Abbassalum
JF-Expert Member
- Dec 11, 2016
- 338
- 176
Wakuu nimeona ili nije kulisema humu uko kwenye magroup ya whatsapp kuna group moja linaitwa TV kiganjani, ili group ni la matapeli kwa sababu gani nasema ivyo wale wahusika wakuu yaani waanzilishi wa ili group wanawashawishi watu wageni mule kuwa wana link ya kuunganisha kwenye simu yako unatakiwa ulipe shilingi 3000/= wakuunganishe kwenye chanel za kuona burudani ikiwemo dstv azam one azam two star tv itv na station nyingi mpaka za nje NK. Za kuona mipila mikubwa kama uefa ligi za ulaya, ukilipia iyo 3000/= ndio wanakutumia iyo link yao wanakuelekeza maelezo gusa maandishi ya blue u douwload zitakuja TV za bure, mimi machale yakanicheza nikawaambia mie siwafanyii uhuni nirushieni iyo link iwapo kama nimepata izo channel, mnazosema nitawarushia 3000/= yenu wakawa wanagoma na kukataa na kusita kunirushia, nikatumia mbinu za kutosha, na kuwabembeleza ndio wakakubali, kunirushia iyo link, cha ajabu kila nikiifungua inakataa, sasa nikajua labda ni kwangu ndio imekataa, nikaingia kwenye lile group watu kibao wanalalamika na wao kwao imegoma kufunguka kwenye simu zao, na mbaya zaidi wapo wenzao wanaochombeza, kuwa wao wanaona na washaunganishiwa safiii kabisa lkn lao ni moja namba yake uyo bwana anaetapeli ya simu pia ninayo na kama kulizwa watu kibao inaonekana washalizwa, nikaona mimi huu uzi niulete uku jf ndugu zanguni muujue na kuuelewa wakuu...!!!!