Wizara ya Maliasili hili ni tatizo

Upekuzi101

Senior Member
Aug 28, 2020
134
348
Habari wana JF,

Kumekuwa na tatizo kubwa Sana hasa kwenye wizara ya Mali Asili na utalii. Wizara ya Mali Asili na utalii inaonekana kama kila mtu yupo huru kuamua kuamka tu na kuweka tozo, gharama na malipo ambayo inaonekana hakuna wa kuhoji uhalali wake au umuhimu wake.

Kuachilia mbali kuwa mtalii anapokuja Tanzania analipa kodi kupitia visa yake na gharama nyingine ukijumuisha, malazi, usafiri, Chakula pamoja gharama za safari kwa wale wnaotembelea mbuga zetu, kote huku Serikali inapata mapato yake bila kipangamizi.

Pamoja na yote haya sasa hivi unapopita wilaya ya Siha na mgeni kwa maana ya mtali ukiwa na gari yoyote lazima ulipe tena.

Wamejianishia tozo zao wameweka hapo wanasubiri kutoza watu. Naomba wizara ya Mali Asili na utalii angalieni hili na kulikemea pia kwa sababu huu utaratibu utakuja kuwa ndio utamaduni wa watu kuamua kulipisha tu makodi yasiokuwa rafiki kwa biashara bila Serikali kujua na wakati mwingine hata hayo mapato kutofika Serikali.

Hili lilijitokeza halina mantiki wizara ya Mali Asili na utalii toeni tamko kuhusu hili maana halina mwisho mzuri wala halimfaidishi yoyote zaidi ya kuumiza biashara ya Utalii maana inaonekana ndiyo sekta kila mtu anaweza Kuja kuchuma tu pesa burebure kwa kutumia vifungu vya sheria ambavyo havina maslahi yoyote kwa Mtanzania.

IMG-20230119-WA0009.jpg
 
Boss ni kwamba, sie tunajisemea tu kwamba hatuna na hatuzihitaji Serikali za Majimbo. Lakini ukweli ni kwamba ukichimba kwenye misheria yetu huko ndani, utagundua tunatekeleza sera ya Serikali za Majimbo kiaina. Kama ulikuwa hufahamu boss ni kuwa, kupitia sheria za Local governments, hizi Serikali za mitaa zina mamlaka kupitia Baraza la Madiwani na kubarikiwa na Waziri wa TAMISEMI kutunga sheria ndogo za Halmashauri.

Kwahiyo unaweza kukuta kuna sheria inaitambua mamlaka fllani ya Serikali kuu kuweka utaratibu wa jambo flani, meanwhile, na Local governments wakajiwekea kautaratibu kao. Kwa ufupi huo ndo uhalisia wa kwenye ground Chief kama ulikuwa hujui nimekudokezea kidogo.

Nyongeza kidogo. Hapohapo ukumbuke kuwa Halmashaui huwa zinapigishwa jaramba zitanue wigo wa kukusanya mapato, na wasipofikia target flani wanatishiwa kufutwa. Kwahiyo hapo DED + BARAZA la Madiwani lazima wachachamae kutafuta vyanzo vya mapato hata mahala ambako hapakuhitajika kwao.
 
Sasa unalaumu wizara bure
Hizo naziona ni by law..kwa kawaida hizo sheria ndogo wamejitungia wao halmashaur baada ya kuona labda kuna mapato ya sekta ya utalii au wamepitia act labda wameona ipo haja.
 
Back
Top Bottom