Wizi m2pu vyuo vikuu nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizi m2pu vyuo vikuu nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by saikon nokoren, Sep 5, 2009.

 1. s

  saikon nokoren Member

  #1
  Sep 5, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello jamiiforum!

  Sijui ni uwelewa wangu mdogo au kuna wizi unaoendelea katika Vyuo vikuu nchini, yaani hii ni too much primitive accumulation,"WIZI MTUPU". Ni jambo la kushangaa ambalo alingii akilini, Mtanisamehe kama nimepotoka,Wanafunzi walio hitimu masomo mwaka huu(kidato cha sita) na wengine waliohitimu miaka ya nyuma, walio omba kujiunga na Vyuo Vikuu kwa mwaka wa Masomo 2009/2010,Wengi wao wamekosa nafasi,cha kushangaza ni kwamba vyuo vyenu wametanga tena Wanafunzi kuomba kujiunga na Vyuo kwa Second admission,kwa wanafunzi waliomba awamu ya kwanza na kukosa kuandika barua kuomba tena na wambao hawakuomba kuomba kujiunga na Vyuo kwa kujaza fomu ya maombi, take note kwamba fomu ya maombi ni Tsh kuanzia 15,000,20,000,25,000 kulingana na chuo husika.SWALI la kujiuliza iweje walio omba awamu ya kwanza wamekosa,huku wakiwa na daraja la kwanza ,pili hadi tatu hawakujaguliwa,Je watakao omba awamu ya pili mtindo si sawa na wale wa kwanza kukosa?Na kwanini uombe kwa kuandika barua wakati ulishaomba, fomu yako pending kwao?Kwanini Vyuo wasiwachague kwanza wale wote waliokosa awamu ya kwanza ndipo watangaze nafasi ya kujiunga kwa awamu ya pili kama nafasi zipo?Nahizi Vyuo Vikuu wanafanya WIZI MTUPU wa Tsh 15,000,25.000,20,000.Je mtindo huu tutafika?
  NAWASILISHA KWANU JAMIIFORUM TUJADILI.
   
 2. D

  Dingiswayo Member

  #2
  Sep 5, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 15
  Mkuu kinachotangazwa sasa ni kwa ajili ya private sponsorship na ile ya kwanza watu waliomba ili wapate ufadhili toka bodi ya mikopo...sasa hawawezi kuanza kuchagua kutokana na maombi yale yaliyopita kwa kuwa unaweza kuwa huna uwezo wa kujilipia as private student ndo mana wanasema..kwa ambaye tayari aliomba na kulipia form kabla basi aandike tu barua kuomba apatiwe nafasi as private candidate..ila ambaye hakuomba kabisa ndo anatakiwa aanze mchakato upya wa form, malipo na vitu vingine.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jibu zuri na linajitosheleza, asante
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  umesomeka vilivyo ....huo ndio ukweli wa mambo.Mwandishi acha jazba.
  ila kuna hili la reserve list mi linanipa tabu sana,nasikia hiyo list inawekwa makusudi kwa ajili ya kujipatia ulaji wao.Ni mtego tu ili mzazi au mlezi aanze kuhangaika kufuatilia ambapo mwisho wa siku atajikuta anajiingiza kwenye utoaji rushwa ili mwanae asome.Hili linanikera kwelikweli....
   
Loading...