dafity
JF-Expert Member
- Aug 16, 2008
- 1,858
- 2,059
Wadau wa JF habari za jioni. Nimetoka Masama Moshi kwenye mazishi ya Mama EvaGrace Emmanuel Lazaro Mwasha mke wa Askofu mstaafu wa kanisa la TAG. lakini ajabu tulivyofika TENGERU basi zima tumetangaziwa kuwa makini na wezi wa simu na vitu vingine kwa abiria. Hii imenitokea mara nyingi sana nikisikia Tahadhari hii. Nyie watu wa TENGERU badilikeni kwa kweli. Mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti na mbunge Joshua Nassary je hamuwezi kufanya kitu kuondoa Sifa hii mbaya kwa eneo hili, jiji la Arusha na Tanzania kwa ujumla? Maana hata watalii wengi "wamelizwa" Mali zao hapa.
Nawasilisha!
Nawasilisha!