Wizi wa Fastjet, TCAA mpo kweli?

Mhhh hawa jamaa ni wahuni sana last week, mwanza to dar reporting time saa 6:05 am tumefika 6:10 am tukakuta check in tayari ndege badala ya kuondoka 8:05 am tukandoka 7:05 am nahisi kuna watu waliachwa wasio enda na muda

fastjet ni kawaida yao siku zote kuondoka kabla ya muda. always utakuta one hour before departure wao washang'oa. wanatakiwa wadhibitiwe waendane na ratiba yao walioitoa na sio vinginevyo. ni muhimu sana kama unasafiri na fastjet kuwahi sana airport.
 

Ulichokisema ni ukweli,nchi hii kwa sasa ukikosana na muwekezaji husijidanganye kama utaenda kulalamika sehemu husika ukasikilizwa maana hao wawekezaji ni mianvuli ya wenye nchi
 
Kama mnaweza kujustify hiyo scenario, wasiliana na TCAA-CCC. Ofisi zao ziko PPF tower, hawa ndo wanahusika moja kwa moja na kumlinda mlaji wa huduma za anga. Otherwise poleni sana wakuu.

Ila tayari huyo mtoto tayari amesha chelewa mipango yake kama alikuwa anaenda kuwahi shule au mtihani tayari ni tatizo,hayo malalamiko yatafuata kama formalities
 
mdogo wako alichelewa,next time muwahi maana ndege si daladala.ukishachelewa rules apply,it means km untaka kwenda na ndege ya saa hiyohiyo inabidi ulipe express ticket na ndo hapo badala ya 32000 unalipa 300000.for the same trip.

Hatukatai,kinachotakiwa ni kuhakikisha hiyo sheria inawafikia watumiaji wa huduma husika,vinginevyo wataendelea kutoa lawama
 

Hiyo ndiyo inaitwa bure ghali
 

Hayaja kukuta mkuu,haiwezekani kila mtu akalalamika juu ya fast jet,kutakuwa na tatizo ingawa mimi sijawahi kukutana nalo zaidi ya lugha zisizo njema wa watumishi wake,
 
Ingawa sijui kilichomtekea kijana huyo lakini kwa vyovyote vile haiwezi kuwa kama ilivyoletwa.
Mnapokata ticket hasa kwenye low budget flights ni busara kusoma 'terms and condition' tena isome vizuri tu maana kuna baadhi ya masharti ni budi kuyaelewa. Kwa mfano ukichelewa hurudishiwi nauli na inabidi ukate ticket nyingine, huwezi kubadilisha 'flight' hivyo ukipanga safari ni budi uwe unauhakika kuwa utasafiri siku na muda huo uliyopangwa.
Kwa ufupi kuna mambo mengi yakuzingatia hivyo msafari ni jukumu lake kuelewa masharti hayo.
 
Ila tu chili shirika Huduma Zao si user friend. Kweli MTU upo security check foleni wao close desk bila kuja kucheck na waliokwenye ukaguzi kama mashirika mengine wafanyavyo . Gate check ni moja queue ni ndefu. Wabadilike hapo kiukweli

Wanadai control system yao ipo nairobi
 
Ila tayari huyo mtoto tayari amesha chelewa mipango yake kama alikuwa anaenda kuwahi shule au mtihani tayari ni tatizo,hayo malalamiko yatafuata kama formalities

Mkuu ni kweli kabisa kuwa ameshaathirika, ila tunachoshauri hapo ni namna anavyoweza kupata haki yake ikiwa ni pamoja na fidia kwa athari aliyoipata. Nimemshauri apeleke malalamiko TCAA-CCC kwa sababu hapo ndo mahali pa kuanzia kudai haki na badae hata mahakani, Wakati mwingine inabidi kukomaa dhidi ya hawa mabeberu ili iwe fundisho. Tumefika mahali tuache ile mambo ya KUBALI YAISHE.
 

