Wizara ya Ulinzi Uturuki: Tutaendeleza special operation kijeshi kaskazini mwa Iraq

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,475
99,169
Waziri wa ulinzi wa uturukii bwana HULUS AKAR akiongea JUMATATU asubuh kwenye briefing kuhusiana na kuanza operation Iyo anasema

"Hatutasimama, Tutaendeleza Hii special operation bila kikomo kaskazini mwa Iraq mpaka pale gaidi wa mwisho atakapomalizwa kabisa uwezo wake wa kijeshi"

"Special operation ya Uturuki ndani ya kaskzini mwa Iraq iliyoanza mnamo jumapili tayar ishaanza kufanikiwa Katika utekelezaji wake wa malengo yake ya awali uku majeshi yetu yakiwalenga zaidi majeshi ya wakurdi ndani ya iraq"

" Usiku wa kuamkia leo, jeshi letu limeripoti kuwauwa idadi kubwa ya majeshi ya wakurdi pamoja na kuharibu kambi zao pamoja na shehena zao za silaha mbalimbali, ambapo kwa mwanZo huu Unaweza kusema malengo yetu tayar yameshaanza kufanikiwa"

Waziri uyo aliongeza kua special operation hiyo itaendelea na utekelezaji wa malengo yake mpaka pale gaidi wa mwisho nchini iraq atakapomalizwa kabisa uwezo wake wote wa kijeshi.

Wizara ya Ulinzi Uturuki imesema pia itaendelea kufatilia na kutoa taarifa za kila Mara katika mwendelezo wa special operation ndani ya iraq iliyopewa jina rasmi la OPERATION CLAW-LOCK mnamo asubuh ya jumapili

Kutokana na maelezo ya wizara ya Ulinzi Uturuki, majeshi ya Uturuki yameharibu makazi,mahandaki, mapango ,maghala ya silaha na mafuta pamoja na vituo kadhaa vya kutoa amri za kijeshi vya Iraq.

Vikosi kadhaa vya mabomu vya majeshi Uturuki vimeshiriki mashambulizi makali ya mabomu kaskazini mwa Iraq usiku wa kuamkia JUMATATU kwa kutumia ndege za kivita.

Wizara ya Ulinzi uturuki imesema Hii special operation imewalenga zaidi wafuasi wa wakurdi nchini iraq ambao wamekua na mgogoro wa mionho kadhaa na jamii ya Ankara nchini Uturuki. Wafuasi hao Ni jeshi ya msimamo mkali was wakurdi PKK, chama Cha wafanyakazi Cha wakurdi (KWP) pamoja na jamii ya wakurdi mamluki wenye msimamo mkali kutoka nchini Syria YPG. Ambapo vikundi vyote hivyo serikali ya Uturuki imevitambua rasmi Kama vikundi vya kigaidi na vinavyotishia USALAMA was nchi ya uturuki.

Waziri huyo aliongezea pia kwamba
"Serikali ya Uturuki imefanya jitihada kubwa Sana za mazungumzo ya kumaliza mzozo huu kwa mionho kadhaa na vikosi vyote vya kikurdi ndani ya iraq pamona na nchini Syria Bila mafanikio yoyote."

"Tulichoamua na majeshi yetu Sasa ni kufanya operation Kali ya kijeshi kuvimaliza vikundi vyote vya kikurdi nchini iraq pamoja na nchini Syria. Na Operation zilizopita ndani ya iraq tumefanya mikoa ya metina, Zap, na avasin-basyan."

"Jamii ya Watu wetu wa ankara wanataka Uhuru wao wa kiitikadi kutoka kwa jamii ya wakurdi ambao Ni haki Yao kutokana na kuzingatia matakwa na masharti ya vifungu mbalimbali vya umoja wa mataifa vinavyolitaka taifa lolote kujilinda dhidi ya Uhuru wake binafs, yaani UN CHARTER for National self defense clauses"

"Special operation Hii inafanyikwa kwa kuwalenga zaidi vikundi vya kigaidi na kwa njia ambayo inaheshimu sheria za kimataifa katika masuala ya utu wa kibinadamu, misaada ya kibinadamu,mateka wa kivita pamoja ana Uhuru binafs wa kimamlaka wa taifa la Iraq"

" Tunapenda pia kuwawaonya Sana mamluki wowote kutoka Syria na pande zozote zile za dunia kutokuingilia operation Hii, hatutakua na chembe ya huruma nao punde TU watakapotia mguu katika special operation hii"

"Nisistize Tena kwamba operation hii inafanya kila linalowezekana kuepuka kuwadhuru Raia wa kawaida, maeneo ya kitamaduni na kidini pamoja na mazingira na majengo ya nchi ya Iraq. Wito wangu wangu Ni majeshi ya kigaidi ya wakurdi ni wasiwatumie raia wa kawaida, maeneo na majengo ya kidini au kiutamaduni Kama ngao Yao ya kivita katika kupambana na majeshi ya Uturuki"

Source: RT

Screenshot_20220419-133711.jpg
 
Sijajua umoja wa mataifa wanalizungumziaje suala la Uturuki kuivamia Iraq,

Naona vyombo vingi vya magharibi viko kimya kuhusu Hii habari, inafikirisha sana
Wakiongea mnasema ni propaganda, wasipoongea mnasema inafikirisha. Acha watu waoneshane makali.
 
Sijajua umoja wa mataifa wanalizungumziaje suala la Uturuki kuivamia Iraq,

Naona vyombo vingi vya magharibi viko kimya kuhusu Hii habari, inafikirisha sana

Unakumbuka walipomshambulia Saddam wakati ule?
Majeshi ya na washiriki waliiba sana mali za Iraq kuanzia artifect zote za zamani sana zingine zikiwa na miaka zaidi ya 3000 zikaonekana zikiuzwa NY, London na Paris ushuhuda upo

Then wakaanza kuiba mafuta na kuyapitisha uturuki nalo linajulikana wameiba sana na Turkey ni washiriki katika wizi
 
Dah! Hii Dunia ina mengi ya Siri Sana,
Inavoonekana hata magaidi Ni visingizio kuhalalisha ujambazi wao
 
Unakumbuka walipomshambulia Saddam wakati ule?
Majeshi ya na washiriki waliiba sana mali za Iraq kuanzia artifect zote za zamani sana zingine zikiwa na miaka zaidi ya 3000 zikaonekana zikiuzwa NY, London na Paris ushuhuda upo

Then wakaanza kuiba mafuta na kuyapitisha uturuki nalo linajulikana wameiba sana na Turkey ni washiriki katika wizi
Hakika mkuu.
Screenshot_20220412-002702.jpg
 
Sijajua umoja wa mataifa wanalizungumziaje suala la Uturuki kuivamia Iraq,

Naona vyombo vingi vya magharibi viko kimya kuhusu Hii habari, inafikirisha sana
Akifa wanayemtaka ndio shida utaskia hata mbongo wa mbagara anabwabwaja.
Lakini akifa wasiyekuwa na time naye ni sawa na mbongo wa mbagara hata kama aliyekufa ni jirani yake hutomsikia.
Wazee wa we stand with paris 😀😀
 
Back
Top Bottom