Wizi mpya vituo vya mafuta

Wizi mpya vituo vya mafuta

Soso J

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2011
Posts
1,976
Reaction score
1,224
Haya wale wamiliki magari,mtindo mpya umeibuka!Wakati wewe ukiamini mafuta yanawekwa kwa tanki la Gari,kumbe muweka mafuta anakuziba ili usione dumu dogo ili aweze kuwa anakuibia jionee kwa picha

f9eb66a0-be3c-4ed9-8b9a-dffaa92bc9dc.jpg
 
Hapana kwakweli umakini uongezeke wale wenye magari maana mbinu hii kiboko
 
Yan unakaa mjini unaibiwa kizembe ivyo

Hayo ndio madhara ya kutojua matumizi ya side mirror
Mkuu una miliki Gari tuanzie hapo, na ulishaenda kuweka mafuta mara ngapi, na sight mirror kazi gani, au hilo Gari umenunuliwa na Shemeji au mumeo kwa hiyo huna haja ya kufuata matumizi sahihi yaliyopo kwenye vifaa vya gari. Kama umemiliki gari au ni Dereva WA muda huwezi kuibiwa kishamba namna hii. Cha kwanza utaangalia kwenye mashine kama kaandika kiasi sahihi ulichosema then utaangalia kupitia sight mirror kinachoendelea. Hakuna mtu mjinga WA kuibiwa namna hii.
 
Mhhh angalia vizuri lakini aliyeshika pampu anakuwa amekuziba/amekupa mgongo sasa side mirror haina kazi labda ushuke tu ndio dawa
Ina mana dashboard ya gari haina mshale Wa kuonyesha kiasi cha mafuta kilichoingia na wewe ukalinganisha na ela iliotoa kulingana na bei ya mafuta kwa lita?
 
Huwezi kuibiwa kizembe namna huyo utakuwa bogus namba moja kwenye Nchi ya Shit hole, au labda uwe umepewa gari na Shemeji yako na haujui uchungu wowote kuanzia mafuta mpaka gari lenyewe
 
Angalia picha kwanza utaelewa!!mwenye gari ameaminishwa kuwa mafuta yanawekwa kwa gari lakini ukweli ni kuwa aliyeshika pampu anaweza kwenye dumu ndio kumeibia kunapokuja

Mafuta zaidi ya 20000 nikiweka huwa nashuka na kuzunguka kabisa kwa mpimaji.

Vituo vya Kampuni ya "JUMLA" ukiweka mafuta hutajuta iwe Dodoma au Bagamoyo kwanza mita inaenda polepole haina haraka. Ukiwasha gari tu, mshale huo umepanda na unaridhika.

Hata wale wa Kampuni ya "DUMA wa Marekani ya Kusini" sio wabaya kampuni ya "Uingereza Kuu na Poland" nao wazuri wako wengi pia wazuri ila hao wako juu.
 
Kwa mazingira hayo ni lazima hiyo ni petrol station za njiani siyo za mjini mjini watu wengi akifanya hivyo lazima aumbuke na wewe mwenye gari unajikuta boss kiasi gani hutaki kushuka kwenye gari kuangalia kinacho endelea huu utakua undezi wa kupitiliza
 
Angalia picha kwanza utaelewa!!mwenye gari ameaminishwa kuwa mafuta yanawekwa kwa gari lakini ukweli ni kuwa aliyeshika pampu anaweza kwenye dumu ndio kumeibia kunapokuja

Noma saaana
 
Mkuu una miliki Gari tuanzie hapo, na ulishaenda kuweka mafuta mara ngapi, na sight mirror kazi gani, au hilo Gari umenunuliwa na Shemeji au mumeo kwa hiyo huna haja ya kufuata matumizi sahihi yaliyopo kwenye vifaa vya gari. Kama umemiliki gari au ni Dereva WA muda huwezi kuibiwa kishamba namna hii. Cha kwanza utaangalia kwenye mashine kama kaandika kiasi sahihi ulichosema then utaangalia kupitia sight mirror kinachoendelea. Hakuna mtu mjinga WA kuibiwa namna hii.
Mkuu mimi namiliki gari ndio tena gar langu la kwanza nilimiliki nikiwa na miaka25 tena kwa ela yangu hua nikienda sheli hua nafungua mfuniko wa tank na siangaiki na mhudu mimi nacheza na dashboard tu maana najua kama mafuta lita 1 ni bei hii mshale utafika hapa

Usipo fika hapatatosha kwakweli

Sasa nyie endeleen kuibiwa kishamba!
 
Back
Top Bottom