SoNotorious
JF-Expert Member
- Sep 11, 2011
- 2,422
- 859
Ndugu wana JF!
Je mnajua jinsi Bank inayosikiliza "CRDB" inavyoibia wateja wake? Fikiria kila ukitoa pesa kwenye ATM wanakata shs. 700.00. Wanasema kwa siku unaweza kutoa shs. 1,000,000.00. Lakini huwezi kutoa hiyo million moja mara moja utatoa mara tatu na kila ukitoa unakatwa shs. 700/=, kwa ujumla utakatwa shs. 2,100/=, hizo ni hela nyingi sana.
Na ujue kila mwezi unakatwa shs 1,500/= kama reja fee. Sasa huu ni wizi kama ule wa ESCROW.
Watanzania tuamke na tukatae wizi wa mchana mchana.
Naomba kuwasilisha!
Kimbembe kingine ni SIM Banking, kuna makato ya 200 kila ukitaka kujua salio ama ukiingia tu hukoVp na ukienda kuuliza salio wanataka jero au wameacha
Kimbembe kingine ni SIM Banking, kuna makato ya 200 kila ukitaka kujua salio ama ukiingia tu huko
acha upoyoyo!! unataka upewe huduma bure!!? nani wa kukuwekea pesa zako bure? ATM zinafanya kazi bila gharama!!!? katoe pesa zako uweke kwenye kibubu!
Benki sio charity nyie makauzu. Wekeni hela kwenye mtungi basi.
povu lote hilo hamna cha maana umesema! hiyo pesa inakatwa ni ndogo tu. kama mnaona ni kubwa, ilinganisheni na nyingine.Unaweza kujifanya unajua lakn wewe ndo ----- na poyoyo kuliko wote.Mtoa mada hakusema watoe huduma bure.Fairnes ktk biashara ni jambo muhimu sana.Tozo km n kubwa kwa malengo ya kulazimisha faida kubwa mwisho wa mwaka huo ndo upoyoyo na wizi.Km inaruhusiwa kutoa mlıon kwa siku,ya nn iwe vpandevpande.Unaonyesha udhaifu mkubwa kiakili pale unaposema akatoe pesa zake aziweke kwenye kibubu.Elewa CRDB ipo kuhudumia umma na wewe km unafanya kaz hapo usijione ndo mwenye CRDB.
CRDB ukiangalia salio tu simbanking, wanakata, lakini NMB-mobile sijaona haya mambo. Kweli watanzania tunanyonywa.
Hapo ndo nachoka kabisa eti simu isipokuwa na hela huangalii salio wakati nmb mobile hata simu ikiwa empty bado salio unachek
Anayekata vocha ni mtandao wa simu, cjajua kama CRDB wanamiliki ntandao wa simu!! Ila ukita kumtumia mtu Meseji, kama mama yako, crdb, tcra, ....kooote unataka unayemtumia Meseji usikatwe?? Haijakaa saw a, mkuu ukitumia simu lazima Vodacom au AIRTEL watakutoza , iyo sio watu wa benki ni mtandao
Aisee tengeneza likibubu weka mkwanja wako lisukume uvunguni hizo pesa haztakatwa hata mia
Bank charges sawa, lakini mbona kila siku wanapandisha tena bila kumjulisha mteja.
Wabongo mfumo wa ujamaa umetuharibu kweli.. Kama ukitoa milioni kwenye Mpesa unakatwa TShs. 7,000/= unaona kukatwa TShs. 2,100/= kwa ajili ya huduma ya ATM ni wizi kweli..?
Ndugu wana JF!
Je mnajua jinsi Bank inayosikiliza "CRDB" inavyoibia wateja wake? Fikiria kila ukitoa pesa kwenye ATM wanakata shs. 700.00. Wanasema kwa siku unaweza kutoa shs. 1,000,000.00. Lakini huwezi kutoa hiyo million moja mara moja utatoa mara tatu na kila ukitoa unakatwa shs. 700/=, kwa ujumla utakatwa shs. 2,100/=, hizo ni hela nyingi sana.
Na ujue kila mwezi unakatwa shs 1,500/= kama reja fee. Sasa huu ni wizi kama ule wa ESCROW.
Watanzania tuamke na tukatae wizi wa mchana mchana.
Naomba kuwasilisha!
mnatakiwa kuwa feya kwa wateja wenu
sio kuwakamua tu kisa awana pa kutunzia
poor business strategy