Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,489
- 14,356
Habari zenu wana Jamii!
naandika habari hii kwa masikitiko, jana majira ya saa 5 asb nilienda kupata huduma ya M-Pesa pale Ubungo Plaza, nilikua naenda kutoa pesa katika account yangu. cha kushangaza yule dada aliyekua ananihudumia aliniambia nifanye process zote mpaka alipopata msg kwenye simu yake, baada ya hapo akachukua simu yangu akawa ana bonyeza bonyeza, akanipa pesa ambayo nilikuwa natoa ilikuwa ni shilingi elfu Hamsini (50,000), akaomba kitambulisho nikampa akafanya process zote akanirudishia kitambulisho pamoja na simu yangu.
niliondoka pale na kuelekea Mlimani City,sasa nikawa nataka kununua muda wa maongezi kwa M-Pesa, kila nikajaribu ikawa inaniletea ujumbe kuwa sina Pesa ya kutosha kununua Muda wa maongezi na nilikuwa nataka kununua sh 5,000, nilijaribu mara tatu bila mafanikio nilipoangalia salio la M-Pesa ikaniambia ni sh 1370, nilipigwa na butwaa kwa sababu wakati naenda kutoa M-PESA nilikua na sh 62,250, moja kwa moja nikajua yule dada atakua amechakachua hela yangu zaidi ya shiling 11,000. sikutaka kurudi kuuliza wala kupiga simu Voda com.
naandika hapa najua kuna watu wa Vodacom mtaona na kujua kuwa baadi ya wafanyakazi wenu sio waaminifu. na anaharibu sifa ya kampuni.
WANA JAMVI KAMA MNATAKA KUTHIBITISHA NENDENI MKAJARIBU KUTOA PESA ZENU PALE UBUNGO PLAZA MAANA TABIA YA MTU MWIZI HAIKOMI SIKU MOJA NA NYINYI MTAKUJA KUTOA USHUHUDA..
KUNA RAFIKI NIMEMWAMBIA AKAJARIBU KESHO NA ACC0UNT YAKE IWE NA PESA NYINGI KIDOGO ILI AWEKE MTEGO.
NAWASILISHA