Nimeisoma na kuikiubali hii thread ya Kamembe, ila mara nyingi wizi mkubwa hufanyika wakati wa kusafirisha masanduku:
Kinachofanyika huwa ni kubadilisha kura ndani ya masanduku na kuyajaza za ccm, halafu fomu alizotaja Kamembe zinabadilishwa. Ni wazi kuwa fomu zilizobadilishwa hazitakuwa na saini za mawakala wengine isipokuwa wa ccm ambaye anahusika moja kwa moja na ubadilishaji huo. Mnapofika kwenye jimbo wakati wa majumisho na kuhakiki, utaona matokeo katika fomu ya wakala wa chama cha upinzani (CHADEMA) ni tofauti na yanayotajwa na msimamizi! Hapo patatokea malalamiko, fomu ya wakala wa ccm itasema sawa na msimamizi alivyosoma, lakini ya CHADEMA tofauti - ubishi huo utapelekea kuhakiki physically kilichomo ndani ya sanduku; hapo ndipo utakuta viroja -kura zimeshabadilishwa ndani ya sanduku, utakuwa huna ujanja tena maana sanduku ndiye msemakweli!
Ndiyo maana mimi nikapendekeza wakala kunukuu namba za karatasi za kupigia kura ili wakati wowote namba hizo hizo ndizo ziwemo ndani ya sanduku- period
Hii itafanya wizi uwe mgumu kwani itabidi wawe na karatasi zenye kufanana namba, na wawe wamepredict vituo watakavyoshindwa.
Pili nikasema wakala aandamane na sanduku lake hadi mwisho wa safari kwa msimamizi wa jimbo na si kwa mtendaji wa kata.
Mkakati narudia tena hapa
unganisha na elimu nzuri ya Kamembe)
Kwa kuwa kila karatasi ya kupigia kura huwa ina namba, na kwa kuwa kila msimamizi wa kituo hukabidhiwa vitabu hivyo kwa namba; yafuatayo yafanyike
1)Kila chama kipate nakala ya namba za vitabu vya kupigia kura vilivyopelekwa kila kituo
2)Mawakala waelekezwe kunukuu namba za vitabu kwenye kituo kabla upigaji kura haujaanza na msimamizi awadhibitishie kuwa hivyo ndivyo vitabu alivyopokea toka msimamzi wa jimbo
3) Iwe ni lazima kwa kila wakala kusaini fomu ya matokeo kituoni na kama ana malalamiko yoyote yale ajaze kwenye fomu ya malalamiko (unajua mkiachia wa CCM pekee akasaini, hata ikijabadilishwa anatafutwa huyo mmoja anasaini na mchezo unakuwa umeisha)
4) Wakati wa kuhesabu kura, iwe vituoni au wakati wa kuhakiki katika ngazi ya jimbo (ambako huwa ndipo matokeo huwa yameshachakachuliwa), kila sanduku la kura lihesabiwe peke yake na ihakikishwe kuwa namba za karatasi zilizozomo zinaoana na namba alizokuwa amekabidhiwa msimamizi wa kituo na mawakala wawe wametoa taarifa kwa vyama vyao juu ya namba zilizotumika kwenye vituo vyao.
5) Kwa kuwa mawakala ndio wameaminiwa na vyama vyao, wayasindikize masanduku ya kura hadi jimboni pale uhakiki na utangazaji unapofanyikia. Kuyasindikiza hadi kwenye kata na kuishia hapo hutoa mwanya kwa watendaji wa kata kushirikiana na CCM kuyabadili. Sanduku lolote litakalowasilishwa bila mawakala litengwe na lihasabiwe tofauti na kama litakuwa na kura tofauti na fomu za mawakala, likataliwe - Nakumbuka hii ilifanyika Temeke wakati Mrema akigombea. Ni marufuku mawakala kusafiri tofauti na masanduku yao - magari yabebe masanduku kidogo na mawakala.