Wizara ya Viwanda na Biashara inapaswa kuongozwa na mtu mbunifu kama January Makamba hivi, TRA iongozwe na mtu kutoka ndani

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Wakati wa vikao vya Bunge mwezi April, Godbless Lema alisema Waziri wa Viwanda na Biashara aliyetimuliwa juzi na Rais Magufuli Bwan.Kakunda hakuwa na uwezo wa kuongoza Wizara hiyo wala kuleta mwekezaji yoyote mkubwa kwa maana hata suti zake zilikuwa kama za mwanakijiji vile - hakuwa akijua kuvaa, hakuonekana kuwa ni "Mtu wa Biashara".

Sasa mimi nafikiri Rais Magufuli bado anakosea - bado anateua "wanakijiji" kuongoza Wizara hiyo ambayo ndo ilipaswa kuwa "marquee ministry" kwenye Utawala wake kwa sababu anatamani kuyafikia "Mapinduzi ya Viwanda", kitu ambacho si ndoto kukifikia kama akiota usiku badala ya kuota mchana kama ilivyo sasa...I mean, akisikiliza ushauri na kupanga safu yake vema atafanikiwa kutuongoza kuyafikia Mapinduzi ya Viwanda ikiwa Wizara hiyo atampa mtu ambaye akili yake ni njema na inafanya kazi sawasawa kama January Makamba hivi - mtu ambaye ni "outward" looking, outgoing, na mbunifu!

Mawaziri aina ya akina Kakunda na Kabudi kwa mfano, ambaye akisimama kuongea anaanza kusimulia habari za Wakoloni na TANU hawawezi kuwa na mchango wowote kwenye Vision ya Rais ya kujenga Uchumi wa Viwanda kwa sababu wana mawazo mgando...akisimama kuzungumza hata mbele ya Rais yeye huanza kupiga simulizi za Mabeberu, Vita vya Majimaji ,Vita Baridi na Ukomunisti wakati dunia ilishaondoka huko - Mtu kama Kabudi anaamini nchi kama Yugoslavia na Umoja wa Sovieti bado zipo hadi leo na anaamini pia Umoja wa Nchi zisizofungamana na Upande wowote(NAM) bado unaexist. Tunahitaji cabinet ministers wenye uwezo wa kuiona dunia kama ilivyo leo, dunia ya mahusiano mazuri ya biashara na uwekezaji, siyo dunia ya nyakati za Vita Baridi - tulikwishatoka huko!

Ushauri mwingine kwa Rais Magufuli ni aina ya watu anaowateua kuongoza Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA). TRA ni taasisi kubwa sana na ngumu kuiongoza - it is too huge and complex - ni ngumu sana kwa mtu anayeteuliwa kutokea nje kumudu kuiongoza kwa sababu anahitaji si chini ya miaka 5 hadi 10 kuifahamu - chini ya hapo hawezi kuelewa chochote wala kufanya mabadiliko yoyote yaliyo na tija zaidi ya kufanya vurugu tu za kuhamisha watu, kusimamisha kazi maofisa walio chini yake, kuwademote wengine na kuunda vikundi vya majungu....na ndiyo maana hadi sasa watu anaowateua kutokea nje wamekwishafika watano katika kipindi kifupi cha uongozi wake wakati Mkapa na JK walikaa na Comissioner General Harry Kitilya kwa karibu vipindi vyote vya Uongozi wao - yeye keshawajaribu akina Dr.Mpango, Maswi, Kidata, Kichere na sasa Mhede - CGs watano ndani ya miaka 3, a complete joke!

Wote hao anaona hawakufanya kazi aliyokusudia waifanye - lakini sababu ya wazi iliyokwamisha utendaji wao ni kwamba hawa ni technocrats tu and not career taxmen - Harry Kitilya aliweza kwa sababu ilikuwa ndo taaluma yake na hakutaka kuingiliwa na wanasiasa - alikuwa na uwezo wa kumgomea hata Rais akitaka afanye mambo yasiyoendana na taaluma ya ukusanyaji kodi/mapato!

Kwa hiyo ushauri ni kwamba Rais ateue Kamishna General kutokea ndani ya TRA, senior officers waliokaa mle miaka at least 10 hadi 15 ndo atafanikiwa - hii kuchukua watu kutoka huku na huko na kuwatupa kuongoza TRA ni kutwanga maji kwenye kinu!

Ushauri huu ni wa Bure, haulipiwi!
 
Emirates iliwahi kuwa na CEO Mwingereza; ndiye aliyelipaisha shirika kufikia hapo lilipo leo. The same applies to TRA, angeweza kutafutwa gwiji mbobezi (sio wa mishahada, sijui nini bali expert) wa masuala ya kodi hata kutoka nje ya nchi, afanyiwe usaili ikiwezekana wa wazi, ili aiweke taasisi katika mwelekeo unaoeleweka; vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu for ever and ever. NMB kama sijakosea walifanya hivyo. Hata hivyo, tahadhari ichukuliwe; haya mambo yasifanywe kisiasa kwa kurejea cases kama Net Group Solutions au TRL bali utaalamu.
 
Emirates iliwahi kuwa na CEO Mwingereza; ndiye aliyelipaisha shirika kufikia hapo lilipo leo. The same applies to TRA, angeweza kutafutwa gwiji mbobezi (sio wa mishahada, sijui nini bali expert) wa masuala ya kodi hata kutoka nje ya nchi, afanyiwe usaili ikiwesekana wa wazi, ili aiweke taasisi katika mwelekeo unaoeleweka; vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu for ever and ever. NMB kama sijakosea walifanya hivyo. Hata hivyo, tahadhari ichukuliwe; haya mambo yasifanywe kisiasa kwa kurejea cases kama Net Group Solutions au TRL bali utaalamu.
hauko serious
ukabidhi revenue authority ya nchi kwa foreigner???
 
Karibuni wadau hapa kina ya bwiru nafungua kiwanda cha nguo nnazo cherehani 5 c haba
 
Kamishna wa Custom Ben alifaa sana kuchukua nafasi hiyo ya Ukamishna Mkuu
 
Emirates iliwahi kuwa na CEO Mwingereza; ndiye aliyelipaisha shirika kufikia hapo lilipo leo. The same applies to TRA, angeweza kutafutwa gwiji mbobezi (sio wa mishahada, sijui nini bali expert) wa masuala ya kodi hata kutoka nje ya nchi, afanyiwe usaili ikiwezekana wa wazi, ili aiweke taasisi katika mwelekeo unaoeleweka; vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu for ever and ever. NMB kama sijakosea walifanya hivyo. Hata hivyo, tahadhari ichukuliwe; haya mambo yasifanywe kisiasa kwa kurejea cases kama Net Group Solutions au TRL bali utaalamu.
Brilliant, it is not a crime to hire a talent from outside ilimradi tu tahadhari na vetting ya kutosha ifanyike!
 
Back
Top Bottom