Wizi mpya umeibuka...kaa chonjo

Wizi mpya umeibuka...kaa chonjo

Majuzi tulijadili kuhusu mtunzi wa riwaya wa kimataifa unayemkubali. Hapo ndio namkubali marehemu Sydney Sheldon. Kama umesoma novel yake ya "IF TOMMOROW COMES"huwezi ukatapeliwa kwa mtindo huo. Kitabu hicho japo ni cha miaka ya tisini au kabla kina mifano kadhaa kama hiyo. Ili usitapeliwe inabidi usiwe na tamaa. Kazi ya tapeli ni kukutia tamaa. Ukiishinda tamaa umemshinda tapeli. Soma riwaya hiyo upate maarifa ya kushindana na matapeli wa aina hiyo.
 
Mim nawashangaa mnaomsema eti kuwa ametunga haijamtokea bali amekopi story ya miaka ya nyuma, mimi sioni ana sababu gani ya kufanya hivyo na pia sioni nyie mna sababu gani ya kutomuamini............anapata faida gani akiwadanganya? Mimi nadhani ni kweli imemtokea....Shaycas, kuhusu vyombo vya dola kutoa taarifa ya utapeli huu mmh nina imani wanajua na wala sijawahi kusikia wakitangaza, sitashangaa kuwa na wao (vyombo vya dola) wanashirikiana nao....... THIS IS BONGO BAAANA
 
