Wizi ATM: Hatimae mwizi maarufu wa kwenye ATM anaswa na CCTV camera

ZionTZ

JF-Expert Member
Oct 6, 2009
1,283
541
Watu wengi husuani wamama na wababa wamekua wahanga wakubwa wa wizi wa mitandaoni pamoja na wa kwenye ATM, nilishuhudia mmama mmoja akilia kwa kuibiwa milioni moja kwenye ATM za bank jina kapuni, kinachonishangaza wizi huu unafanyika kwenye ATM kabisa mahali ambapo full time kuna askari analinda, sasa nashindwa kuelewa hawa askari hua hawawaoni hawa watu.

Haiwezekani mtu asie mfanyakazi wa bank kukaa ndani ya kichumba cha ATM akitoa msaada kwa wateja na askari asishtukie, moja kwa moja inaonyesha hawa watu wanamtandao wao fulani wa kupiga pesa. Tunaomba IGP S. SIRRO alivalie njuga hili suala, mtu kama huyu sio wa kuachwa abaki mtaani, mahali pake ni JELA kabisa. Pesa ilivongumu alafu mtu akuibie kirahisirahisi hivi. [HASHTAG]#HAIKUBALIKI[/HASHTAG].

Tazama video hii kwa usalama wako na mali zako, angalia jinsi anavojifanya anakusaidia kumbe anakuibia na kama huyu mtu unamjua mtaje hapa ili tuokoe ndugu zetu wengine.

Sijaona mtu akiiba nimeona mtu huyo huyo akisaidia watu,
Anabadilishia watu ATM card anazo nyingi, anajifanya anamsaidia mtukwa kuchukua ATM card yake na kuweka kwenye mashine nyingine ila haweki aliyoichukua kwenye mashine (haweki kadi husika) anaweka nyingine/haweki na kuziba na wallet ili anaesaidiwa asishtuke.......ukiangalia vizuri yeye hatoi hela kwenye mashine bali anazitoa kwenye wallet yake
 
Sijaona mtu akiiba nimeona mtu huyo huyo akisaidia watu,
Jamaa kwenye kipochi chake kwa chini ana kadi fake ya ATM,sasa anapojifanya anakusaidia faster anabadili kadi anakupa hiyo kimeo na kuchukua ya kwako.Wakati unahangaika nayo anasoma PIN then anasepa.Anaenda ATM sehemu nyingine kulamba mpunga.PIN anakuwa keshaisoma na KADI alikubambikia kimeo na kuichukua ya kwako nzima
 
Sasa kama anachukua hizo kadi namba ya siri anaipata wapi au wanamwambia mana pale sijaona wakizungumza zaidi ya kupewa kadi asaidie kuiingiza kwenye mashine.
Angalia anavyojibaragudha kumsaidia na kuhesabu hela mara nane nane huku macho yapo kwenye ATM. Yaani hapo ndio anakariri nywira ya mhusika.
 
Sasa kama anachukua hizo kadi namba ya siri anaipata wapi au wanamwambia mana pale sijaona wakizungumza zaidi ya kupewa kadi asaidie kuiingiza kwenye mashine.
Yaani jamaa haondoi mguu hadi mteja wake aweke pin code akiwa anachungulia mkuu. Angalia hapo
upload_2017-5-31_1-46-14.png
 
Pale anakuwa anakupumbaza ili uone kwamba yeye anajishughurisha na mambo yake na pesa si tatizo kwake
Na wewe lazima utahangaika kuingiza PIN mara nyingi sababu kadi si yenyewe so anapata wasaa mzuri wa kuisoma PIN yako.Target kubwa ni wamama
 
Angalia anavyojibaragudha kumsaidia na kuhesabu hela mara nane nane huku macho yapo kwenye ATM. Yaani hapo ndio anakariri nywira ya mhusika.
Daah. Ila nasikitisha saa nyingine baadhi ya watu wanaposhindwa kujishughulisha na kutegemea usanii usanii kwa kujipatia pesa ambazo hata hawajazitolea jasho.

Kwa muonekano wa nje kamwe huwezi kumdhania.
 
Na wewe lazima utahangaika kuingiza PIN mara nyingi sababu kadi si yenyewe so anapata wasaa mzuri wa kuisoma PIN yako.Target kubwa ni wamama
Mzee WA Liverpool bank yenu hii Exim nini au ni nbc maana vichumba vyao vinafanana fanana rangi...
 
Mimi binafsi nina mashaka na huyo jamaa na wahusika wote wa benk hasa wale wa usalama kupitia hizo camera za cctv. Kwanza kabisa huyo jamaa kwa mujibu wa video nilizozipata na kuziangalia kwa makini amekuwepo hapo ATM tena moja kwa nyakati tofauti kwa mfululizo wa siku tatu, kuanzia Alhamis, ijumaa na jmosi. Lkn cha kushangaza ni kwamba siku zote hizo wahusika wa benk hawajashtukia sijui camera zinafanya ninj au alikuwa na ubia na wahusika fulani wa benki ndio maana walimpotezea. Lkn cha kushangaza zaidi ni huyo aliyetumia simu kuchukua hizo scrip kwenye talakilishi na kuanza kuzisambaza alikuwa ana maana gani? Kwann hawakumuhisi huyu jamaa mapema kulingana na mazingira kwa mtu haruhusiwi kukaa ndani ya ATM. HAPO WAWAJIBISHWE MPAKA WAHUSIKA WA BENKI
 
Daah. Ila nasikitisha saa nyingine baadhi ya watu wanaposhindwa kujishughulisha na kutegemea usanii usanii kwa kujipatia pesa ambazo hata hawajazitolea jasho.

Kwa muonekano wa nje kamwe huwezi kumdhania.

Ivi awa watu wana roho gani unajua nashindwa kuelewa unamka asubui uende kuibia watu,..aseeh uu ni ugonjwa si normal ii,..
 
Sasa kama anachukua hizo kadi namba ya siri anaipata wapi au wanamwambia mana pale sijaona wakizungumza zaidi ya kupewa kadi asaidie kuiingiza kwenye mashine.
Akishachukua kadi yako anakubadilishia we ukiwa unahangaikaa kuchokonoa ye ndo kamaa hivyoo unavyomuona anazuga anapanga pangaa helaa kwenyee walet yakee akishafanikiwa kuiona yako anasepaa we huku kakadi kanamezwa sababu lazima utakuwa umeingiza no ya siri yakwako wakati kadi sio yako na yeye kashachunguliaa no ya siri anaenda ATM ya jirani anatindua mzigo. We ukija spid unatokwa povu kadi ikitolewa sio yako
 
Back
Top Bottom