Wizara zatakiwa kukaza mikanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara zatakiwa kukaza mikanda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ileje, Apr 13, 2012.

 1. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda amezitaka wizara zote kukaza mikanda kwa kuwa hakuna uwezekano wa serikali kukusanya mapato kama ilivyotegemea. Hali hii itaifanya baadhi ya miradi iliyopangwa kujengwa mwaka huu wa fedha kutokamilika.

  Aidha sababu nyingine ya serikali kushindwa kutimiza malengo yake ya kukusanya mapato kunatokana na nchi wahisani kadhaa na benki ya dunia kutotimiza ahadi zao za kuisaidia bajeti ya serikali.

  Source: TBC
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Wako wanapambana na maandamano ya CDM watakumbuka kukusanya kodi lini
  Ufisadi unaoendelea serikalini hawauoni yaani inakuwa kama fuko la serikali limeliwa na panya yaani wakikusanya mafisadi wameshatoboa mfuko inamwagika yote na kuchukuliwa
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Zito aliwahi kusema kuwa serikali imeishiwa
  Mkulo kasema Zito mwongo kabisa na serikali ina fedha za kutosha kwa mwaka mzima wa budget
  Wakandarasi kibao wa barabara wamesitisha kufanya kazi zao kwa maana hakuna fedha
  Dr magufuli anatutangazia kuwa wakandarasi wako kwenye site wanafanya kazi kumbe wameweka vifaa pale wakaacha wakarudi mjini kusubiri fedha
  Fedha za kwenda nje kutalii na kusema kuwa unaenda kutuombea fedha za kutusaidia zipo ila matunda ya hizo ziara hatuyaoni
  Afadhali amefunguka kusema kuwa wizara zifunge mkanda hali mbaya
   
 4. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Baadhi ya wizara hivi sasa ziko ICU! Mfano wizara ya maji miradi yote imesimama kwa kuwa Benki ya Dunia imegoma kuendelea kutoa fedha hadi serikali ieleze matumizi ya fedha ambazo zilikwishatolewa!
   
 5. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ila mbona fedha za ziara zao za kwenda kufungua vyuo na machinjio zopo sana tuu na wanakuwa na msafara wa magari ishirini kwenda kufungua mradi wa Milioni kumi wakati ukipiga mahesabu gharama za per diem na mafuta ya hizo gari zinatosha mradi mwingine kama huo
   
 6. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Yalisemwa hapa, tukapiga kelele sana bwana mkubwa na safari zake anafilisi nchi lakini hawakusikia
  Leo mnafunga mikanda kwamba mnazuia posho? Mishahara au?
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Hawajazuia chochote bado posho na marupurupu yao yako pale pale
   
 8. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Matumizi yanayokusudiwa kupunguzwa ni pamoja na matumizi ya magari kwa junior staff, office stationary na posho za lunch na overtime kwa junior staff!
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  Kwa junior staff tu na sio wote ?
   
 10. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Mawaziri, Makatibu wakuu, Wakurugenzi, Wakuu wa mikoa mwendo mdundo!

  Wakuu wa wilaya hoi wanakufa na tai shingoni!
   
 11. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  DENI LA TAIFA NI ZAIDI YA TRILLION 14....JK ameitumbikiza kwenye dibwi la umasikini mkubwa nchi hii
   
Loading...