Mzee wa Kwembe Kati
Manyerere Jackton pamoja na maelezo yako marefu lakini bado hujaweza kutushawishi kwamba hakuna mkono wa Muhongo na Maswi katika mkutano wenu ambao utaambatana na tamasha la michezo ambalo mmeliandaa kulifanya baada ya kumaliza kuseminika hapo Ntwara.
Jambo moja ambalo ni muhimu kulitambua ni kwamba wahariri wa vyombo vya habari hapa nchini miongoni mwao kuna ambao wanafahamika kwa kupokea rushwa au ukipenda iite bahasha kwa lugha yenu wanahabari.
Tunafahamu kuna wahariri wasafi kabisa wanaofanya kazi yao kwa weledi lakini pia tunafahamu wapo wahariri njaa kali wao bila bahasha nene hakieleweki na hilo ndilo wamelifanya Muhongo na Maswi kuhakikisha kwamba wanawatumia kuficha madhambi yao ya kugawa gesi ya watanzania kwa wazungu wa Norway tena kwa haraka haraka wakati bado nchi hatujakuwa na sera ya gesi.
Kama kweli wahariri wa vyombo vya habari msingekuwa mnaendekeza matumbo yenu mngekuwa mmelipigia kelele suala hilo lakini kwakuwa mmeamua kuwasaliti watanzania ndio maana mmeamua kulala kitanda kimoja na serikali yenu sikivu.