Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 49,264
- 19,595
Polisi waua majambazi 6 -MOROGORO
Eline Shaidi, Morogoro
Daily News; Sunday,July 20, 2008 @00:01
Polisi wamewaua watu sita wanaotuhumiwa kuwa majambazi waliovunja na kuingia kwenye chumba cha kuhifadhi fedha cha Benki ya National Microfinance (NMB) tawi la Kilombero, usiku wa kuamkia jana.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Thobias Andengenye alisema majambazi hao wakiwa na shotgun na bastola, waliingia kwenye chumba hicho baada ya kuvunja milango kwa kutumia gesi. Andengenye alisema majambazi hao waliuawa kabla hawajafanikiwa kuchukua fedha zo zote kutoka kwenye chumba hicho.
Polisi walipata taarifa kutoka kwa wasamaria juu ya mpango wa uporaji na hivyo askari walipangwa ndani ya benki mapema, huku wengine wakiwa wamezunguka nje, alisema. Aliongeza kuwa majambazi waliingia ndani ya benki kwa kutumia mlango wa nyuma hadi kwenye chumba cha kuhifadhi fedha baada ya kuyeyusha mlango.
Kamanda alisema baada ya polisi kuona majambazi wameingia kwenye chumba hicho ndipo walipofyatua risasi moja hewani kuwataka wajisalimishe, lakini wakakiuka na kuanza kurushiana nao risasi. Alisema majambazi walifyatua risasi nne na polisi walijibu na kisha kuwajeruhi.
Walikufa kabla ya kufikishwa hospitali kwa matibabu. Baada ya kufanyiwa upekuzi, watu hao walikutwa na risasi 10 za shotgun, mitarimbo miwili, mitungi mitatu ya gesi, bisi bisi, visu, hirizi, funguo na karatasi yenye maelekezo yanayoaminika kutoka kwa mganga wa kienyeji, alisema.
Vingine walivyokutwa navyo ni karatasi mbalimbali za kesi katika vituo tofauti vya polisi (RB), mkasi wa kukatia nondo, namba ya gari T 145 AVK, vitambulisho vya benki ya CRDB, mifuko ya kuhifadhi fedha na turubai linaloaminika walilitumia kukingia mwanga wakati wakitumia gesi ili mwanga usionekane.
Kamanda huyo alisema watuhumiwa hao vile vile walikutwa na magari mawili ambayo ni Toyota Hilux Pick-up lenye namba za usajili STJ 6154 lililokuwa likiendeshwa na Mwichande Mwinkindo (41) mkazi wa Kimara B Dar es Salaam na Toyota Corolla T 149 ATL mali ya Husna Hussein lililokuwa likiendeshwa na Msafiri Chitawa (37), mkazi wa Tabata Changombe Dar es Salaam.
Madereva wote wawili wamekamatwa na jambazi mmoja aliyekuwa nje anatafutwa. Akizungumzia tukio hilo Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema; Hii ndiyo njia sahihi ya kukabiliana na uhalifu. Alisema kwa kiasi kikubwa polisi wamefanikiwa