CAMARADERIE
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 4,419
- 1,929
Gamba JipyaHizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
Mwenzetu ana Multiple ID anajua anachozungumza!Mkuu ulikuwepo enzi za nyenzi.com, jamboforums.com jee?..au umeibukia jamiiforums?..
Kalaga baho
Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
Sijui tufanyeje na hawa wezi!
Gamba Jipya,
Labda bado hujasoma Taarifa ya CAG. Siyo hiyo tu ya Stimulus package tu. Fedha za zilizokuwa zinahojiwa ni zile tu zilizotoka kwenye Own Source, ambazo CAG ameshindwa kuziona zilienda wapi, na Serikali haikutoa ushirikiano kwa kumpa Listi ya Makampuni au atu waliopewa fedha hizo. Kumbuka Stimulus package ilitangazwa na JK siku mbili tu kabla ya Mkutano wa Bunge wa Bajet, na Serikali tulipoishaiuri utaratibi Transparent kama zilivyofanya nchi zingine ambazo tuliwapa mifano hai walikataa katakata. Hivyo fedha zote zinazohojiwa hapa ni zote 1.7 trillioni ambazo tunadai Serikali itoe listi yote ya waliopewa Fedha hizo.
Katika Ukurasa wa 127 wa Ripoti ...kwa mwaka unaoishia 30 June,2010 (Hesabu Serikali Kuu) CAG anahoji pia 70 Billioni zilizopelekwa TIB kwa ajili ya Kubadilisha TIB kutoka Taasisi ya Fedha na kuwa Benki inayoshughulikia Kilimo. Hadi anawasilisha Taarifa yake Bungeni, March 2011, CAG ameshindwa kuona fedha hizo i) Ziko Akaunti gani ndani ya TIB? ii) Hajaonyeshwa dondoo za ripoti ya fedha kuonyesha mapokezi na urari wa mfuko huo iii) Mkataba na TIB kuonyesha makubaliano ya jinsi fedha hizo zinavyotakiwa kutumika iv) Kibali cha Baraza la Mawaziri kuonzisha Benki hiyo ya Wakulima. Isitoshe inadhaniwa kuwa 70 Billioni yote au sehemu yake kubwa inatokana na Fedha zilizokuwa zikirejeshwa kutokana na EPA. Hii ni hali ya hatari sana. Tena 2010 ilikuwa mwaka wa uchaguzi. Kuna maswali mengi ya kujiuliza.
Unauhusiano na Chama cha Gamba nini? Umetumwa kuja kuvuruga? Umejiunga juzi tu (16th April, 2011), umezisoma lini hizi taarifa? Gamba lako jipya halibadili mawazo na sumu yako. Tumekushitukia.
Dawa ni CAG kupewa meno ya kuwashtaki na kuwa-prosecute mahakamani wote anao wakuta katika ukaguzi wake kwamba wametuibia fedha.Kuendelea kutoa taarifa tu mwaka hadi mwaka bila kushtaki haina maana, na ndio maana wizi unaendelea kama kazi.
Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
RIPOTI YA MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI MWAKA ULIOISHIA TAREHE 30 JUNI, 2010 inasema
5.9 Kukosekana kwa orodha ya waliolipwa kiasi cha Sh.48,000,270,000 kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa uchumi
Serikali ililipa kiasi cha Sh. 48,000,270,000 katika Benki Kuu ya Tanzania kama sehemu ya mchango wake wa kuchochea ukuaji wa uchumi ili kukabiliana na msukosuko wa uchumi ulioikumba dunia. Hata hivyo, hatukupatiwa orodha ya walionufaika na fedha hizo za kufidia hasara na kulipia mikopo wala utaratibu utakaotumika kwa wafanyabiashara husika kurejesha fedha hizo pindi hali ya uchumi itakapoimarika. Kwa hali hiyo, nimeshindwa kujiridhisha kuhusu uhalali wa malipo hayo na urejeshwaji wake
utakavyokuwa. CAG L.S Utouh
Hii si EPA ya pili?
Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
Tukumbushe ufumbuzi wake ulikuwaje; ikiwezekana tutajie hayo makampuni yaliyolipwa fedha hizo.Hizi ni habari za zamani sana mkuu na tumekwisha zizungumzia na kupata ufumbuzi wake kutoka sehemu husika, leta hoja mpya na zenye mashiko achana na zilipendwa, nchi hii inahitaji mchango wako.
Huyu nadhani ni MSGamba Jipya
Join Date : 16th April 2011
Posts : 31
Thanks:
0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power : 0
Wewe ni gamba jipya au EPA mpya, na hii habari uliizungumzia wapi na kupata ufumbauzi sababu hapa umejiunga juzi tu. Tuambie Jukwaa uliloizungumzia na ufumbuzi wake.