kabwigwa
JF-Expert Member
- May 17, 2014
- 933
- 1,543
Habari wanajamvi,Juz Kati nilitaka kusafirisha mzigo wangu ambao ulikua Ni zawadi kwa Jamaa Yangu ambaye anaishi nje ya nchi.Ilikua Ni kinyago kimoja Na frem ya picha yenye vinyago vidogo ndani.Nilipofika posta nikaambiwa natakiwa nipate kibali kutoka Mali asili Na utalii,nikahoji Mimi sio mfanyabiashara hizo Ni zawadi Tu iweje niwe Na kibali nikaambiwa niache ubishi Kama nataka kusafirishiwa mzigo bas nifuate kibal wizarani.IKabidi nitoke mpaka wizarani ,nimefika wizaran saa nane Na nusu,nikaambiwa muda wa kazi imeisha nirudi siku ya pili.Nikahoji iweje saa nane Na nusu iwe mwisho wakadai ukifika huo muda hawaruhusu wagen kuingia wizaran.Siku ya pili nikaenda wizaran nikaelekezwa utaratibu kuwa nilipie 87,300 , nikahoji kwanini nilipie wakati Ile Ni zawadi Tu kwanini kusiwe Na kiwango labda kuanzia idadi Fulani ya vinyago ndo mtu alipie hicho kibali?Nikaambiwa huo ndo utaratibu wao.IShu ikaja kwenye malipo,unalipia kwa nmb,Crdb Na mpesa. Nikaenda Crdb akaunt haijawa activated,fikiria unakaa bank said ya saa moja Na nusu then unakuja kuambiwa akaunt Ni inactive.Nikarud wizaran wananiambia ungetumia nmb Na M-PESA,Crdb bado haifanyi kazi.Ikabidi niende nmb nikalipie,Kama mnavyojua folen za NMB siku ikapotea tena.Siku ya tatu ndio nikafanikiwa kupata hicho kibali Na kutuma mzigo wangu.Thamani ya vitu nilivyotuma havizidi 20,000 lakin kibali kina cost 87,000 is it fair?Najiuliza Ni watalii wangap wanaacha vinyago vyao airport kwa utaratibu mbovu Kama huu?Mgeni anaenda kutoa sifa gan huko kwao?Tutalalamika utalii haukui kisa vitu vidogo Tu vinatuharibia sifa kimataifa.Huwez nunua kinyago 10,000 then kibali ulipie 83,700 Ni upuuzi mtupu.ushauri WA bure jitangazeni kimataifa Na sio kuleta tozo zisizo Na mana hakuna ubunifu.Maonesho ya Sabasaba mliamua kututoza 1000 licha ya kile kiingilio cha kawaida hamkuwa fair hata kidogo watu wenu wa marketing sidhani Kama wanafanya kazi ipasavyo.
Muwe Na jion njema.
Muwe Na jion njema.