Ndugu wapendwa, Story ifuatayo ni ya kweli. Najua kwa kiasi fulani itakuwa inaninizalilisha kwa kutokuwa makini lakini naona ni vyema niwashirikishe rafiki zangu ili msije mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa kama vile ndugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza kutuelezea yaliyomsibu ndugu yake labda na mimi ningeweza kuepuka utapeli huu. Kinchosikitisha matapeli wenyewe ni watu wanaotufahamu vizuri. Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo likizo) nikapokea simu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye alijitambulisha ananifahamu, na kwa jinsi alivyonitaja kwa jina na career background details zangu sikuwa na shaka kwamba hanifahamu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo: TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.Mimi: Nzuri Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?Mimi: Hapana, nani mwenzangu?Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na uliwahi kunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World food programme, Kigoma kama Chief supplies officer.Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba sikumkumbuka ila kwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali, siku jiuliza sana , after all alikuwa hajasema anachotaka) Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kama unavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna maghala makubwa ya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha vyakula haviharibiki huwa tuna weka presavative inayoitwa Damoline Liquid solution made in Sweeden, hii inapatikana MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises. Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplier aliyeshinda tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayo madawa akanidhulumu na kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10% angeniripoti kwa mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya bali kusubiri contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasa ndio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii kazi utaweza kuifanya ukizingatia unalipwa cash on delivery! NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi hivyo sikuwa na doubt yeyote, bali nikaona hii is just another deal kama ambazo nimeshawahi kufanya successfully. Mimi: Okay sasa unataka nifanye je? Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr. Shija, huyu ndiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier wetu wa zamani aliye ni dhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa kazi tena, wewe uende ujifanye unaulizia hiyo liquid solution, na u negotiate ujue atakuuzia shillingi ngapi. Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupe quotation, alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya. Basi wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitate kuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na strangers na akataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa kuwa siwezi kumwambia ukweli kuhusu aliyenipa namba yake, ikabidi na mimi niwe muongo kwa muda, nika pretend kuwa mimi ni mkulima na nahitaji hiyo presavative kwa ajili ya maghala yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani na kukiri kuwa anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair ya chupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa angalia nilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni kaomba punguzo na akasema atauza kwa 1million. Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya kupata bei nimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata ni kuwa mimi nitauza kwa USD. 1700, na tofauti kwa maana ya faida tutagawana, hivyo nisubiri aniunganishe kwa bosi wake for further final details. Basi wandugu kama mnavyonijua katika issue za fwedha, nikachukua calculator ya simu ili nijue deal ina shillingi ngapi, hela zilivyokuwa nyingi hata calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50 pairs @ usd 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kama usd 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFU tunagawana pasu pasu. Guys you can imagine what was going on in my head! Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake ambaye ni mzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo: MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new supplier?MIMI: YESMZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid solution; we are looking for 50 pairs?MIMI: Yes I have sufficeint stockMzungu: what is your price per pair?Mimi:$1700Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to be paid in dollars or TZSMIMI: Dollar of course, you how how unstable the local currency is ( Hapo tena na mimi nataka kuonyesha kuwa ni International businessman)Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be paid cash or by cheque?Mimi:CashMzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new supplier we need this liquid urgently possibly today, and since you have said you have enough stock we are taking off this morning from Kigoma coming to Dar, please arrange for the transport to take us to Movenpick, we will pay usd. 200 for your fuel, but most importantly make sure you bring one pair of the sample with you. Mimi: No problem at all I have been in this business for quite sometime now you can be sure everthing will be fine. Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque book, nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample yakwenda kuwaonyesha wateja wangu. Baada ya kutoka bank nikampigia dr. shija ili aniuzie hiyo sample, akasema kwa sasa ametoka ofisini ila sample anazo katika gari na alikuwa anaelekea Mwananyamala hosp, then Magomeni alafu Muhimbili, hivyo tukutane Magomeni hosp. Yaani jinsi nilivykuwa naendesha gari basi hata kama ni mashindano ningeweza kushinda, basi mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija. Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi wake asingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo fedha na yeye anipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana akaja akaingia kwenye gari nikamwambie anipe hizo sample kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFP wanavyotaka! NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION. Bila hata aibu yule kijana akaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa itakamilishwa saa nane. Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri, nikampigia dreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza bei kutoka airport mpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000 nikamwambia usijali ntakupa 50,000/=!!!!!!!!!!!!! (Kumbuka mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri). Basi mimi mbio nikaenda airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ili tumalize biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakuna kitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi tena nikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride nikamsimulia jamaa mmoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza akasema hata ndugu yake ametapeliwa wiki iliyopita, nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yake alipigwa 3.5m last week. Taarifa nilizonazo mpaka nikuwa hii ni network ya wahaya na mpaka sasa ni wahaya wengi wameishaibiwa ukilinganisha na makabila mengine. So guys thats my story
Dah dah dah! Pole sana mie niliokolewa na michuzi blog hbr hii inaandikwa sana kule michuzi blog!Walinipigia, wacha niwasanifu namba zao zoye wanazotumia ninazo bahati mbaya tu sikupata ushirikiano wa polisi kuwanasa!But tumeapa wakiingia line kwa mtu wa krb yangu awatege tuwakone tubonde wenywe kipigo cha mbwa mwizi!Na kweli cku si siku akapigiwa rafiki yangu wakaribu, amekwenda nao kila akiwambia waje town hawataki wanadai mshikaji aende sinza, tukaachana naoBut pole sana ndugu
 
Kaka nilivyoanza kusoma story yako mwanzoni tu,nkajua nini kingefuatia,biashara kubwa km hyo lazma ingekuwa na restriction za hapa na pale,ww hukuingiwa na wasi wasi??
All in all pole sana!!
 
Hata kama ni "copy and paste" ni habari nzuri, tuendelee kuhabarishana.
 
watu wana akili! Dah, hapa naona wamekuonea huruma, 1m ni kidogo mno, kwa jinsi ulivyokuwa na wenge la utajiri hata kama ungeambiwa 10m ungeona cha mtoto. Pole sana.
 
teheeeeeeee, teheeeeeeee
,..wat kind of personification is this?
 
Pole sana ndugu ndio nchi yenyewe pesa inatafutwa kwa kila njia. Tuwe waangalifu.
 
