KUNA WIZI UMETOKEA BENKI KUU
Jambazi "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu",wote wakalala chini
HII INAITWA DHANA YA USHAWISHI-kubadilisha njia ya kawaida ya kufikiria
Kuna dada kwa woga akawa amelala chini kimitego,
Jambazi "dada embu kuwa na adabu chukua kanga jifunike hili ni tukio la ujambazi na sio la ubakaji.
HUU UNAITWA WELEDI-zingatia ulichofundishwa kufanya
Walipotoka kwenye wizi jambazi mdogo ambaye ana shahada ya uzamili ya biashara akamwambia mwenzake,"tuzihesabu hizi fedha,yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu,"wewe mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu saa mbili watatutangazia kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi gani.
HUU INAITWA UJUZI-Sikuhizi ujuzi ndio bora kuliko vyeti
Baada ya majambazi kuondoka meneja akamwambia mhasibu wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi".
HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI- kushabiihana na mazingira magumu kwa faida binafsi.
Mhasibu akafurahi na kusema,"dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana.
HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA-Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi
Meneja kafurahi sana kwakuwa sasa matatizo yake yametatuliwa na wizi uliojitokeza.
HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-shikilia nafasi psle inapojitokeza hata kama ni hatari kiasi gani
Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa millioni 100 umetokea leo benki kuu,
Majambazi kuskia hivyo wakaanza kuhesabu zila pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu.
Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema, "dah! yani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezesha msuli bora umeneja kuliko ujambazi".
HII INAITWA ELIMU- ishike sana elimu inanguvu kuliko dhahabu
MWISHO