Wizi wa aina Yake, Kuweni makini na mtoe tahadhali kwa wengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi wa aina Yake, Kuweni makini na mtoe tahadhali kwa wengine

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by doup, Apr 5, 2012.

 1. doup

  doup JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Jana nimesimuliwa kisa cha ajabu sana kutoka kwa jirani yangu, ambaye ni mama wa makamo wa kunizaaa hivi. Mama alikwenda kwenda kuchukua pesa kwenye ATM kwa ajili ya manunuzi ya sikukuu (kwa wenyeji njia ya kwenda Kitunda au Gongo la mboto) ni pale banana - ukonga kwenye tawi la Akiba.

  Basi anatoka tu kwenye ATM, kaja mama mwingine na kujifanya ametoka Tanga, anaulizia Ofisi za wizara nishat na madini, huku wanatembea kulekea kituo cha daladala jirani akamwabia office hizi anafahamu ziko mjini, kabla hajatoa maelezo ya kina kijana kwa nyuma yao akadakia, aaah office hizo ziko town unauliza huku? mi naelekea huko, ghafla gari saroon inapiga breki, anaelekea town buki(1000), jammaa anawambia kina mama mi nachukua hii niwahi, na yule mama mgeni wa tanga na yeye anasema ngoja na mimi ni pande hii. Jirani bila hisia zozote akajua hawa ni wasafiri wenzangu tumekutana hapa hapa na katika harakati za kutaka kuwai akaamua kupanda hiyo gari wakamuweka kati kiti chanyuma.

  safari akiaanza, wanakaribia Tazara, jirani anawambia mi nashuka hapo, bahati mbaya ilikuwa mida ya kama saa tatu asubuhi hivi, hivyo akuna foreni, jamaa wakapita taa za tazara, jirani akaanza kuhoji imekuwaje? bila hiyana gari nzima wakabadirika mama toa kila kitu ulichonacho kwa usalama wako, kwanza leta hiyo simu!, kung'uta begi. Kufika kituo kinaitwa banda la ngozi wakamshusha hapa kapigwa na butwaa asijue la kufanya.

  Anafika Polisi, anaambiwa mama hata usipoteze muda wako, tumeshapata matukio ya watu hao mengi, lakini hakuna mtu anayetuletea namba ya gari, hivyo hakuna cha kufanya. Jirani akabaki amechoka zaidi, Mungu si Athumani, begi lilikuwa na tundu kwa ndani katika kukagua anapata mia tano ilijificha huko siku nyingi anapanda daladala na kurudi nyumbani kwa uzuni kubwa.


  Tujihadhali, cha kuchangaza kama Polisi wanataalifa na watu hawa, intelejensia yao imeshindwa kufanya kazi kuwanasa?? kweli polisi yetu kimeo kama hakuna maslahi hakuna msada kabisa.
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,054
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Dah! Aisee!
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,517
  Likes Received: 2,259
  Trophy Points: 280
  Intelijensia ya polisi wa bongo? Acha kusumbua wababa wa watu rushwa imekuwa ngumi juu ya mdororo wa uchumi!
  Hii habari ya kupanda taxi na strangers mi staki hata kuisikia! Huwezi kufanya urafiki na mtu mmekutana tu stendi/kituoni,period! Naskia mwenge kuna bajaj zinafanya style ya daladaka nazo, tutasikia mengi zaidi.
   
 4. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bongo yako chaguo lako. I trust no one.
   
 5. s

  sugi JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  daa,kila siku watu wanabuni njia za kujikwamuakimaisha,na tutarajie meeengi sana,hasa baada ya wachuuzi wa ubungo kutimuliwa!
   
 6. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  POLICE imekuwa kimbilio la wengi, lakini pia wengi wameilalamikia. Ninachojua mimi, kazi ya ulinzi ni jukumu la kila mtu. Unapofanyiwa tukio baya, kwanza wewe
  1. umejiandaa vipi usifanyiwe?
  2. umeonesha ushirikiano gani ili kupata haki yako?
  3. unajielimisha kiasi gani kuepuka kuingia kwenye hatari?
  4. unapotendewa mambo yasiyo mazuri unafanya nini ili usaidiwe?

  ni vizuri kila mtu akachukua hatua kabla ya kuomba msaada. unaenda polisi hata namba ya gari hauna, polisi wataanzia wapi kukusaidia? kuwa makini
   
 7. N

  Njangula Senior Member

  #7
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bongo Dar es salam siamini mtu. Nikija huko huwa na tahadhari ya hali ya juu mno!
   
 8. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  duh . . . . .
   
 9. c

  collezione JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Kila siku nalia na polisi wa Tanzania. Walahi, sijawahi kuona nchi kama Tanzania na polisi wake.

  Mliotembea nchi za nje watakubaliana na mimi... Nchi hii hakuna usalama kabisa. mtu yoyote anaweza akafanya uhalifu anavyotaka. Na hamna mtu atakaye kusaidi.

  kwenda polisi ni kutakaa kutapeliwa tena.... Sijawahi ona nchi kama Tanzania.

  Hivi kwanini tunalipa kodi kama polisi hawawezi kutulinda?. Mimi naomba niwaulize waJF. Maana Tanzania hakuna umeme, maji ya shida. Hospital migogoro haishi. MaShuleni hakuna walimu. Miundombinu mibovu... Usalama hakuna...

  Swali, jamani kwanini tunalipa kodi???
  Au tunalipa kodi kuwalipa mishahara kina Jk na wenzake. Ili waweze kusafiri kila nchi??
   