Pole mkuu, mimi pia ilisha nitokea mara mbili, mwaka juzi mara moja bahati nilikua nimesha tumiwa e-mail na one of my friends.
Tapeli alivonipigia cm exactly aliongea kama ile e-mail ilivyohadithia kwa hiyo nilimwambia tapeli huyo anipe muda nimalize kazi then tutaongea, nikiwa natafuta njia ya kumkamata, but badae nikaaachana nae na alinisumbua sana kwa sim sikupoke.

Last month tena nimepigiwa sim nikatajwa jina na ubini pia, tapeli huyo akaongea maneno hayo hayo, na sikuzote huwa wanadai wanafanya kazi WFP, then nikamwambia mimi pia niko WFP mbona sikufaham na hakuna biashara kama hiyo? akadai ooh mi niko UN kigoma.
Nikamgombeza sana nikamwambia ukiendelea utaishia kufungwa utapeli wako hautakusaidia, akaniambia kwahiyo umekataa business nikamjibu ndiyo nimekataa na ukiendelea ntakufunga.

Nimegundua hawa watu wanapata contact kwenye bsns card za watu na ndo wanazozitumia bila hata kujali na ndio maana hua wanaanza kwakusema bado uko office flani.
TNikweli tunatakiwa kulijua hili kwani lipo.
 
Ndugu wapendwa,

Story ifuatayo ni ya kweli. Najua kwa kiasi fulani itakuwa inaninizalilisha kwa kutokuwa makini lakini naona ni vyema niwashirikishe rafiki zangu ili msije mkatapeliwa kama mimi na wengine wengi wameshatapeliwa kama vile ndugu yake Galeba, laiti Galeba angeweza kutuelezea yaliyomsibu ndugu yake labda na mimi ningeweza kuepuka utapeli huu. Kinchosikitisha matapeli wenyewe ni watu wanaotufahamu vizuri.

Mnamo muda wa saa tano asubuhi nikiwa nyumbani (nipo likizo) nikapokea simu nisiyoifahamu kutoka kwa mtu ambaye alijitambulisha ananifahamu, na kwa jinsi alivyonitaja kwa jina na career background details zangu sikuwa na shaka kwamba hanifahamu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

TAPELI: Mr. Alex Matovu habari za siku nyingi.
Mimi: Nzuri
Tapeli: Vipi bado unafanya kazi Blue Financial Services?
Mimi: Hapana, nani mwenzangu?
Tapeli: John, nilikuwa nafanya kazi Wizara ya elimu, na uliwahi kunisaidia nikapata mkopo, ila kwa sasa nipo World food programme, Kigoma kama Chief supplies officer.
Mimi: okay sasa nikusaidie nini John (ukweli nikwamba sikumkumbuka ila kwa kuwa tulikuwa tunatoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali, siku jiuliza sana , after all alikuwa hajasema anachotaka)

Tapeli: Sasa nina issue naomba unisikilize kwa makini, kama unavyofahamu WFP tunatoamisaada ya vyakula hivyo tuna maghala makubwa ya kuhifaadhi chakula, hivyo ili kuhakikisha vyakula haviharibiki huwa tuna weka presavative inayoitwa Damoline Liquid solution made in Sweeden, hii inapatikana MSD na kwa licensed dealers kama Mohamedi Enterprises. Kwahiyo tuli float tender mwaka jana na supplier aliyeshinda tulikubaliana anipe 10% lakini baada ya ku supply hayo madawa akanidhulumu na kunitisha kuwa iwapo nitamdai hiyo 10% angeniripoti kwa mabosi wangu. Kwa hiyo sikuwa na cha kumfanya bali kusubiri contract yake iishe alafu nimtafute supplier mwingine. Sasa ndio nikaona nikupigie ndugu yangu maana nakujua wewe hii kazi utaweza kuifanya ukizingatia unalipwa cash on delivery!

