rmashauri
JF-Expert Member
- Jan 29, 2009
- 3,011
- 454
hahahaaaa basi safi,tukikutana tena, unitambulishe mkuu
Mkuu hebu niambie ni Benki gani nzuri katika hao washirika wa Umoja Switch? Hizi zingine naona sasa zinatishia usalama wa pesa zetu
hahahaaaa basi safi,tukikutana tena, unitambulishe mkuu
Mkuu hebu niambie ni Benki gani nzuri katika hao washirika wa Umoja Switch? Hizi zingine naona sasa zinatishia uasalama wa pesa zetu
Wandugu wanajamvi. Siku za karibuni kumekuwepo wizi wa kutisha kwenye mabenki kutumia mitandao. Lakini inaonekana benki zetu hawajachukua tahadhari ya kutosha na bado haijulikani liability inakuwa ya nani endapo wizi unatokea.Mwezi Mei 2012 rafiki yangu aligundua ameibiwa kiasi cha mil2 kupitia kwenye Master card. Yeye aliripoti haraka sana, akapeleka vielelezo vyote kule makao makuu ya NBC. Iligundulika kuwa maeneo walikochoka hela ni kule Mlimani city pamoja na kwenye ATM za exim.Hata hivyo waliahidi kumpa majibu sahihi baada ya siku 45! (just imagine kama ndo ilikuwa akiba yako unasubiri muda wote huu). Juzi kati benki wamempigia simu na kumwambia inaelekea hela alizichukua mwenyewe (hawakutoa cctv evidence ju-justify conclusion yao). Sasa ndugu anahaha na mwezi huu ni mwezi wa kuwarudisha watoto shule, lazima kulipia ada. Mbaya zaidi rafiki yangu amechanganyikiwa in terms of what next. Je sheria za kifedha zinamlinda vipi mtenja wa benki endapo tukio kama hili likitokea? Pili huyo rafiki anafikiria kuwachukulia hatua za kisheria....je kuna mtu anaweza kutoa mwongozo (sio wa spika bali wa kisheria) ni jinsi gani rafiki yangu anaweza kupata haki yake?
Kwa maoni yangu:
Inaelekea benki zetu nyingi zimeshindwa kuthibiti wizi huu, lakini kuna uwezekano kabisa wafanyakazi wa benki ama wale wanaohusika na ATM wakawa sio waaminifu wanachukua namba za siri na kuwaliza wateja. This is not acceptaable and should be dealt by all means
Mkuu asante. Nadhani suala la kutumia media linaweza kuwa zuri, kwa kuwa image yao itagundulika kirahisi. Kwa sasa nadhani wanawadharau wateja wao
[/QUOTE]Samahani nilikwenda mashambani tangu nimetuma thread jana. Lakni ndo nimerudi sasa. Nilitaka kusema kuwa mhusika ameprint hivyo vyote, yeye amekuwa makini kwa kuwa kila mara anapodraw hela kwenye ATM anachukua na kutunza slip zile. Sasa alipokwenda NBC aliawapatia nakala za zile slip ambazo zilifuatiwa na wizi, akaambatanisha na barua ya malalamiko. Jambo la kushangaza ni kwamba NBC walipompigia simu kumweleza kuwa hawatampa, alikwenda ofisini kwao tena, Mshituko ukawa kuwa kwenye barua yake ya malalamiko hakuna zile attachments...haijulikani ni nani amezichukua!
Otherwise unalosema ni kweli ni vema kuweka hela nyumbani vijisenti vyako kuliko kuhangaika na vibenki uchwala. Changamoto ni watoto wa kova, wakizinusa nyumbani kwako umekwenda na maji. Pia hela zinashawishi, sometimes you end up spending on unnecessary things. Otherwise kwa mfumo wetu wa Tz hakuna mtu ambaye angependa kuweka (achilia mbali kukopa fedha benki). Kimsingi mifumo ya kibenki kwa Tz inabakia kiama kwa wtz wengi. Kama mfano tu, rafiki yangu alikopa kiasi cha Tz mil 24, gharama za loan processing wakamkata Tzs .9mil. Huo mkopo analipa tz 745,000 kwa mwezi muda wa miaka minne (4). Zidisha 48monthsx745,000 unapata 35.8mil. Kwa maana nyingine kwkt miaka 4 mtu analipa almost Mil 12 kwa mkopo wa mil 24! Sasa ukija kwenye reality, unaona kuwa kwa mfumko wa bei tulio nao pengine benki za mikopo zipo sahihi....maana items (hasa za ujenzi) za kiasi cha mil 24 gharama yake kwa sasa ni zaidi ya 40milion! QuOTE=Kwetunikwetu;4278226]Nafikiri anaweza kuomba bank statement then aangalie hizo fedha zilitokaje......then afungue kesi ya madai dhidi ya benki. My experience kuna jamaa yangu aliwahi kulizwa 4,000 USD toka Barclays Uganda, alikomaa nao mpaka wakamrudishia. Sometimes hivi vijisenti ni bora kuvifungia ndani tu badala ya kuhangaika na mabenki uchwara
Kwa maelezo ya wadau hapa nimegundua kuwa NBC na CRD si slama kuweka pesa zako hko na hasa kwa watumiaji wa VisaCard na Master card. Nimeogopa.
Huu wizi upo jamani. Nimeshuhudia rafiki yangu alikuwa masomoni nje. Akawa amenunua credit skype. Basi baada ya muda kazaa wakakomba hela zake benk ya NBC. Akafikiri ni frauding ya kwenye mtandao ikabidi aulize benk. Alipofuatilia akakuta kwanza iliingizwa sh laki 8 kwenye akaunti yake halafu siku ya pili ikatoweka na hela yake pia akaambia ametumia hela kwenye suermaket huko nje wakati hajatumia. Alipewa bank statement akauliza hii laki 8 imeingizwa na nani? Maana kwenye statement haineshi nani kaingiza. Alianzia UDSM branch wakamzingua kwa majibu yasiyoeleweka. Akaenda makao makuu na corprate branch pale wakamwambia hapa pana tatizo, yule dada pale akataka kumsaidia lakini alipoenda kwa boss wake akachomoa. Jamaa akaambia aende samora branch ambako kuna kitengo cha mawasiliano. Pale samora alivyokuwa anaelezea akatokea mama mmoja mfanyakazi akawa anambinya yule dada kaunta. Tukaona hapa kuna mchezo ambao umefanyika. Yule dada wa kaunta akataka kutusaidia kwasababu aligundua kuna kitu pale, lakini yule mama akaja tena akamwambia yule dada hii kesi ngumu kidogo rafiki yangu aandike barua ili apewe majibu. Tukagundua kuwa huu mchezo ni wa wale wa samora mawasiliano, udsm branch na makao makuu. Kwahyo huu ni mchezo wa wafanyakazi wa benki