitoka bank na pesa always make sure yu dont have a tail....nor abandon the cash in a car........ushawishi uliufanya wewe

2. Miliono moja jamani ilikuwa ni kwenda nayo tu mbona inakaa mifukoni bila ya shida?????

Never leave valuables unattended.....!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
a,e,i,o,u.

sijui kama bado unamkumbuka mwalimu wako aliyekufundisha kusoma na kuandika.

elimu bado inaendelea, kwa mwalimu usiyemjua.

pole ndugu, uwe mwangalifu kutunza fedha na vitu vya thamani.
 
Pole sana ndugu' kweli mjini SHULE! siku hizi nikuwa makini.
 
Simuamini yeyote, popote! Siweki pesa kwenye gari ng'o! Hata kama ni buku! Nazifunga kwa handkerchief bank huwa wanacheka sana, kama ni m kushuka chini nazipakia kwenye brazia fasta na kwenye pochi nabakiza kiasi kidogo mayb for fuel etc!

Kwa kifupi maisha yamekuwa magumu sana, kila kiumbe kinatafuta unafuu, pole lakini!
 
Hapo ndipo niliposhikwa na mshangao nimekuja garini na kukuta hela zote (1m) hakuna na gari haijavunjwa kioo wala mlamngo. walichofanya (wezi hao) wametoboa kwa juu ya kioo kisha wakabetua ile lock kwa ndani na kufungua mlango kilaiiini na kuchukua chao.

sijajua tofauti ya hayo maneno mawili..pole anyway,hii ndo daslam
 
Pole sana ndugu, tunajifunza kutokana na makosa, Muombe Mungu atukurudishia maradufu!,
 
Siku ingine, kama ni lazima sana kuacha pesa kwenye gari basi uiweke sehemu ambayo ni unexpected kabisa.
 
Kama umelipia na umepewa risti na hiyo kapuni ya kupaki, unaweza peleka polisi malalmiko kisha ukatoa ushahidi, hiyo kamapuni ya parking itakulipa.
Note; Je unaushahidi gani uliacha 1m ndani ya gari?, je baada ya kuona kioo kimetendwa ulimwita mtu wa parking na kumwoshesha na evidence zinatosheleza? if yes file a case. Kama mtanzania usiogope kupoteza muda, utasadia jamii na wewe binafsi pia.
 
Pi a roho mbaya za jamii huchangia sana wizi huu sababu yeye hana gari anatembea kwa mguu ata akimkuta mtu anavunja anajipitia tu ,usiniambie hakuna aliyewaona wezi ni.wapo ila walinyamaza ukaibiwa .jamii pia ikiamini cha mwenzio ni chko itasaidia sana kutokomeza wizi huu
 
Ndugu zanguni napenda kuwasimulia yaliyonikuta weekend hii katikati ya jiji kwenye parking ya serikali, ni kwamba nilitoka bank kudraw some amount (kama 1m) hivi kisha nikaiweka kwenye gari lakini ndani kwenye dashboard kwa chini pale mlango wa abiria, kisha nikaenda kufanya some shopping maduka ya karibu, nikarudi baada ya nusu saa.

Hapo ndipo niliposhikwa na mshangao nimekuja garini na kukuta hela zote (1m) hakuna na gari haijavunjwa kioo wala mlamngo. walichofanya (wezi hao) wametoboa kwa juu ya kioo kisha wakabetua ile lock kwa ndani na kufungua mlango kilaiiini na kuchukua chao.

Maswali:

Je huu ndio mtindo wa kisasa wa kuwaibia watu kwenye magari jijini? manake sikuwa najua hii kitu, kama na nyie hamfahamu napenda kuwajulisha sasa huu wizi wa namna hii upo na mnatakiwa kuwa makini mnapodraw hela Bank, na nahisi kuna kundi la watu wanafuatilia watu wanaotoka Bank.

Je kwenye Parking areas za serikali ni kwamba hakuna ulinzi au ndo ile parking at your own risk?? kwani gari ina alarm kabisa lakini cha kushangaa wale wa parking hawakusikia chochote.

Pili, je ni hatua gani natakiwa nichukue ili haki itendeke kwani inavyoonekana wale jamaa wa parking system watakuwa wanahusika kwa njia moja ama nyingine.

Ni hayo tu

Hao wezi hakika wapo kwenye parking zote na ndio fani yao. Wakati mwingine wanatoa msaada, kwa mfano wakati fulani pale parking nyuma ya Forodhani nilijisahau nika-lock gari bila kuzima na walinisaidia kufungua. Walichofanya ni kupenyeza bisibisi kwenye mlango kwa juu na kupanua kidogo kisha waya mrefu unabonyeza autolock na kufungua. Ilichukua kama dk. 2 na wakanionya nisiache vitu vya thamani ndani ya gari.

Pole sana Ndugu Carina. Experience ni mwalimu mzuri sana, anakupa mtihani kwanza kisha somo baadae, nadhani utakuwa umejifunza kuwa makini na kutoach vitu vya thamani ndani ya gari.
 
Last edited by a moderator:
Simuamini yeyote, popote! Siweki pesa kwenye gari ng'o! Hata kama ni buku! Nazifunga kwa handkerchief bank huwa wanacheka sana, kama ni m kushuka chini nazipakia kwenye brazia fasta na kwenye pochi nabakiza kiasi kidogo mayb for fuel etc!

Kwa kifupi maisha yamekuwa magumu sana, kila kiumbe kinatafuta unafuu, pole lakini!

We noma lol!
 
Inaonekana unaiamini gari yako sana,ivyo ndo maana ukaiamini, chakufanya usiamini garikwani hata nyumbani yanaweza kutokeahayo. pole mkuu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom