Wizi wa fedha Exim bank Arusha branch

Wizi wa fedha Exim bank Arusha branch

Huyu mleta uzi kama katumwa vile...nadhani nae hana taarifa kamili anatoa za juu juu tu na kuanza kusiliba, au hao walioibiwa niwajinga kias gani wakae kimya tu nawewe ndo ulalamike? Kuna kitu hapa...maana hata join date yake inaonesha lengo lake ilikua ni kuleta huu uzi....
Kwan tatizo nn?ndiyo anajarib kutafuta msaada sasa
 
Kuna mmoja alimuoa demu wangu kisha akamsaliti na chotara moja ya kiarabu. Baadae ishu ya exim ikamsimamisha kazi akarejea kwa mkewe. Nimemsahau jina lbd atakuwa mmoja wao.
 
WAFANYAKAZI WA EXIM WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 27 JELA KWA KOSA LA UTAKATISHAJI NA UHARIBIFU WA NYARAKA


WAFANYAKAZI wa Benki Ya exim waliokuwa wanakabiliwa na makosa 318 ikiwa ni pamoja na kugushi,kuharibu nyaraka,na utakatishaji fedha haramu na wizi wa dola za kimarekani 521,000 wamehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela huku wafanyakazi wengine saba wakiachiliwa huru kutokana na mahakama kushindwa kudhibitisha makosa yao



Aidha wafanyakazi hao wamehukumiwa mapema leo kwenye MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha/Arumeru ambapo wamekutwa na hatia mbalimbali kinyume cha sheria.



Akisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya masaa 5 kuanzia saa 4.30 asubuhi hadi saa 9.07 Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Deusdedit Kamugisha aliwataja aliowatia hatiani ni pamoja na mshitakiwa namba mbili Liliani Mgeye{33},Daudi Nhosha{39},Doroth Cjijanja{50},Genes Massawe{32},Christopher Lyimo{34} na DeusdediT Chacha{35}.



Alisema watuhumiwa wengine waliokutwa na makosa ya kugushi nyaraka na kuharibu nyaraka ambao ni pamoja na Nhosha Massawe na lyimo wamehukumiwa kwenda jela miaka minne kila mmoja kwa kosa hilo.


Hakimu Kamugisha aliwataja walioachiwa huru na mahakama baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha katika ushahidi wao kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo ni pamoja na mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ambaye alikuwa meneja Mkuu wa Exim Benki{T} ltd tawi la Arusha Bimel Gondaili.


Wengine ni pamoja na Livingstone Mwakihaba{37} maarufu kwa jina la ‘’stone’’,Joyce Kimaro{36},Evance Kashebo{40},Tutufye Agrey{32},Joseph Neki{30} na mfanyabiashara Gervas Lubuva{54}.
Moderator pandisha hii update pale juu
 
Ila inauma asee alafu alikuwa afunge ndoa soon,kaacha mchumba mzuri kweli aisee
Mhhhhh mbona mwanamke wa kawaida sana au hizo picha zinakuzuzua?

Hujamuona live? Labda kama ugonjwa wako ni boobs

Na mark x yenyewe ilikuwa ya demu
 
Pole mkuu inauma sana,kama umethibitisha transactions hukuzifanya/hamkuzifanya wenyewe ni mkondo wa sheria tu.Benki zote ziko covered na bima ivo kuchelewesha kiwafikisha kwene sheria ni kuchelewesha haki zako,sio lazima uende mahakamani lah Bali kamata wakili na mpe mchomgo alafu mtokee manager wa branch ukiwa na wakili wako na uwaeleze muelekeo wako baada ya majibu Yao,kazi ya kufatilia walioiba sio kazi ya mteja ni kazi Yao na haifai kwa namna yoyote wewe kucheleweshewa au haki yako ya kibenki kuingiliwa,once ukiingia na wakili kitaeleweka,walishatoa pesa ya marehemu ndugu yangu na nilipoomba bank statement kulionekana taarifa za miamala ata baada ya jamaa kufariki uku karatasi ya muamala wake WA mwisho ukionesha nini kilikuwa kwene a/c ambayo kwa wakati huo a/c ilionekana haina ata shilingi!
Walinizungusha na nilipopeleka wakili na kuwaambia nia ya kesi kwao (bank) na sio mfanyakazi alioiba akakimbia....haraka walikaa na wakatoa ile pesa.
Asante.
 
Kuna mmoja alimuoa demu wangu kisha akamsaliti na chotara moja ya kiarabu. Baadae ishu ya exim ikamsimamisha kazi akarejea kwa mkewe. Nimemsahau jina lbd atakuwa mmoja wao.

So mzee jama aakiwa kisongo wewe ukawa unapiga ile Mtalaka atongozwi ?
 
Back
Top Bottom