NOTE: nimeshawahi ku deal na supplies officer wengi hivyo sikuwa na doubt yeyote, bali nikaona hii is just another deal kama ambazo nimeshawahi kufanya successfully.

Mimi: Okay sasa unataka nifanye je?

Tapeli: Unachotakiwa kufanya ni kwenda MSD umuone Dr. Shija, huyu ndiye mkuu wa hapo na ndiye aliyekuwa supplier wetu wa zamani aliye ni dhulumu, sasa kwa kuwa sitaki kumpa kazi tena, wewe uende ujifanye unaulizia hiyo liquid solution, na u negotiate ujue atakuuzia shillingi ngapi. Kwahiyo nakutumia simu yake mpigie muongee akupe quotation, alafu akisha kupa bei nipigie ili nikuelekeze cha kufanya.

Basi wandugu nikampigia dr. shija, mwanzoni shija ana hesitate kuzungumza na mimi aki pretend kuwa hapendi kuongea na strangers na akataka kujua namba yake nimeipataje, sasa kwa kuwa siwezi kumwambia ukweli kuhusu aliyenipa namba yake, ikabidi na mimi niwe muongo kwa muda, nika pretend kuwa mimi ni mkulima na nahitaji hiyo presavative kwa ajili ya maghala yangu yaliyopo arusha. Basi akawa na imani na kukiri kuwa anayo stock yakutosha, na hiyo liquid inauzwa kwa pair ya chupa mbili zenye ujazo wa 1000mls, kila pair ni 1.2m. Sasa angalia nilivyoingia katika mtego, baada ya kunipa bei ni kaomba punguzo na akasema atauza kwa 1million.

Nikafanya kama nilivyoelekezwa na John wa WFP kuwa baada ya kupata bei nimjulishe nilivyomjulisha akasema kinachofuata ni kuwa mimi nitauza kwa USD. 1700, na tofauti kwa maana ya faida tutagawana, hivyo nisubiri aniunganishe kwa bosi wake for further final details.

Basi wandugu kama mnavyonijua katika issue za fwedha, nikachukua calculator ya simu ili nijue deal ina shillingi ngapi, hela zilivyokuwa nyingi hata calculator iligoma, maana WFP wanahitaji 50 pairs @ usd 1700, mimi nanunua kila pair kwa 1million ambayo ni kama usd 770 hivyo difference usd 930 x 50 pairs = USD 46500, ALAFU tunagawana pasu pasu. Guys you can imagine what was going on in my head!

Basi kweli muda si mrefu nikapigiwa simu na huyo bosi wake ambaye ni mzungu na mazungumzo yalikua kama ifuatavyo:

MZUNGU: This is Mr. Scheinder from WFP, are you the new supplier?
MIMI: YES
MZUNGU: Do you have enough stock of Damoline Liquid solution; we are looking for 50 pairs?
MIMI: Yes I have sufficeint stock
Mzungu: what is your price per pair?
Mimi:$1700
Mzungu: ahaaaaaaaa thats a very good price, do you want to be paid in dollars or TZS
MIMI: Dollar of course, you how how unstable the local currency is ( Hapo tena na mimi nataka kuonyesha kuwa ni International businessman)
Mzungu: No problem, we have enough dollars, you want to be paid cash or by cheque?
Mimi:Cash
Mzungu: Okay no problem, now listen very carefully mr. new supplier we need this liquid urgently possibly today, and since you have said you have enough
stock we are taking off this morning from Kigoma coming to Dar, please arrange for the transport to take us to Movenpick, we will pay usd. 200 for your fuel, but most importantly make sure you bring one pair of the sample with you.
Mimi: No problem at all I have been in this business for quite sometime now you can be sure everthing will be fine.