Ushauri wako ni mzuri ila inategemea na family husika na uwezo na muda wa muhusika
 

mkuu,gharama za uendeshaji wa biashara ya ndege ni kubwa mno,ndege moja ya fast jet airbus A319 inabeba abiria 156(all economy),hebu piga kwa hiyo elf 45 unayolipa hata kama ni wewe mfanya biashara utatoka kweli?unajua bana watu hatuelewi maana ya low cost airline.unapaswa kulipia kile tu unachotumia ambacho ni kiti kwenye ndege na kamzigo kako kadogo ka mkononi ambako kwa wastani hakapaswi kuzidi kilo nane hadi kumi.imagine unaondoka hapa kumi na mbili asubuh moja na nusu uko mwanza ukilinganisha na mtu aliyelipa elf 50 kwa basi hata chalinze hajafika.unataka nini kingine mkuu na elf 45 yako hiyo.kama mtu kachelewa kachelewa,chek in desk inafungwa dk 40 sharp kabla ya muda wa ndege kuondoka,wewe unapaswa kufika pale dk 41 kabla ya safar kwani zikibak dk 40 tu hawapokei abiria.unamlaumu nani kwa hilo?
 

mkuu nadhani umeshahudhuria kwenye foleni za upigaji kura,au hata kwenye mabenki,unakuta ikifika muda flani,wale watakaoruhusia kupata huduma ni wale tu waliokuwa kwenye foleni.ukija zaidi ya muda huo hata kama umewakuta wengine bado wako kwenye folani huwezi pata huduma.inawezekana kabisa dogo alikuta watu kwenye foleni lakini lakini alichelewa zile dk 41 ambazo alipaswa kuripoti kabla ya muda wa ndege kuondoka.

pole zake sana ila siku nyingine ajitahidi kukip tym
 
Kwenye tickets zao kuna maelezo yanayomlinda mteja ikiwa kawafanyiwa ndivyo sivyo. Naambatanisha kipengele hicho hapa chini:

Check-In
Check-in counters
open 2 hours before
departure
Departure Gate
Departure gate
opens 40 minutes
before departure
Hand Baggage (1 Item)
56 x 45 x 25cm
1 item of hand baggage per person is permitted.
* Passengers arriving later than 40 minutes before departure for check-in,
or 10 minutes before departure at the boarding gate will be denied boarding.
 
Kwenye tickets zao kuna maelezo yanayomlinda mteja ikiwa atafanyiwa ndivyo sivyo. Naambatanishaa maelezo hayo hapa chini:

Check-In
Check-in counters
open 2 hours before
departure
Departure Gate
Departure gate
opens 40 minutes
before departure
Hand Baggage (1 Item)
56 x 45 x 25cm
1 item of hand baggage per person is permitted.
* Passengers arriving later than 40 minutes before departure for check-in,
or 10 minutes before departure at the boarding gate will be denied boarding.
 
Hapana fastjet wana mambo ya ajabu sana hasa kwenye ruti ya Mwanza. Kwa sababu ni mbali na unaweza kuta kuna mkubwa au mtu maarufu hakuwa amekata tiketi na amepata safari ya ghafla kwenda Mwanza wanachofanya ndio hicho wanatafuta kisingizio ili tu wampatie yule mkubwa nafasi mimi ndugu yangu yalimkuta lakini kwa sababu anaujua huo mchezo alikimbilia ofisini kwao Mwanza wakamrudishia hela yake.
 
lazima ulipe kiasi fulani na ndio nia yao
Kwa mashirika mengine hata yale ya kimataifa unapobadilisha siku au muda unalipa kiasi fulani cha heia lakin kwa fastjet gharama ya kubadilisha huwa mara mbili mpaka tatu ya fedha uliyolipa mwanzo. Hii inapelekea kama unahairisha safari kuisamehe nauli yako na kutafuta usafiri mwingine au hata kufanya upya booking.
 
NAIROBI PALE NDANI KUNA BANGO LA TCAA LINANAMBA iNCASE UMEONEWA UMEOMBWA RUSHWA NEXT TYM UNAWAPIGIA

CHA PILI AKUNA SHERIA INAYOMKATAZA MTU KUHUDUMIWA NDANI YA FOLENI...HAKUNA NA AIPO..NA NAAMINI KIJANA ALIKUTA COUNTER IMEFUNGWA NA IKIFUNGWA IMEKULA KWAKO WELL KNOWN..SIJUI NISEMEJE HAPO

SWISSPORT AIJAAJIRI MABWEGE KIASI HIKO KUGOMA KUkuhudumia ndani ya fole.i...ikitokea hata kuna msururu sa folen ithahakikishwa unaisha na dly itakuwa juu ya airline .wao wana hakiyakuomba kufunguliwa mapema counter kama wana watu wengi zaidi ya normal waliozoea..
 

Mkuu sidhani kama Fast Jet ni Low cost...
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…