beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Serikali imechukua tahadhari ili kuhakikisha nzige wa jangwani ambao ni tishio kwa mazao ya chakula na nyasi hawaingii nchini na kuleta madhara kwa wakulima na wafugaji, ikizingatiwa kuwa Tanzania inapakana na nchi zilizoathiriwa na wadudu hao.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya aliliambia HabariLEO kuwa, kutokana na hofu iliyokumba baadhi ya wakulima katika mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Kilimanjaro kutokana na kuibuka makundi makubwa ya wadudu waliodhaniwa kuwa ni nzige.
Alisema baada ya wizara yake kupata taarifa hizo ilipeleka wataalamu wake katika mikoa iliyoripoti wadudu hao hususani katika wilaya za Korogwe mkoani Tanga, Mwanga mkoani Kilimanjaro na Ilala jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo Kusaya alisema uchunguzi wa wizara ulibaini kuwa wadudu hao si nzige kama wananchi walivyodhani, bali ni panzi wanaofanana na nzige wasio na madhara katika sekta ya kilimo.
Alisema wadudu hao mara nyingi hujitokeza kila mvua zinaponyesha na imekuwa kawaida katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro kujitokeza kwa makundi katika vipindi vya mvua za vuli pamoja na za masika.
“Mpaka sasa serikali haina taarifa yoyote ya uwepo wa nzige wa jangwani nchini, hao walioonekana katika mikoa hiyo ni panzi wa kawaida ambao si tishio kwa mazao ya kilimo,”alisema.
Kwa mujibu wa katibu mkuu huyo, baada ya taharuki ya wananchi kutokana na uwepo wa wadudu hao na baada ya kujiridhisha kuwa hawana tatizo, wizara iliamua kutuma maofisa wengine kwa ajili ya kuwadhibiti ili kuondoa hofu kwa wananchi.
Hata hivyo, Uongozi wa Mtaa wa Buguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam kulikokutwa makundi makubwa ya panzi, ulifikia maamuzi ya kuteketeza mazalia ya panzi hao ili kuondoa hatari inayoweza kulikabili eneo hilo katika siku za baadaye.
Viongozi wa mtaa huo walitumia moto kuteketeza mazalia ya wadudu hao ili kuweka mazingira salama ya wakulima wa mbogamboga katika eneo hilo linalozalisha mbogamboga kwa wingi katika jiji la Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Buguruni Kisiwani, Uwesu Uwesu, aliwatoa hofu wananchi na wakulima wa eneo hilo akisema wadudu hao watadhibitiwa ili kuondoa hofu iliyotanda kwa wananchi kuhusu hatari inayoletwa na uwepo wa wadudu hao.
“Hapa walikuja wataalamu wa Wizara ya Kilimo wakatuthibitishia kuwa wadudu hawa si nzige wa jangwani, bali ni panzi wanaofanana na nzige ambao hawana madhara kwa mazao ya wakulima,” alisema Uwesu.
Aliongeza kuwa, baada ya wataalamu kutoka wizarani kuwaelimisha kuhusu wadudu hao, waliwaita watu wa kupulizia sumu hali iliyowafanya wadudu hao kufa, ingawa baadaye lakini baadaye wakagundua kuwa wadudu hao walilikuwa wametaga mayai mengi.
Mkulima katika Wilaya ya Mwanga, Msami Mkwizu alithibitisha kuwepo kwa wadudu hao katika kata za Kifaru, Kileo, Usangi na Ugweno huku akisema kwa wakulima wazoefu wanawajua wadudu hao lakini kwa wakulima wapya walipata hofu na kiwewe wakidhani ni Nzige walioko Kenya.
Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu kati ya nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo hazijaguswa na nzige wa jangwani tangu mwaka jana mpaka sasa. Nchi nyingine ni Rwanda na Burundi ambazo nazo hazijaripoti uwepo wa nzige wa jangwani katika maeneo yao.
Nzige wa jangwani walianzia katika nchi za Ethiopia, Sudan Kusini na Somalia na kuenea katika nchi ningine kama Eritrea, Kenya, Uganda na nchi za Mashariki ya Kati kama vile Saudi Arabia, Yemen, Pakistan na India.