Masikini bila kujua nimeingizwa kingi, nikachukua cheque book, nikaandika cash withdraw 1million ili nikanunue sample yakwenda kuwaonyesha wateja wangu. Baada ya kutoka bank nikampigia dr. shija ili aniuzie hiyo sample, akasema kwa sasa ametoka ofisini ila sample anazo katika gari na alikuwa anaelekea Mwananyamala hosp, then Magomeni alafu Muhimbili, hivyo tukutane Magomeni hosp. Yaani jinsi nilivykuwa naendesha gari basi hata kama ni mashindano ningeweza kushinda, basi mimi mbio mpaka magomeni hosp namsubiri dr. shija. Nikampigia akasema yupo ndani hospitalini na yupo na mabosi wake asingeweza kutoka ila anamtuma kijana wake nimpe hizo fedha na yeye anipe hizo dawa, kweli ikawa hivyo kijana akaja akaingia kwenye gari nikamwambie anipe hizo sample kwanza nikazisoma ziko exactly kama WFP wanavyotaka! NIKAKABIDHI HELA 1 MILLION. Bila hata aibu yule kijana akaniomba 50,000/= nikamwambie asijali maana deal kubwa itakamilishwa saa nane.

Kwa kuwa wageni wangu walishaniambia niwaaandalie usafiri, nikampigia dreva tax wangu aje airport saa nane, nikamuuliza bei kutoka airport mpaka movenpick ni ngapi akasema 25,000 nikamwambia usijali ntakupa 50,000/=!!!!!!!!!!!!! (Kumbuka mimi ntalipwa usd 200 ya usafiri).

Basi mimi mbio nikaenda airport terminal one kusubiri ndege ya WFP ili tumalize biashara, nilipofika kuulizia reception nikaambiwa hakuna kitu cha namna hiyo na mimi ni mtu wa 10 kutapeliwa, basi tena nikajirudia kimya kimya. Nikaenda kula chefs pride nikamsimulia jamaa mmoja yaliyonisibu, kabla sijamaliza akasema hata ndugu yake ametapeliwa wiki iliyopita, nikampigia Galeba akasema yeye jamaa yake alipigwa 3.5m last week.

Taarifa nilizonazo mpaka nikuwa hii ni network ya wahaya na mpaka sasa ni wahaya wengi wameishaibiwa ukilinganisha na makabila mengine.

So guys thats my story
utapeli wa kizamani sana mkuuu zamaani sana mkuu
 
Pole sana, kila siku kuna mbinu mpya ya kufanya mkono uende kinywani hata kama ni haramu.
 
Pole sana ndugu yangu,
Huu utapeli haujitokezi sasa kwa mara ya kwanza. Ninachokuomba ni kuwa unaweza kufuatilia kupitia polisi, Makampuni ya simu na TCRA ili upate hela zako. Unless hizo namba hazijasajiliwa na TCRA wamefanya utapeli wa kutuambia tusajili huku wakijua kuwa hawakuwa makini na zoezi lao lakini wanawajibika 100% kujua wenye namba na mahali walipo.

Aidha napenda kutahadharisha watanzania wenzangu kuwa macho na fedha za chapchap. Ukitaka utajiri wa chapchap unaweza kuambulia hasara ya chapchap!
 
Kuna ndugu yangu mmoja bado kidogo alizwe kilichomsaidia baada ya kupata iyo dil aliwashirikisha jamaa zake wakamtonya kwamba hao ni matapel
 
umeniacha hoi pale ulipochukua calculator ya sim, dar zero zero zikazid mpaka ikagoma, kwel imani huja kwa kusikia, unapompa m2 chans ya kumsikiliza wakat humjui hapo ndo shda inapoanza
 
Duh ,pole sana mkuu
nina imani hata mimi ningeweza kuingia.
Ninashukuru kwa taarifa
 
Tunashukuru sana kwa kutuzindua! Vile vile kuna matapeli wanaotuma emails kutapeli watu. Watakuambia umeshinda bahati nasibu au kuna kibunda cha urithi cha kugawana n.k. Tusitake utajiri wa bila jasho una cost yake!
 
Back
Top Bottom