Wizi wa fedha Exim bank Arusha branch

Wizi wa fedha Exim bank Arusha branch

Na ndio hapo umuulize mtoa mada aseme vizuri....otherwise hata mi simuelewi japo habari ya wizi niliisikia

Jamani hata mimi ndo ninaiona hii habari...lakini mbona raia mwema inaeleza wazi. tatizo tunapenda kutafuniwa na kumezeshwa...someni raia mwema ili muone exim walivyo manyemela.
 
Huyu mleta uzi kama katumwa vile...nadhani nae hana taarifa kamili anatoa za juu juu tu na kuanza kusiliba, au hao walioibiwa niwajinga kias gani wakae kimya tu nawewe ndo ulalamike? Kuna kitu hapa...maana hata join date yake inaonesha lengo lake ilikua ni kuleta huu uzi....

Kwa hiyo mkuu kuna joining date katika jf ili uhalali wako wa kutoa maoni uonekane? Wewe vipi bana, unaniambiaje mimi niliye join karibuni? Umenikera mwana jf...au na wewe ni mfanyakazi au kibaraka wa exim nn? Waache watanzania wa join everyday na watimizi right yao ya kutoa mawazo anytime...acha kucritisize joining date ya wana jf...criticize maada hasa baada ya kuisoma vizuri. Maana hata wewe una joining date yako...au na wewe ulivyo join 3/11/2010 ulikuwa una maada yako binafsi tofauti na kutoa kutaka kuwa kati ya wana jf? Kama ndo hivyo basi ni bora ujitoa jf...alafu unaonekana kama kibaraka vile!!! Nasema haya yote maana mimi umenikera mkuu...kila mtu ana haki ya kujoin any date na any day anayofeel like yeye na sio lazima iwe kwa spefic matter...na hata kama ni hivyo bado ana haki hiyo...who are you to judge joining date of a member? watu wengine bwana...kama vile wanatumwagwa!!!
 
Mwana jf, kweli mi ndo nimeisoma hii issue kwenye raia mwema na inauma kuona pesa nyingi kiasi hiki zinaibiwa na watu walio wachache...na kama ni kweli basi haina budi exim warudishe hizi hela. Bona pia wamewashtaki wafanyakazi wao waliohusika na wizi huo? kwa ufahamu wangu kidogo mimi naona watakuwa wameiba kweli ndo maana benki wawafikisha watu hawa mahakamani. na kama ndo hivyo kwa nini hawa watu wasirudishiwe hela zao? exim kuweni waungwana kama vile mlivyowapokea wateja wenu siku ya kufungua akaunti zao bas vivyo hivyo watendeeni uungwana huo...ni busura ndogo tu inatakiwa kutumika hapa.
 
Kwa hiyo mkuu kuna joining date katika jf ili uhalali wako wa kutoa maoni uonekane? Wewe vipi bana, unaniambiaje mimi niliye join karibuni? Umenikera mwana jf...au na wewe ni mfanyakazi au kibaraka wa exim nn? Waache watanzania wa join everyday na watimizi right yao ya kutoa mawazo anytime...acha kucritisize joining date ya wana jf...criticize maada hasa baada ya kuisoma vizuri. Maana hata wewe una joining date yako...au na wewe ulivyo join 3/11/2010 ulikuwa una maada yako binafsi tofauti na kutoa kutaka kuwa kati ya wana jf? Kama ndo hivyo basi ni bora ujitoa jf...alafu unaonekana kama kibaraka vile!!! Nasema haya yote maana mimi umenikera mkuu...kila mtu ana haki ya kujoin any date na any day anayofeel like yeye na sio lazima iwe kwa spefic matter...na hata kama ni hivyo bado ana haki hiyo...who are you to judge joining date of a member? watu wengine bwana...kama vile wanatumwagwa!!!
Ishu ni kwamba wewe ndio umekua mlalamikaji wa hao unaosema wameibiwa halafu unaishia kusiliba badala ya kuweka wazi kilichotokea ili nasisi tu judge kwa uelewa wetu....kuibiwa banks ni kitu kinatokea mara nyingi hata majuzi majambazi waliiba tena wakiwa na sare za kipolisi...sasa sijakuelewa ni kwa vipi usitupe full storry maana kwenye wizi wa fedha kuna mambo mengi tofauti na tunavyofikiria, kwani wateja, wafanyakazi wote huwa ni sehemu ya wizi kutegemea na mazingira
 
Jamani hata mimi ndo ninaiona hii habari...lakini mbona raia mwema inaeleza wazi. tatizo tunapenda kutafuniwa na kumezeshwa...someni raia mwema ili muone exim walivyo manyemela.
Na mmewakomalia kweli hao exim, ngoja tukasome mkuu
 
Jamani hata mimi ndo ninaiona hii habari...lakini mbona raia mwema inaeleza wazi. tatizo tunapenda kutafuniwa na kumezeshwa...someni raia mwema ili muone exim walivyo manyemela.

Wana JF wengine wanaishi nje ya nchi. Kitu kikiletwa mtandaoni kiletwe kamili sio kutoa references au kuleta homework. Hapa ni jamvini, elezeni kimetokea nini toka mwanzo.
 