 10. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu, unawauliza polisi na PCB kama rushwa wanapokea? Rushwa yao inapitia accounts na sio mikononi inayojaa haraka. Ukitaka polisi wajitume hakikisha anatapeliwa polisi, tena bosi. Wanajua kila kitu na pengine wanakatiwa kitu kidogo kulinda matukio hayo yasivuje. Ukisikia wamekamata mtu ujue huyo mtu ama alitaka kuwabania au alishawabania na sasa wanamrudi. Polisi yetu ukipatwa na janga usihangaike kuwapigia simu maana watakuambia longolongo tu, sanasana watafika kwenye eneo la tukio wiki mbili baadaye kama una bahati. Ngoja aibiwe afande wa polisi, hapohapo mtu ananaswa.

  Nilienda kituo cha Magomeni na rafiki yangu mmoja aliyeporwa begi usiku na watu waliokuwa na gari aina ya Vitz usiku tena jirani tu na kituo cha polisi maeneo ya Upanga. hatukukumbuka kwamba kuna kituo jirani pale tukaenda Magomeni. Kwa ufupi polisi aliyekuwa counter alikataa kusaidia hata kuchukuwa maelezo ingawa aliambiwa passport, kadi za benki, pesa taslim na document muhimu zipo ambazo wahalifu wanaweza kuvitumia kwa uhalifu mwingine. Polisi hakukubali kusikiliza mpaka wale polisi almaarufu TIGO alipoombwa na kuongea na aliyeko counter, jamaa yangu alilazimika kutoa 60000 ili apate RB kwa usalama wake. Kesho yake akaenda pale kuchukua form akauziwa kila moja 5000 bila risiti na bila mhuri wala sahihi - MAGOMENI KITUO CHA POLISI!!!! Ndipo nikaambiwa kumbe Urafiki na Magomeni ni dugu moja baba yao anaitwa rushwa. Nikachekwa kwa nini nilienda huko bila kuuliza ushauri. Hao ndio polisi wetu. Kisingizio ati maisha ni magumu sana, as if raia wanaishi dunia tofauti na ya mapolisi.

  Ukipata matatizo hakikisha mhalifu anashughulikiwa haraka hapohapo, akipona asimulie wenzake na akidead wenzake watulie angalau kwa wiki moja wakiomboleza mwenzao. Ama sivyo watakutanguliza wewe kifoni. Kama sinema vile, tunaongea kando ya njia tukisubiri jamaa yetu atupitie, ghafla gari ikapita karibu kabisa na jamaa yetu na kukwanyua mkoba uliojaa vitu muhimu sana. Ndio wizi mpya wa siku hizi, wanatumia magari au pikipiki kupora. Saa ngapi utapata akili kusoma namba za gari wakati wamejiandaa kwa uporaji na kuziba namba za nyuma kwa karatasi?

  Nikiona kibaka anachomwa moto niko tayari kumnunulia mafuta ya taa achomeke vizuri zaidi, maana kumpleka polisi ni kujisumbua na kujiongezea gharama isiyo tija. Ukitaka kuamini nisemacho, omba Mungu likufike ushuhudie wewe mwenyewe, utajua naongelea nini.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Karibuni daslamu
   
 12. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jumamosi moja nikiwa k'koo nasubiria basi na mzigo wangu wa vitenge nilionunua dukani akanifata dada mmoja akanisalimia vzr ghafla akajifanya Mkenya kwa lafudhi yake aliyobadilisha akaanza kuniuliza dada "eti kitumbini ni wapi wanakouza vitenge"nikamjibu sijui akaniuliza tena kwa hapa maeneo yanayouza vitenge yako wapi"mi sikumjibu nilimuitikia kwa kichwa ishara ya kukataa akacheka na kuondoka dawa ya watu wanaouliza uliza hasa katika mazingira tata iwe umetk benki kuchukua mkwanja au dukani kununua mzigo ni kuwapa majibu negative ili wakuache ukijiloga tuu ukaanza kuwa positive imekula kwako wengine wana dawa unaweza shangaa umejikuta uko feri hujui umefikaje na kitu pekee ulichobakiwa nacho ni nguo tu ulizovaa baada ya kukombwa kila kitUu!!
   
 13. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #13
  Apr 5, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  Usipande tax za kuchangia
   
 14. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #14
  Apr 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,111
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  naogopa kucomment maana asije akawa amechuku alfu kumi tu kwenye atm alafu tupoteze muda hapa weka kiwango alichoibiwa mpwa
   
 15. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MMmmmm,sijui umuamini nani manake hata mwanamke mwenzio pia nae sie....
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Polisi wanataka waletewe ushahidi badala ya wao kuutafuta. Halafu huo wizi ni wa muda mrefu ila sio maarufu sana.
   
 17. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kila kukicha mbinu mpya za wizi na ujambazi, Police wamekimbilia kupambana na watu walioko kwenye siasa tu
   
 18. Cassava

  Cassava JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 282
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Apewe pole yake, miye mwenyewe huwa nazipanda hizo tex za book pale ubungo kwenda posta kwa tahadhari sana, kabla sijaipanda huwa nasoma namba kwanza.
   
 19. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,696
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Arusha nasikia wapo wezi namna hii ila wako more advanced...yaani wakikukuta wanakuongelesha ukijibu tu au ukipeana naye mkono wanahamisha akili yako wanaanza kukuremote. Wanaenda na wewe home unaingia ndani unawatolea kila kitu chenye thamani eg pesa, simu, gold items etc. Na ili wasiweze kufanya hivyo inabidi atakeyeshitukia gemu akuzabe kibao ndio akili inarudi kwenye line.
   
 20. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Tutalaumu polisi bure kwa matukio kama hayo na hasa mwanzo mwanzo.

  Jee polisi wasimamishe kila gari waichunguze au mulitaka wafanye nini hapo?

  Angalau kungekuwa na namba ya gari au hata kitambulisho cha mmoja wao ndiyo tungelaumu lakini mmmmh mengine jamani!
   
Loading...