Wizi mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi mpya

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by echuma, Aug 11, 2012.

 1. echuma

  echuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Jamani jihadharini na wizi huu

  Nimepigiwa simu na mtu nisiemfahamu akajitambulisha anaitwa Bwana Mrisho akajifanya ananifahamu hadi sehemu yangu ya kazi, nikamuuliza anashida gani akasema eti yeye kwa sasa yuko Arusha anafanya kazi na kampuni ya GTI mwaka sasa na wanashugulika na kutoa chanjo kwa wanyamapori.

  Dhumuni la yeye kunipigia simu kulikuwa na mambo mawili kwanza ni wanafungua ofisi mpya Masaki hivyo wangehitaji msaada wangu kuwaonyesha vifaa na watumie njia gani ili wafanikiwe katika biashara yao,la pili akasema yeye ni Operation manager kwenye hiyo kampuni na kwa sasa kuna wazungu wake wako sea cliff hotel wamekuja na ndege yao kutoka ujerumani iko airport na wapo kwenye kikao ila saa sita kinaisha, baada ya hapo watahitaji kuonana na supplier wa dawa za mifugo ili awapatie dawa na supplier wa mwanzo alipata scholarship ambapo yeye na mhasibu huwa wanapata kitu kidogo kutoka humo so wanataka mimi nikaonekane kama supplier halafu kwenye mgao na mm watanipa nikawambia NDIO.

  *Akanitumia namba za dokta ambae anauza hzo dawa niongee nae nimwambie mimi ni mjasiriamali nlikuwa nahitaji pea 50 ,nikampigia akasema bei ya wajasiriamali ni 2.5 milioni kwa pea moja akauliza nahitaji pea ngapi nikamwambia akasema mzigo umeingia juzi hvyo zipo, nikampigia tena Mrisho nikamwambia zipo akasema niuulize tena kwa sasa vitu viwili bei ya package( dawa zitasafirishwa hvy kuna package wanafanya ili zisigusane) pamoja na risiti plain ili ndio tuje tubadilishe bei halafu yeye anaongea na mhasibu waweke cha juu shilingi ngapi?mhasibu yeye yuko sea cliff na wazungu nikapiga akasema package 400,000 na risiti 200,000 halafu yeye akapata jibu cha juu ni 500,000 kila pea mgawo utakua 800,000 kila mmoja nyingine ndio zitamaliza pesa ndogondogo zitakazohitajika. ila dokta alisema kutokana na wajasiriamali kuwa waswahili muda mwingine hivyo tunatakiwa tulipe laki sita kwanza ya package na risiti.

  *Akanambia watanipigia wazungu kuuliza kama nauza hzo dawa zinaitwa GUSTAVIC(ya ujerumani) nauza na bei gani ok wakapiga wakahitaji pea 50 ambapo niliwaambia bei 3,000,000 malipo nikawambia pesa sio cheki na iwe ni tsh sio usd akasema sawa atanipigia baada ya muda mfupi.

  Akapiga tena Mr Mrisho akisema wazungu wamefurahi kuongea na mm na wako willing kutoa hiyo pesa ila wapo wanafanya mchakato na mhasibu ili watoe pesa ila kuna tatizo moja *yeye yuko porini na pesa anazo ila ziko benki hivyo ili dili lisiharibike inabidi nitafute mahali hiyo laki sita nimlipe dokta nikienda sea cliff ndiko ntachukua kwenye fungu halafu yeye pesa yake atanipa account namba nimtumie nikamwambia sawa. mara dokta akapiga anasema vijana ndio wanatoka ofisini mda huo kwenda kununua package kwa ajili ya wateja wengine kama niko serious nitoe pesa ili na mm wafate hyo package nikamwambia muda huo nnadrive anipe nusu saa nimtumie akanipa namba za kutuma hzo pesa moja tigopesa nyingine mpesa .

  Nikaanza kuona biashara inaingia dosari ntafanya nao kazi ila sio hela yangu kufanya nao kazi nkafikiria kwanza nikapata maswali yasiyo na majibu 1. Hao wazungu wametoka ujerumani kwann waje kununua dawa za ujerumani Tanzania?,kama mhasibu na huyo Mrisho wanazonamba za Dokta kwann wasimfate wenyewe ili mgao uwe mkubwa kwao?,Na itakuwaje mtu unafahamiana nae kibiashara hamhaonana zaidi ya mwaka uje umuamini akuchukulie pesa nyingi kiasi hicho?kama inatakiwa deposit kwann isiwe ya package peke yake hadi iwe package na risiti ntalipiaje risiti kabla ya kupewa? nikaamua kuingia kwenye mtandao nikaandika jina la dawa ikaonyesha majibu mengi ila moja ni la alert ya wizi na namna hiyo nikawatumia sms wasijaribu tena kunitafuta.

  Tuweni makini jamani usikubali ofa hata kama ni kiasi kikubwa kutoka kwa usimjua inamaana yake kwake*
   
 2. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Wizi wa kizamani sana huo! Ungewakamatisha hao!
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pole kama umekwepa wizi huo mkuu!
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutujuza, but, hiyo style ya wizi imeripotiwa mno humu janvini.
   
 5. echuma

  echuma JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  me nilishazoea wa *tavuti huu wa rununu ilikuwa haijawahi kunitokea*
   
 6. echuma

  echuma JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ila namba zao ninazo nahisi hata namba huwa wanabadilisha au wanakuhack mwenye namba wanatumia kama wa tigopesa
   
 7. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Du!Umepona na mtego huo,mshukuru Mungu
   
 8. echuma

  echuma JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35

  Ndio kikubwa tu halafu siku ya kufa nyani miti huteleza
   
 9. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kwa hakika usemayo ni kweli!Hapa inaonekana ni jambo la kawaida kwa baadhi ya watu ila kuna watu huumia kwa mambo kama haya
   
 10. echuma

  echuma JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2012
  Joined: May 20, 2010
  Messages: 326
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mimi kawaida yangu ni kupata maelezo sana ili nikuelewe ila hawa hata sikuuliza sana,nimekubali wanatumia akili ila kuna sehemu ubunifu umepungua
   
 11. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Duh!nakumbuka ilikuwa mwezi wa tano dada mmoja pale iringa alipigwa kihivyohivyo,tena wale jamaa walijitambulisha kama wakenya.Huyu dada alitoa mkasa mzima kupitia Ebony Fm.
   
 12. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna jamaa alilizwa mil150 kwa staili hiyo
   
 13. CRISTA

  CRISTA Member

  #13
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 5, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 15
  Pole sana na yaliyokkuta laki sita mchezo
   
 14. k

  kpepeo New Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  du pole sana bwana
   
Loading...