Hii kitu ni ngumu sana mm hawa jamaa nawapatana kuna mmoja nimemuwekea dhamana wakati tunasubiri kuna mzee mmoja akawa anamsubiri aliyekua meneja anasema alimpa fedha zake amuwekee kama m6 hivi .sasa atazipataje hizo fedha na kama hawa watu walifanya uzembe kama huu hutegemei kwamba mtu aliyesimamishiwa mshahara toka mwezi wa saba mwaka jana atakakulipa fedha .
 
Kabla ya kuchagua benk unayotaka kuweka fedha zako ni muhimu kufanya research juu ya integrity ya management ya benk kwa sababu sasa benki nyingi sio mahali salama sana!!!
 
Hapa sharia ichukue mkondo wake.......si swala la kusubiriwa. Exim Mwanza haina wateja tena.....so bye bye

Stanbic mwanza waliwahi kunipa hela mbovu ambazo hazifai kabisa,walinichanganyia na hela nzuri
hizi bank zina matatizo gani,kwa tz bank makini ni 2 tu,nbc na crdb,zingine tupa kule
 
Stanbic mwanza waliwahi kunipa hela mbovu ambazo hazifai kabisa,walinichanganyia na hela nzuri
hizi bank zina matatizo gani,kwa tz bank makini ni 2 tu,nbc na crdb,zingine tupa kule

Mh,hapo kwenye red uliza vizuri mkuu
 
Hii issue ni kweli na kesi iko mahakamani na Wafanyakazi wamesimamishwa..... Wizi uliofanywa na wafanyakazi ni wa aina tatu. Wa kwanza ilkuwa ni kucheza na exchange rate hasa kwenye zile kadi za Tanapa na NCAA hapa wafanyakazi waliiba kwa kutumia exchange rate za uongo kwa hili Wafanyakazi wameshtakiwa, Wizi wa pili ni kiasi kupungizwa kwenye account bila maelezo zaidi limetokea kwa wenye makato ya mkopo. Wizi wa tatu ni wale wateja ambao huwa na tabia ya kuwaachia bank tellers pesa na kuondoka ili wafate slip badaye, wengi hela zilikuwa haziwekwi na katika hili bank imejiotoa..
Kesi iko kimyakimya coz nafkiri wameamua iwe hivyo ili kulinda reputation ya Bank ila baadhi ya Wafanyakazi kesi imewakalia vibaya though wanahonga sana ili kesi iishe ila sidhan.
 
Wakuu, kuna taarifa imenipita hizi siku mbili. Kwamba kuna watu wamekamatwa na wako mahabusu kwa sababu ya wizi wa mitandaoni. Nimetaarifiwa kwamba wezi hao wamekamatwa mnamo July 17, 2015 yaani Ijumaa iliyopita na wametangazwa kwenye moja ya TV.

Kwa sababu mmoja wao nimesikia aliwahi kufanya kazi benki hii EXIM, sasa nimekuja mitandaoni kuona kama habari hii imeshaanikwa.

Wenye data zaidi kuhusu hili tuhabarishane maana kuna jamaa tunao mtaani kumbe ni watuhumiwa na tunatakiw akujihadhari nao.
 
WAFANYAKAZI WA EXIM WAHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 27 JELA KWA KOSA LA UTAKATISHAJI NA UHARIBIFU WA NYARAKA


WAFANYAKAZI wa Benki Ya exim waliokuwa wanakabiliwa na makosa 318 ikiwa ni pamoja na kugushi,kuharibu nyaraka,na utakatishaji fedha haramu na wizi wa dola za kimarekani 521,000 wamehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela huku wafanyakazi wengine saba wakiachiliwa huru kutokana na mahakama kushindwa kudhibitisha makosa yao



Aidha wafanyakazi hao wamehukumiwa mapema leo kwenye MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha/Arumeru ambapo wamekutwa na hatia mbalimbali kinyume cha sheria.



Akisoma hukumu hiyo kwa zaidi ya masaa 5 kuanzia saa 4.30 asubuhi hadi saa 9.07 Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Deusdedit Kamugisha aliwataja aliowatia hatiani ni pamoja na mshitakiwa namba mbili Liliani Mgeye{33},Daudi Nhosha{39},Doroth Cjijanja{50},Genes Massawe{32},Christopher Lyimo{34} na DeusdediT Chacha{35}.



Alisema watuhumiwa wengine waliokutwa na makosa ya kugushi nyaraka na kuharibu nyaraka ambao ni pamoja na Nhosha Massawe na lyimo wamehukumiwa kwenda jela miaka minne kila mmoja kwa kosa hilo.


Hakimu Kamugisha aliwataja walioachiwa huru na mahakama baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuthibitisha katika ushahidi wao kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo ni pamoja na mshitakiwa wa kwanza katika kesi hiyo ambaye alikuwa meneja Mkuu wa Exim Benki{T} ltd tawi la Arusha Bimel Gondaili.


Wengine ni pamoja na Livingstone Mwakihaba{37} maarufu kwa jina la ‘’stone’’,Joyce Kimaro{36},Evance Kashebo{40},Tutufye Agrey{32},Joseph Neki{30} na mfanyabiashara Gervas Lubuva{54}.
 
Inaonekana uyo Doroth Chijanja ana undugu na yule jamaa David Chijanja aliepata ajali pale Usa river kwenye Mak x
 
Back
Top Bottom