Faru Jenny
Senior Member
- Dec 29, 2016
- 101
- 71
Wadau wa JF habari za jioni. Nimetoka Masama Moshi kwenye mazishi ya Mama EvaGrace Emmanuel Lazaro Mwasha mke wa Askofu mstaafu wa kanisa la TAG. lakini ajabu tulivyofika TENGERU basi zima tumetangaziwa kuwa makini na wezi wa simu na vitu vingine kwa abiria. Hii imenitokea mara nyingi sana nikisikia Tahadhari hii. Nyie watu wa TENGERU badilikeni kwa kweli. Mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti na mbunge Joshua Nassary je hamuwezi kufanya kitu kuondoa Sifa hii mbaya kwa eneo hili, jiji la Arusha na Tanzania kwa ujumla? Maana hata watalii wengi "wamelizwa" Mali zao hapa.
Nawasilisha!
Mkuu sio Tengeru ya sasa unayoongelea. Tengeru inahistoria hiyo na sio ilivyo kwa sasa. Kiujumla ongezeko la watu kuja limebadi sana tabia za wameru. Wameru ni kabila ambalo sio maarufu sana kwa watanzania ambao hawajafika Arusha.
Watu wengi wamewafahamu wameru baada ya kufika Arusha. Ni watu wenye asili ya ukorofi, ubabe, wakabila (hawapendi sana watu kuja) ila mazingira yamewabadili kwa lazima.
Wenyewe wanaonaga fahari kusifiwa wababe na wakorofi lakini mbali na hayo hawana sifa chanya nyingi zaidi ya kujifia kutoa mkuu wa majeshi (Sarakikya) na kutuma muwakilishi wao wenyewe kudai uhuru wa wameru kwa malkia Uingereza enzi za ukoloni.
Wameru wa sasa jeuri yao inaishia mto nduruma kama unaenda mjini na Usa kama unaelekea Moshi. Hiyo ndio teritory yao ya kujidai.
Nakuaga bar moja inaitwa Sumni hapa Tengeru. Vijana ni wapole kabisa siku hizi hawana matata. Uhalifu ni wa kawaida tu kama wa maeneo mengine sio ule wa zamani uliokuwa distinguished kwa Tengeru pekee.